Njia hizi zitakurahisishia usafi jikoni na kuweka jiko lako safi bila bacteria

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
1618138343371.png

Njia hizi zitakurahisishia usafi jikoni na kuweka jiko lako safi bila bacteria

1. Tumia chumvi na ndim kusafisha ubao wa mbao wa kukatia vitu jikoni. Mwagia chumvi kwenye ubao halafu sugua na ndimu.

2. Safisha tray zako za kuchoma kwenye oven kwa kuchanganya nusu kikombe maji na nusu kikombe baking soda iache ikae kwa muda wa saa halafu sugua na sponge au brush.

3. Safisha sufuria yako iliyoungua kwa kuchanganya kikombe 1 baking soda na kikombe 1 vinegar uchemshe kwenye moto mkali. Ikishachemka iweke kwenye sink uwekee vijiko 2 vya chakula baking soda. Sugua na sponge au brush na sufuria yako itatoka alama ya brown ya kuungua.

4. Ukitaka alama ya chai na kahawa kutoka kwenye vikombe mwagia baking soda kwenye kikombe halafu wekea maji kidogo ifanye nzito. Sugua na brush taratibu na itatoa alama zote.

5. Kama sink lako la jikoni lina toa harufu mbaya na limeziba mwagia jagi zima ka maji ya moto yaliochemshwa vizuri halafu mwagia kikombe cha baking soda kwenye tundu la sink sehem maji yanapopita. Halafu mwagia kikombe cha ndimu itaanza kufanya mapovu. Mwagia tena maji ya moto na sink lako litakuwa safi.

6. Kama microwave yako ina mafuta mafuta unaweza kusafisha kwa kuweka nusu kikombe cha maji kamulia limao 1 na tupia ndani limao ulizokamua halafu iweke ndani ya microwave uwashe moto mkali kwa dakika 3-4. Iache kwa muda wa dakika 5 mvuke usambae ndani ya microwave halafu fungua ufute kwa ndani.

7. Kama una chombo cha udongo kimevunjika na umeshindwa kuokota vigae vidogo sana unaweza kuweka mkate wa boflo juu yake na kuubonyeza , vile vigae vidogo vitaganda kwenye mkate.

8. Safisha jagi lako la blenda kutoa alama na harufu kwa kuweka nusu ya jagi maji ya vuguvugu, drop ya sabuni ya kuosha vyombo na maji ya ndimu au vinegar halafu saga.

9. Wekea maji kitambaa chako au taulo la kusafishia counta ya jiko weka kwenye microwave kwa sekunde chache lipate moto halafu futia counta inasaidia kutoa mafuta na uchafu kirahisi.

10. Kusafisha alama ya brown kwenye vikaango chini jaza sinki maji ya moto na baking soda halafu roweka kikaango kwenye sinki kwa dakika 15-20. Sugua na steel wire na osha. Unaweza kurudia ikiwa alama sugu.

Pia soma: Rahisisha maisha, tumia njia hizi zitakuondolea usumbufu
 
Mkuu kwa Jinsi ulivyoepeza kuhusu baking Soda.Hii kitu haifai kabisa kuila/ kutumia kwenye upishi.
 
Asante kwa haya madini Chef, baking soda hua ni msaada sana jikoni na kwenye mambo mengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom