Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,200
- 55,837
Habarini Great thinkers wote.
Lengo la uzi si kumtoa mtu kwenye imani yake
"Religion is an opium" sote tunakumbuka hii tulisoma kipindi cha sekondari,tena namkumbuka yule mwalimu wangu wa GS pale shuleni.Hii sentensi sio tu kwenye religion hata kwenye kuamini vitu mbalimbali.
Ili maisha yaweze kuwa na maana lazima mtu awe na kitu cha kuamini, waislamu wanaamini wataenda peponi, wakristo vivyo hivyo,wengine wanaamini wakifa watafufuliwa tena, wengine wanaamini ukifa ndio basi tena. Kile mtu anachoamini akilini mwake ndio kinakuwa foundation ya kila kitu anachofanya hapa duniani,kwamba matendo yake yote atafanya ili aweze kutimiza malengo ya imani yake.
Imani inawemfanya mtu aamini kitu kimoja kwa kiwango ambacho kitafanya asiamini vitu vingine ambavyo haviendani na kile anachkiamini.Muda mwingine wengine wanaenda mbali zaidi mpaka wanafikia hatua ya kuona wengine ambao wana imani tofauti na wao kama maadui au wanepotea(extremist,msimamo mkali)
Katika jamii tunayoishi kila mtu ana imani yake na vitu fulani.Mfano wakristo,waislamu,wahindu etc.
Lakini sote tunafahamu kila kitu lazima kifanyike kwa kiasi fulani (na usahihi) laa sivyo kinakuwa kama Addiction au hatari kwa maisha ya muhusika.
Kipindi nasoma Sekondari kuna mshikaji wangu alikuwa vizuri tu form ,ila mpaka anafika form six urafiki wetu ulikufa baada ya yeye kuwa amejiingiza kwenye imani above average,alikuwa anashinda msikitini,analala huko,ansomea huko,na matokeo ya form six hakufaulu.
Mbaya Zaidi mtu ambaye yuko kwenye Imani fulani ni ngumu sana kumuelimisha au kumrudisha kwa njia ya kumuelewesha kwa maana kwamba imani yake inamwambia yeye yuko sahihi kuliko wewe.
Mfano.Kuna watu huwaambii kitu kuhusu mwamposa, wale wanaojitoa muhanga,Mackenzie,Kibwetere,ijapokuwa unajua kabisa wamejazwa imani mbaya au wanatapeliwa,kibaya zaidi watakushawishi wewe uungane nao pindi unapojaribu kuwaelimisha.
Swali,Je ni njia gani inafaa kwa ajili ya kumtoa mtu huko?