Njia ambazo mtu anaweza kutengeneza pesa mtandaoni bila mtaji

nilichoelewa hapa yani mtoaji mada na wachangia hakuna mwenye uelewa mpana juu ya hizi mambo za mtandaoni
Wewe mwenye uelewa mpana ebu ngia tujifunze kwako maana mpaka umeona hakuna mweenye uelewa ujue unajua sana, ila kwa mm navyojua kweny digital hakuna anaejua zote kuna watu ni experts tu kwenye mambo ya SEO, wengne ni blog kama blogger, wengne ni youtubers, wengne ni affiliate marketing na zote hzo elimu yake ni ndefu sana na hazna mwisho kama mm tangu mwaka 2014 mpaka leo naifunza mambo mapya kwenye SEO na affiliate marketing.

ndio maana kuna forums kama hz ili kuongeza maarifa mtu akiejifunza SEO mwaka 2014 kurud nyuma ukimpa le website or blog aipandshe rank kwenye search engine tegemea kupgwa tu penalty kama huyo mtu hakuongeza maarifa coz daily search engne inazd kuwa smart.
 
Nimeweka nanga hapa....nina computer nzuri ina uwezo MKUBWA sana ila sijui namna ya kuingiza pesa
 
Kuna namna nyingi kutegemea na ujuzi ulionao mfano:

1. Kufanya freelancing ukatengeneza apps, website, graphics kwa watu/makampuni

2. Kufungua blog/youtube channel na kuweka maudhui yatakayokuletea hadhira kubwa na hivyo kupata fursa za matangazo.

3. Kufanya kazi mbali mbali zinazohitaji uwezo wa kibinadamu mfano kupangilia picha, kufanya utafsiri wa maneno mfano subtitles kwenye movie.

4. Kama una nyumba au chumba cha ziada unaweza kutangaza kupangisha kwa mitandao kama Air BnB.

5. Kuwa influencer kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na TikTok.

6. Kufanya biashara za forex au cryptocurrency (onyo sio kila mtu anaweza kutengeneza faida)
 
Inahitaji kuwa na camera??ila kila nikifikiria content nakosa idea kbs kwa mfano ww unapendekezaje?
Hapana hauhitaji kuwa na camera kama ni picha zipo mtandaoni na kama ni clip za video pia zipo tena za free ambazo yeyote anaeza kuzitumia bila kubughudhiwa.

Ukitaka kupata idea kirahisi basi angalia kile kitu ambacho unakipenda na ukigeuza kuwa contents, sababu kama kitu unakipenda basi huwa unakifuatilia na kama unakifuatilia basi utakuwa na material mengi kuhusu hicho kitu, hivyo basi hayo material ni rahisi kuyageuza kuwa contents.

Mm binfsi nafanya mambo yahusuyo filamu.
 
YouTube channel yako inaitwaje
 
Back
Top Bottom