Njia gani nzuri kutoka Dar kwenda Mafia, Pwani?

jac salum

Senior Member
Mar 23, 2017
183
129
Habarini wana JF: Naitaji msada kufahamu njia nzuri kutoka DSM kwenda Mafia. Nimepata ajira Mafia na sina ufahamu na kisiwa cha Mafia. Pia naomba munijuze yafuatayo;-
  1. umbali kutoka DSM-MAFIA
  2. Gharama za usafiri kiasi gani?
 
Hongera kwa ajira Mwalimu wa masomo ya Sayansi.
Kuhusu usafiri sijui.
 
Kuna mabum ambayo yanachukua almost masaa manne kutoka nyamisati to mafia, nauli mpk mwaka 2013 ilikua around 13000. Anzia stendi ya mbagala ambapo kuna mabasi yaendayo nyamisati ila nauli sikumbuki sjui buku kama hivi. Mabum c hatari km onavoaminishwa, km umepata ajira ni heri ukakodi huko na sio kwenda na kurudi itakugharimu mno.
 
Ili upate uzoefu safari yako ya kwanza Nenda na boti....unachkua gari za mbagala to nyamisati,nyamisati pale rufiji unachkua boti kwenda mafia/kilindoni.....

Ova
 
Ndege au aende Nyamisati au aje kwetu Shungubweni avizie lift ya mashua za wavuvi, akifika baharini huko wanamuhamishia mashua za wavuvi wa Mafia, akikosa wanarudi haipiti siku tatu atafika tena bure.
Mkuu huo ushauri sio mzuri kama ni mara ya kwanza kusafiri na chombo baharini anaweza akadondokea baharini
 
Ndege au aende Nyamisati au aje kwetu Shungubweni avizie lift ya mashua za wavuvi, akifika baharini huko wanamuhamishia mashua za wavuvi wa Mafia, akikosa wanarudi haipiti siku tatu atafika tena bure.
Hivi kwanini kule hakuna boti za uhakika km azam....wasafiri ni wengi...
Nadhani wangeweka boti moja ya maana ndege zisingehusika sana..
Mafia ni sehemu maarufu sana...na watu wengi wanapangwa kazi kule
 
Back
Top Bottom