Njia Gani sahihi ya kutoa nguvu za giza kwa mtu aliyerogwa?

Mel James

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
344
241
Naomba kuwasilishia mada yangu Kama inavyosema kwenye kichwa cha habari. Naombeni mnijuze njia sahihi ya kutoa nguvu za giza au uchawi kwa mtu ambaye amerogwa.

Waganga wa kienyeji hapana kabisa na wachungaji wala kuombeana hapana. Nisaidie njia nyingine ambayo itanisaidia.

Natanguliza shukrani za dhati kwenu.
 
Naomba kuwasilishia mada yangu Kama inavyosema kwenye kichwa cha habari. Naombeni mnijuze njia sahihi ya kutoa nguvu za giza au uchawi kwa mtu ambaye amerogwa. Waganga wa kienyeji hapana kabisa na wachungaji wala kuombeana hapana. Nisaidie njia nyingine ambayo itanisaidia. Natanguliza shukrani za dhati kwenu.

Only evil book can undo what the evil has done.
 
Naomba kuwasilishia mada yangu Kama inavyosema kwenye kichwa cha habari. Naombeni mnijuze njia sahihi ya kutoa nguvu za giza au uchawi kwa mtu ambaye amerogwa. Waganga wa kienyeji hapana kabisa na wachungaji wala kuombeana hapana. Nisaidie njia nyingine ambayo itanisaidia. Natanguliza shukrani za dhati kwenu.
kwanza Unawezaje kujua kuwa umerogwa mkuu
 
Njia nzuri ni kupiga NYUNGU. Hakuna kinachoshindikana katika nguvu ya NYUNGU
 
Sangoma anapata hicho kipaji kutoka ulimwengu wa roho! Amin amin nawaambie "uchawi Upo na waganga wapo " Ukishikwa shati wewe gonga kipepsi kilichoshiba hata uondoe meno yote ashike adabu. Mambo ya kumuachie Mungu ni danganya toto!
 
Njia sahihi ambayo hata mimi naitumia ni kutokuamini uwepo wa hivo vitu. Wewe amini hamna vitu kama hivo.
Wewe inaonekana pia hujui vitu hivi vinakuathiri vipi.

Pili,hii si njia sahihi sababu haizuii wewe kupigwa kiraba au kipapai.

Tatu, utaamini vipi kutokuwepi kwa vitu hivyo wakati vipo ? Huoni unajidanganya na umeamua hilo.

Nne, mimi nataka nikuroge wewe, kisha utakuja kuwapa habari wadau humu.
 
Wewe inaonekana pia hujui vitu hivi vinakuathiri vipi.

Pili,hii si njia sahihi sababu haizuii wewe kupigwa kiraba au kipapai...
Wewe unatambuaje uwepo wa kitu?
Hizo nguvu za giza umeshawahi kuziona?
There, Niloge sasa hivi.
 
Wewe unatambuaje uwepo wa kitu?
Hizo nguvu za giza umeshawahi kuziona?
There, Niloge sasa hivi.
Jibu la swali la pili :
Maumivu ya Moyo ushawahi kuyaona au Njaa ushawahi kuiona ? Kutokuliona jambo au kulidiriki hakumaanishi ya kuwa halipo au halikuwepo ? Ushawahi kumuona babu yako wa kumi ? Kipi kinakufanya uamini ya kuw alikuwepo ? (Swali hili utalijibu baada ya kujibu swali la kabla yake)

Jibu la swali la kwanza :
Natambua uwepo wa kitu kwa njia nyingi, na hizi ni chache :

1. Shuhuda za watu wa kweli awe mmoja au zaidi.
2. Maandiko matakatifu kwayo yaliyosalimika na mikono ya watu.
3. Akili
4. Uhalisia

Tatu, sahihi ni "Niroge" na si "Niloge".Nakuroga sasa hivi, angalia kiganja chako cha mkono wa kuume, umeona nini na unajisikoaje ?
 
Sawa Jurjani.
"Niroge"? Sahihi ni "niloge" au haya ni maneno mawili tofauti?
 
Back
Top Bottom