Njia alizotumia Msukuma kuingia kwenye Siasa Za Fanana na Za Gwajima, Msukuma upambe kwa Lowasa mpaka unafiki Gwajima Kufufua Amina na Misikule!

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF

Ukimwona kwa macho ya kurukaruka unaweza ukadhani Msukuma na Gwajima ni ndugu lakini hawana ubini kabisa japokuwa wote ni kabila moja la kanda ya ziwa. Katika harakati za kutafuta pesa wamejituma haswa na baada ya kufanikiwa bila kujari viwango vyao vya elimu wakajongea kwenye siasa.

Ni dhahiri njia walizotumia zinafanana sana kwa kuwa wanaanza na upambe, uchawa wanamalizia na unafiki ndipo wanapofanikiwa kuwateka watu kisiasa.

Mwanzoni mwa mwaka 2014 Lowasa alivyokaza kabisa kuutaka Urais aliyekuwa wa kwanza kuibuka kumsaidia kufanya upambe na uchawa ni Msukuma, aliwahi kumkodia helicopter ya kufanyia mikutano. Watu walijiuliza msukuma ni nani? Kumbe ndio ilikuwa janja ya kujulikana. Baada ya Lowasa kukatwa na CCM yeye akajigeuza mnafiki na mitusi tele kwa rafiki yake Lowasa alivyoamua kuachana na CCM. Hapo alifanikiwa kutengeneza mazingira yake kupata ubunge kirahisi mno.


Safari ya Gwajima kupitia unafiki ilivyomwibua kutoka madhabahuni kwenda kwenye siasa, ilivyoanza. Hakuna asiyejua mapambano ya Mhasham Cardinali Pengo alivyotukanwa mitusi ya nguoni kwa kukataa kubariki walaka, nyakati hizo alikuwa mpambe wa Lowasa na Halima mndee, alifanyiwa figisu na chama mpaka akaondolewa tanganyika parkers. Akakumbana na lungu la makonda. Lakini huko nyuma kuibuka kwake alitumia uongo wa kufufua misikule na kutaka kumrejeshea Amina Chifupa uhahi. Hapo ndipo aliwakamata haswaa wanasiasa mpaka wakawa wanatumia kanisa lake kujinadi. Gwajima ndiye aliyekiwa mshenga mkuu wa lowasa na Chadema. Tusiende mbali unafiq mkubwa wa kujiingiza siasa alitumia njia ya covid kwamba haungani na chadema bali Magufuri kukataa watu kujifungia kuepuka maambukizi. Basi hakuishia hapo akaomba msamaha na makonda na pengo akarudi CCM na kuomba ubunge, kwenye kura za maoni alikatwa na wajumbe lakini Magufuri akamtaka Gwajima dili ikaishia kushinda ubunge.
 
Back
Top Bottom