Njemba ajisalimisha polisi akiwa uchi kwa kumuogopa mjeshi baada ya kumfumania na mkewe

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
762
772
Mwanaume mmoja nchini Kenya amejisalimisha kituo cha polisi cha Embakasi Jijini Nairobi akiwa hana nguo baada ya kukimbia kutoka kwenye fumanizi nyumbani kwa mke wa Mwanajeshi.

Imeelezwa kuwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni Mwanajeshi alirudi ghafla nyumbani bila taarifa na kumkuta mkewe na mwanaume huyo wakiwa ndani, ndipo alipofanikiwa kukimbia.

Alifika kituoni akiwa mwenye wasiwasi mkubwa huku akiomba msaada wa kuokolewa dhidi ya mume wa mwanamke aliyekutwa naye, ambaye alikuwa anamtafuta kila mahali.

Akiandikisha taarifa katika kituo cha polisi, mwanaume huyo aliyefumaniwa amesema kuwa mwanamke alimuambia kuwa ni mjane, baada ya mumewe kufariki katika shambulio la Dusit d2 mwaka uliopita
EDEB47DD-9483-4AD3-A2D3-0F039983708E.jpeg
 
Shambulio la Dusit, Sijui ndio nini Hahaaa
Ulitakiwa kuuliza Dusit ni nini ila usingeongezea kejeli..hapo mwisho...
Inamaana Shambulio la magaidi Alshabab kwenye hiyo Hotel ya Dusit mlikuwa wadogo sana..mbona limetokea mwaka juzi tuu.nisamehe kwa lugha niliyotumia..
Nilitaka kumtetea mleta mada hajakosea chochote.
 
Mie hoi huku
Hata wewe hukumbukia Shambulio la magaidi wa Alshabab kwenye Hotel ya Dusit mbona halina muda mrefu??
Je la miaka mingi kidogo Westgate utalikumbuka kweli...ingia kwenye google au youtube uone picha na video za shambulio la Dusit hotel utaona mauaji hayo.
 
Ahahahaha.
Jamaa akikaa selo na mjeshi afanye kasoo kidogo naye akakae naye selo moja.
Nimewaza hivyo hivyo. Yaani hapo na mjeda nae afanye tukio maeneo ya jirani na hicho kituo awekwe ndani akapambane na mgoni wake. Jamaa hapo marinda yake yako hatarini sana
 
Ulitakiwa kuuliza Dusit ni nini ila usingeongezea kejeli..hapo mwisho...
Inamaana Shambulio la magaidi Alshabab kwenye hiyo Hotel ya Dusit mlikuwa wadogo sana..mbona limetokea mwaka juzi tuu.nisamehe kwa lugha niliyotumia..
Nilitaka kumtetea mleta mada hajakosea chochote.
Vizuri sana mkuu kwa ufafanuzi wa kina wengine walikuwa bado wanakojoa kitandani
 
Back
Top Bottom