Njia ambazo azijazibwa ili kuzuia wizi wa kula Tanzania na Africa

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Wanajamvi tangia nchi za bara la Afrika livae koti la siasa ya vyama vingi(pluralism politics) na kuandaa uchaguzi mara nyingi vyama mbadala au upinzani vimekua vikishindwa na mwisho kulalamika kua uchaguzi aukua wa haki au wa kidemokrasia. Tumeyashudia hapa Tanzania,Kenya,Uganda na Zimbabwe.

Vyama vya siasa au upinzani umekua ukisubiri mpaka siku ya kupiga kula na kuhesabu kula na kutangaza matokeo na kisha kulalamika. Hapa kuna mambo ambayo vyama vya siasa au upinzani inabidi kua makini kabisa na kutambua njia zinazo tumika ili kufanikisha wizi wa kula.Nitajaribu kuzitaja

1.Ugawaji au utengaji wa majimbo kwa upendeleo wa chama(garrymandering)

2.Upangaji wa vituo vya kupigia kula

3.Uandikishaji mfano watu ambao hawapo au si raia

4.Uchakachuaji wa daftari la wapiga kula maana serikali ndo inaliweka ilo daftari

5.Kutoa rushwa kwa wapiga kula au wagombea ili wajitoe au wasipige kampeini kwa uhakika

6.Kutumia dora yaani polisi na jeshi kwenye uchaguzi

7.Kutumia raslimali za serikali kwenye kampeini

8.Kutumia vyombo vya habari vya binafsi au serikali kupendelea upande mmoja

9.Kutoa vitisho kwa wapinzani mfano kuwafunga ,kuwapiga na kuzua kashfa dhidi yao

10. Kutotoa elimu kwa wapiga kula na taarifa muhim

11.Mwisho ni wakati wa kupiga ,kuhesabu na kutangaza.

UKAWA hizi njia zizibeni mapema maana tusije baki nakulalamika tu
 
Back
Top Bottom