Njia 3 'blogging' inanisaidia kupata kipato na jinsi inavyoweza kufanya hivyo kwako pia

amai_martha

Member
Jul 27, 2021
8
25
Ulimwengu umebadilika, hatuwezi kukataa kuwa teknolojia imebadilisha maisha yetu, kwa namna ambayo ni chanya na hasi pia. Siku hizi vitu ambavyo wazazi wetu hawakuwaza kama chanzo cha kipato imekuwa chanzo cha kipato kwetu, na kwa hali ilivyo ya ugumu wa ajira na wahitimu kuwa wengi tumejikuta kuwa imebidi tuje na njia nyingine za kibunifu za kujiajiri kwa hiyo kwa namna hiyo lazima tuipe sifa teknolojia kwa kuwa chanzo cha ajira na kipato kwa wengi wetu.

Kwa miaka mitatu sasa nimekuwa nafanya 'blogging' na 'vlogging', nina tovuti na pia ninaweka maudhui yangu YouTube, nilianza haya mambo nikiwa chuo, ambapo nakumbuka jumamosi moja nikiwa nimechoka sina cha kufanya nikaamua kuanzisha blogu na kuweka maudhui ya mambo ninayojifunza kwenye maisha ambayo naona yangekuwa na msaada kwa vijana wengine, na hapo ndipo safari yangu ya ilipoanzia. Na kwa YouTube huwa naweka maudhui yanayohusu maisha ya chuo ili kuwasaidia wanaoenda chuo au waliopo vyuoni kukabiliana na changamoto yoyote ile lakini pia huwa nawapa ushauri na dondoo zinazowarahisishia maisha ya chuoni.

Toka nianze 'blogging', nimepata faida nyingi sana, sio tu za kipesa ila pia za kimahusiano, nimeweza kupata marafiki wapya ndani na nje ya nchi, nimeweza kuongelea mada mbalimbali kwenye tovuti yangu ambazo siwezi kuongea na marafiki zangu na hivyo ikawa kama namna ya kupata uponyaji maana jambo likikaa sana moyoni nalo sio zuri, nimeweza kutia moyo watu, jambo ambalo hunifanya nijisikie vizuri moyoni, nijisikie kama nina msaada kweye maisha ya mtu mwingine, nimepata mpenzi kupitia blogu na la mwisho na la muhimu kwa makala hii ni nimepata pesa.

Hizi hapa ni njia tatu ambazo 'blogging' imenisaidia kupata pesa;

1- Nilitumia ujuzi wangu wa 'blogging' kuonyesha kuwa ninaweza uandishi, na hivyo nikapata kazi kwenye 'digital marketing agencies' kadhaa nchini. Niliajiriwa kwao kwenye kazi za uandishi na utengenezaji maudhui ya mtandao na ukweli ni kuwa walikuwa wakiangalia blogu yangu kama sehemu ya ujuzi wa hiyo kazi niliyokuwa nimeomba.

2- Nimeweza kupata kipato kwa kufanya 'freelance writing and editing' ndani na nje ya Tanzania. Nimekuwa 'editor' na 'writer' wa makala kwenye tovuti, ripoti, CV nk kwa watu binafsi na makampuni ambayo yalikuwa yanahitaji huduma hizo, hii yote ni kutokana na ujuzi wa uandishi niliogundua ninao kupitia 'blogging' ambayo naifanya.

3- Nimeweza kutengenezea watu matangazo na kadi kwa kutumia mtandao. Nakumbuka nilipokuwa chuo nilikuwa nawaandikia ujumbe wapenzi wa watu niliokuwa nakaa nao 'hostel' kwenye sikukuu ya wapendanao, hapo ndipo nilipojua nina kipaji cha uandishi ambao unaweza ukazidi tu blogging, kwahivyo huwa natengeneza kadi za sikukuu yoyote ambazo watu wangependa ziwe na maneno matamu kwa watu wanaowapelekea, lakini pia huwa natengeneza 'posters', 'business card' nk.

Najua kuwa mambo mengine ambayo nimeyasema nayafanya kupitia blogging ni mambo ambayo yanachukua muda, ila kwenye maisha huwa siamini kwenye kuchelewa, huwa naamini mtu akiamua kuanza leo pia anaweza kupata mafanikio yake kupitia 'blogging' na 'vlogging' kama lilivyo fungu lake kwenye maisha. Muda huu ambao vitu vingi vinaenda kidijitali zaidi naona fursa nyingi zipo viganjani mwetu lakini pia tunaweza kuzitengeneza kwa kudandia hili treni la teknolojia.

Najua kuna changamoto nyingi ambazo mtu unaweza kutana nazo likija kwenye swala la 'blogging' na 'vlogging' mfano vifaa hasa wakati wa kuanza, najua unaweza taka mpaka ununue camera nzuri, labda laptop nk. Na mara nyingi unajikuta hili ndio linakufanya usianze, mimi huwa nashauri watu waanze na vile walivyonavyo. Kutengeneza maudhui na kujiweka mbele ya watu ni jambo linaloogopesha sana, cha msingi ni kuanza pale unapopata wazo badala ya kusubiri, mara nyingi ukisema usubiri muda mrefu utajikuta hauanzi kitu. Tumia simu janja yako na fungua blogu uanze kuweka maudhui ya mambo unayoyapenda na uone hiyo safari unayoianzisha inaweza kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.

Je nimekushawishi kufanya blogging? Kama umeshashawishika, umepanga kuanza lini?

~ M
 
mkuu nisaidie blog template nzuri kama inawezekana mm ni blogger mwenzio niliyepata mzuka mkubwa wa kuanzisha blog maana nina material mengi adimu,najiona mbali sana
 
Haya mambo ni mazuri ila yanahitaji commitment
 
Boss nataka Blog ya elimu inagharmu Tsh ngap??
0763208101
 
Kwa Bloggers na Vloggers karibuni sana kwenye group letu la Telegram. Huko utaweza kujifunza vitu tofauti tofauti kuhusiana na blogging na vlogging, kuuliza maswali kama unatatizo lolote na mengineyo mengi, Karibuni sana.

Blog ni sehemu nzuri sana ya kutengeneza pesa mtandaoni.
Blog nyingi nimeona zinafeli sana mwasababu huchanganya NICHE.
Utakuta humo humo kazungumzia Tech, habari, muziki, n.k kiufupi blog haieleweki maudhui.
Chagua NICHE moja tu. Kama ni tech, muziki au habari.
Itasaidia kuwa post nyingi na zilizoshiba kimaudhui
kwa mwenye blog anahitaji mwandishi kwa blog yake anicheki
 
Hiyo blog siyo yangu. Mwenyewe nimequote tu. Baada ya kuperuzi huko mtandaoni.
bro hii iko na password mpaka nilipie hela ndio nipate.kwa mm niliyeanzisha blog kutokana na bandiko lako kunipa mzuka ingawa nina vitu adimu vitakavonifkisha mbali ndan ya muda mchache tu unanisaidiaje? tukiacha kwanza mambo ya kulipia maana sina kitu nina pc tu hapa.
 
Tozo mpya za Miamala zitumike kutengeneza Walipa Kodi kwa hiari na fursa za kifedha mtandaoni.
 
Back
Top Bottom