Njia ipi nayoweza tumia kusafirisha mifugo kwenda Zanzibar

Kwa njia ya maji kuna meli za mizigo za aina mbili Azam sea link na sea star. hizi unaweza safirisha hivi.
Ukawapakia mifugo yako kwenye gari lako then gari likaingia kwenye meli hadi zanzibar ukifika unawasha ndinga yako unaenda fanya delivery sehemu husika au

Ukawaambia jamaa wakapakia mifugo kwenye gari zao then wakagikisha mpaka sehemu husika hizo meli zina siku zake za kwenda sio kila siku. Meli inaondoka saa nne usiku saa 12 asubuhi inakuwa imefika.

Kuhusu nyama unaweza safirisha kwa meli hizi au
kwa zile speed boti ambazo zinachukua saa moja na nusu tu na zinaenda kila siku
Kuna boti za aina mbili Azam kilimanjaro na Zanzibar one/zanzibar two
Choice ni ya kwako bei hazipishani sana.

Muhimu zaid fika ofisini kwao kwenye kampuni hizi zote mbili wakupe maelezo then wewe mwenyewe utaamua.

Ofisi za hizo kampuni zote mbili zipo posta bandarini pale ile bandari ya kwenda zanzibar.


Kuna njia nyingine ya magendo hii utasafirisha nyama kwa jahazi. Majahazi yanapatikana bagamoyo kule fanya ukavizie upate connection.
Wanasafiri mida ya saa tano sita saa 10 wapo Zanzibar wanapakua.
Magendo yana risk nyingi ila ndio sehemu ya kujitajirisha hapo maana utakwepa gharama za usafiri na kodi za hapa na pale

Choice ni yako

All the best kuelekea uchumi wa buluu
 
Kwa njia ya maji kuna meli za mizigo za aina mbili Azam sea link na sea star. hizi unaweza safirisha hivi.
Ukawapakia mifugo yako kwenye gari lako then gari likaingia kwenye meli hadi zanzibar ukifika unawasha ndinga yako unaenda fanya delivery sehemu husika au
Nakushukuru sana ndugu yangu kwa maeelzo fasanani,nimepata mwanga na sasa najua wapi pa kuanzia. Asante sana Mkuu.
 
Wadau wasalaam

Nimepata tenda ya kupleka Ngombe na Mbuzi Zanzibar kutokea Dar es alaam. Naomba ushauri njia ipi nayoweza tumia kusafirisha mifugo(ikiwa hai) na pia kusafirisha kama nyama ikiwa imechinjwa.

Ahsante.
je hawa mifugo unawatoa mkoa au mikoa gani?
Tanga kuna Meli kuba ya miziko ya Azam, ndio wasafirishaji wakubwa wa mazao ya shambani kwenda Pemba na Unguja.
 
Na mm naombeni ushauri kuhusu kodi hapo kwenye boat za azam nataka kusafirisha Maziwa ila sijui kodi zina tozwaje ili nipige hesabu kama kuna faida .. Maziwa kwa madumu je mzigo unatozwaje nauli na kodi inatozeaje..

asanten
 
Angalizo:Kuna mtu mmoja alianza biashara hii--yeye alikuwa akisafirisha Ng'ombe kwenda ZNZ kwa kutumi Mashua.Msafirishaji alidai Ng'ombe wale walianza kupigana na mifugo wengine kwenye chombo na mawimbi yalikuwa makali mno---kati ya ng'ombe wake 20 walibakia wa3 tu!
 
Nakushukuru sana ndugu yangu kwa maeelzo fasanani,nimepata mwanga na sasa najua wapi pa kuanzia. Asante sana Mkuu.
Pia inatakiwa uwe na kibali kutoka wizara ya mifugo Cha kusafirisha nyama, hiki utaenda kulipia pale Temeke Veterinary. Kama hauna itabidi umtafute mtu mwenye kibali utumie chake na utampa pesa ya maji.

Kuna pesa utalipia Kwa bandari unapeleka mzigo kwenye meli itakipwa Kwa ukubwa wa mita za mraba wa mzigo( Cubic Metres -CBM) na Kodi kama ipo basi utakadiriwa na mtu wa customs.
 
nami nataka kufahamu nikiwa nasafirisha mbaazi kwenda znz napata kibali wapi na nifanyaje wakuu nisaidieni hili?
 
Back
Top Bottom