Njia bora za kuchochea na kudumisha mahusiano katika ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia bora za kuchochea na kudumisha mahusiano katika ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mpilipili, Aug 7, 2012.

 1. M

  Mpilipili Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Wana JF naomba tuchangie mada hii. Nimeianzisha kwa makusudi kwani ndoa nyingi za siku hizi zinakosa vichocheo muhimu, wanandoa wanachokana mapema mno, imethibitika kuwa mahusiano ya wakati wa uchumba yapo juu zaidi kuliko mahusiano baada ya ndoa na yanaanza tu kuporomoka inapomalizika fungate.

  Nikianza kuchangia ukitaka kuimarisha mahusiano/mapenzi ndani ya ndoa fanya kati ya mambo haya:
  • Kila mmoja ampende na kumjali mwenzake
  • Kila mmoja awe mwaminifu kwa mwenzake
  • Jitahidini kuwa pamoja hasa baada ya kazi lakini sio full time, mkiwa full time mtachokana mapema, ruhusuni muda wa kutosha kila mmoja kum-miss mwenzake hii itachochea mapenzi zaidi, msipigianepigiane simu hiki kinaweza kuwa chanzo cha ugomvi hususani unaposhindwa kujibu a missed call ya mwenzako kwa wakati
  • Fanyeni mambo yenu kwa uwazi na ukweli, mfano katika shunguli za maendeleo kama ujenzi, biashara, nk
  • Badilisheni mazingira siku moja moja kama hamna watoto ikibidi hameni kitanda au tokeni nje-outing spend a night out with your wife/husband, hii itawaongezea feelings and emotions
  • Samehaneni mnapokoseana, mama jifunze kusema samahani mpenzi, baba jifunze kusema samahani dear haitawagharimu chochote zaidi ya kuimarisha uhusiano wenu
  • Msisikilize umbea wa ndugu au majirani, no comment about your affairs is acceptable
  • Kama mna matatizo katika uzazi waoneni wataalamu na mpate ushauri stahiki, msiwe na papara
  • Msimsahau Mungu, mkabidhini maisha yenu

  Haya wana jamvi tuchangie mada hasa tuliokwisha oa/olewa
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  nyimaneni dudu...i inaongeza mahaba.

  TRY IT AT HOME.
   
 3. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ishini kama marafiki siyo kama bos na mfagia ofis....lol
  kutaniana sometyms, (zingatia mood hapa), sio humo ndan muda wote mpo siriaz kama maafande
  peanen muda huru wa kila kuwa na friends wake na issue zake binafsi bila kuingiliana...
  mara moja moja fanyen baadh ya shughul za home pamoja, kama kupika...., (wow this is so romantic hak ya nan)
  kama kuna kitu kimekukera kuhusu mwenzio hakikisha kabla hamjalala mmefix au kabla hamjatoka asubuh kwenda kwenye mihangaiko muwe mmemaliza tofaut zenu
  asubuh mnapokwenda maoficn au popote kutafuta kilacho, muagane vizur, kakiss, maneno mazur ya kutakiana siku na kaz njema, na ndan ya hayo maneno mumuweke na Mungu kidogo...................
   
 4. C

  CAY JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa dudu ikikosekana bado ni ndoa tena?
   
 5. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hujui kiini cha ndoa za siku hizi (yebo yebo) kutokudumu, sababu kubwa hazidumu ni hii; watu wanaoana kwa kuangalia maslahi tu, na si vinginevyo. Zamani watu walikuwa wakioana kwa kupendana au kuchaguliwa na wazazi wao, ndiyo maana wanandoa wa zamani walikuwa wanatofauti kubwa kati yao ya kielimu/uchumi, mfano, mwalimu wa shule ya msingi aliweza kuolewa na mkuu wa mkoa, tajiri aliweza kuoa ktk familia maskini na maskini kuoa ktk familia tajiri. Hali hii ilisababisha watu kutoficha tabia zao halisi kabla ya ndoa. Siku hizi mtu akitaka kuoa/kuolewa anaficha tabia yake halisi na baada ya muda fulani ndani ya ndoa anaionyesha tabia yake halisi, hapo ndipo utamu wa ndoano unaponoga.
   
 6. m

  mgweno kasure Senior Member

  #6
  Dec 29, 2016
  Joined: Aug 20, 2016
  Messages: 144
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  ndoa zilikuwepo zamani siku hizi tunasogeza siku tu
   
 7. mwenye shamba

  mwenye shamba JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2016
  Joined: May 31, 2015
  Messages: 697
  Likes Received: 755
  Trophy Points: 180
  Siku moja mie nilikuwa nshavaa nguo zang za ofsin tayari kwa kuondoka na wife alikuwa asharud kulala baada ya kuniandalia maji.sasa nikamuaga then nkaondoka,kama dk mbili hv dudu likasimama ikabd nirud daah wife alifurahi sana aisee
   
Loading...