Njia ipi ya Mpango wa uzazi ni bora kwa wanandoa?

Kumekuwa na dhana mbalimbali nyingine potofu juu ya njia bora za uzazi. Wengine wanaogopa kutumia kondomu kwa sababu tu zinatumika na vijana wazinifu.

Wengine wanaogopa kutumia vidonge eti vinaongeza makalio au cancer.

Sasa ebu tuambiene kwa wanandoa ipi ni njia bora ambayo haina madhara kiafya wala kimaadili.

1. Kondom
2. Sindano
3. Vidonge
4. Vijiti

Hizo ndio ninazo zifahamu kwa sasa kwa kujisomea kwenye vijitabu.

View attachment 1720486
Hakuna njia salama ya uzazi wa mpango kati ya hzo ulizoztaja...
 
Mbegu za rosary
Kuzika kitambaa cha damu ya hedhi kikiwa ndani ya chupa
Nk..

Hizi ni kiasili na mambo ya vijijini kwetu a.k.a mila potofu ili kijiji kwetu bdo znafanya kazi!!?
 
Kidogo ufafanuzi hapa mkuu.
Hususan ukitumia Copper IUCD (Cu-IUD) hiki hakibebi homoni yoyote , kwahiyo Mama hatokumbwa na shida ya Hormonal imbalance.

Nahii husaidia uzazi kurudi muda mfupi tu baada ya Mama kuondoa kitanzi anapohitaj kuzaa.

Tofauti na Njiti, vidonge ambavyo hupelekea kutokuwepo na usawa wa homoni, nahii humlazim mama kukaa miezi karibu sita au zaidi homoni kurudi sawa na yeye aweze kubeba mimba.

Lkn pia, kwa uzoefu wa kikazi , , njia za uzazi mpango zinazotumia Homoni, zimechochea kwa kiwango fulan ongezeko la akina mama kuzaa watoto wenye Congenital abnormalities .....(Huu ni utafiti wangu usio rasimi kupitia uzoefu wa kikaz )


Kwa hiyo kuepukana nayo, kwasasa binafsi napendelea kuwashauri akina mama kutumia Cu-IUD .
 
Yani ulale na mke wako then ndomu ihusike? Never aisee, kalenda.... withdrawal method haiwezi kumuangusha mja hata siku moja.
 
Kuna maali nimewambia, hata katone kamoja kanatosha kubebesha mimba.

Kuna ule ute wa mwanzo unaotoka kabla ya kumwaga.

Huo nao husababisha mimba.
Du unasema kweli mkuu?maana nilitaka niwashe moto kwa wife nilikuwa namlia tyming tu ili nilianzishe na uzee huu
 
Dunia hii ya ajabu sana, kuna wengine wanatafuta lakini mimba inagoma, wewe katone tuu kamoja kanaharibu mambo
Unaambiwa leo salama kabisa tupia, unacheza kandanda safi unakuta umetipa nyavu mzee, zinaanza unajua sijaona siku zangu , na huu uchumi ulivyo unaanzaje kuwa na team ya mpira
 
Back
Top Bottom