Njia gani ni sahihi za kuikomboa Simu iliyozama ghafla katika Choo cha Shimo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Inawezekana humu kukawa kuna Watu ambao hili limewakumba kama siyo kuwatokea hivyo si vibaya wakatupa uzoefu wao ili na sisi tuweze kufahamu kwa manufaa ya baadae.

Ikitokea tu ndiyo umetoka kununua Simu yako tena hizi za " kisasa " kabisa ambazo ni za gharama sana halafu ghafla ukashikwa na haja ambayo ikakufanya uwahi kwenda uani " chooni " na wakati huo huo ile Simu yako ulikuwa umeiweka mfukoni na ulipofika tu huko msalani wakati wa kujiandaa kuteremsha " makombora " yako ya " mwendokasi " bahati mbaya ile Simu uliyokuwa umeiweka mfukoni ikachoropoka na kutumbukia katika lile shimo la choo.

Katika mazingira kama haya utatumia mbinu gani kuikomboa hiyo Simu na pengine katika ile Simu kuna vitu vyako vingi sana muhimu na si ajabu labda muda mfupi tu ujao ulikuwa unangojea Simu ya " dili " au Demu ambaye umemtongoza kwa siku nyingi na amekulia vyako sana yupo njiani kuja kwako na ili afike inabidi kila mara afanye mazungumzo nawe ili uweze kumwelekeza.

Karibu tutoe uzoefu wetu tafadhali kwani yawezekana jambo hili likamtokea mwenzetu yoyote muda si mrefu.

Nawasilisha.
 
Dah... hiyo mbona bado itakuwa ndani ya kipindi waranti:) Wapigie wakupe nyingine:rolleyes:
 
Kama cm ni ya milioni 2 kwenda juu nabomoa Choo ila kama ni laki 8 kushuka chini naipotezea
 
1.cha kwanza simu ikiingia maji/chooni wahi kutoa betri , kama betri yake ni built-in fungua hiyo simu au peleka kwa fundi battery ichomolewe-- UKIFANYA IVO UNAZUIA MAJI KUSABABISHA SHOTI, UNAPUNGUZA RISK YA SIMu KUPATA SHOTI
2.Ifungue fungue simu yako tenganisha kila kitu alaf isafishe kwa mswaki na benzene/petrol ili kuhakikisha maji yote yanapotea
3.ianike juani ili ikauke kwa uhakika.
4.rudishia simu yako washa itakua haina shida

NB: simu itapona iwapo tu itakua haijapiga shoti, pia inategemea muda ambao simu yako imekaa ndan ya maji/mavi , pia inaweza ikapona ila ikapata matatizo kama mic,speaker ,touch au display kufa.
Wasalaam
 
Back
Top Bottom