NgimbaErick
Member
- Mar 31, 2020
- 85
- 131
Inawezekana unatamani biashara au kampuni yako kuwa na website mtandaoni, lakini huna fedha za kutosha kulipia gharama za kutengeneza website. Hivyo basi kuna njia mbadala ambayo binafsi naiona ina uafadhali katika kutengeneza website Bure.
Maana, kuna njia nyingi lakini, katika hizo nyingi zao si nzuri na hazina manufaa kulingana na muda (mfano; wix, blogger, weebly, google sites). Pia kuna ambazo ni Nzuri lakini Ngumu kwa mtu wa kawaida kutumia (mfano; webflow).
Basi kwenye nakala hii, nitakuonesha njia ya BURE ambayo ni RAHISI, BORA, na ITAYOLETA MANUFAA. Nayo ni kwa kutumia 000Webhost (Free Hosting) pamoja na Wordpress.
MUHIMU: Njia hii (ya bure ya WordPress) ni nzuri, lakini usitegemee kupata matokeo sawa na website ambayo imetengenezwa kwa kutumia gharama za Hosting, Domain pamoja na Designer/Developer.
Moja kwa moja nitaenda kukuonesha hatua kwa hatua kuanzia usajili wa Hosting a Bure mpaka kuweka Website yako ya Wordpress Mtandaoni.
Yaliyomo:
- Kusajili Hosting ya Bure (000Webhost)
- Ku-install Wordpress
- Ku-install Plugins na Themes
- Ku-install Template
- Ku-upload taarifa zako
- Hitimisho
1. KUSAJILI HOSTING YA BURE
- Tembelea Website ya 000Webhost (www.000webhost.com), kisha bonyeza “GET STARTED”
- Ukifika hapa chagua sehemu iliyoandikwa “FREE SIGN UP”
- Hii ni sehemu ya kufanya usajili kama ilivyo kwa program zingine tumia Email yako kufanya usajili au tumia “GOOGLE” kujisajili fasta zaidi.
- Utakapokamilisha usajili utakutana na ukurasa kama huo, tafadhali bonyeza kwenye hayo maneno ya chini kabisa yanayofifia, ili kufanya hii kazi kuwa fupi zaidi, kwasababu kila kitu ntakuelekeza hapa, huna haja ya kufuata mwongozo wao.
- Utapoletwa hapa andika jina la Biashara au Kampuni, pamoja na Password, bonyeza “SUBMIT” .
2. KU-INSTALL WORDPRESS
- “SELECT” Install Wordpress.
- Jaza Admin Username na Password (Hakikisha umehifadhi taarifa hizi kwa kuwa zitatumika kuingilia kwenye WordPress), Kisha Bonyeza “INSTALL”.
- Itachukua takribani dk 3 kuinstall Wordpress, kisha utaletewa ukurasa wenye button iloandikwa “GO TO CONFIGURATION PAGE” Bonyeza hapo.
- Kwenye ukurasa huu utatumia zile taarifa za Admin Username na Password, kwa ajili ya kuingia kwenye Dashboard ya Wordpress.
MUHIMU
- Kufikia hapo umeshafanikiwa kupata Hosting ya Bure na WordPress bure. Kilichobaki ni kutengeneza Website yako kwa kutumia WordPress hii ni kazi rahisi na pia kuna watu wengi mno wenye ujuzi na wordpress hivyo ni rahisi kupata msaada mtandaoni.
- Lakini … Nimeandaa Mwongozo unaoendelea, utakaokupa Mwanga katika kutengeneza Website Nzuri kwa Kutumia Wordpress bila Kujua Coding na ndani ya Muda Mfupi tu, utakuwa umetengeneza Website yako.
KUTENGENEZA WEBSITE KWA WORDPRESS: KUTENGENEZA WEBSITE KWA WORDPRESS
Imeandaliwa na Erick Ngimba
Emali: hello@erickngimba.com
Website: www.erickngimba.com