Nje ya ukatibu wenezi wa ccm taifa, nape ni nani pia katika ccm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nje ya ukatibu wenezi wa ccm taifa, nape ni nani pia katika ccm?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Manywele., May 27, 2012.

 1. Manywele.

  Manywele. Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana jioni katika taarifa ya habari ITV nilimsikia Nape akisema "hata akibaki peke yake CCM haitakufa" nika baki na maswali kichwani je, yeye ni miongoni mwa waasisi wa chama, au kashaona kuwa viongozi wote na wana CCM Wote wako mguu nje mguu ndan ktk chama hicho kuwa mda wowote wanaweza kukihama chama hicho? Naombeni msaada wenu wana JF.
   
 2. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kula maharage panya wote hao?by Nnauye Jr.
   
 3. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135


  ..ni mwana-ccm.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Mkuu Manywele, kijana alizaliwa CCM, akakulia CCM, na atafia CCM, iwe ni CCM itamfia au yeye ataifia ila ni CCM damu, hata ukimchanja na kiwembe, damu itakayotoka siyo ya rangi nyekundu, bali ni ya rangi ya Kijani na Manjano!.

  Kijana alikuwa Chipukizi tangu akiwa miaka 4, baadae akajiunga UV-CCM, akawa kiongozi na mjumbe wa baraza kuu la UV- CCM na mjumbe wa NEC na sasa ni mjumbe wa CC, Mjumbe wa NEC na Katibu Mwenezi wa CCM. Japo kichama M/Kiti ndio most powerful akifuatiwa na makamo na KM, then CC na NEC, kiukweli the real powers within CC lies with JK then huyu kijana!. Wengi kule ni spent force wameisha jichokea wanasubiri tuu kuzama na dubwana lao!.

  Enzi zake za UV-CCM, wakati EL akiwa ni Mlezi wa UV-CCM. EL akampatia lile jengo la UV-CCM pale mjini, rafiki yake yule mdosi kwa bure, kijana akastukia dili akapinga na kuita huo ni ufisadi, UV- CCM wakamshukia na kumfukuza, na kuitaka NEC kumvua uanachama, JK akamnusuru!. Yeye na EL wakawa paka na panya!.

  Hatimaye baadae sio tena akafukuzwa CCM bali akaingizwa rasmi CC na EL ndio akatimuliwa CC!. Ndani ya CC akaamua ili kummaliza EL, akabuni mkakati wa kujivua gamba ili EL, RA na Mzee wa Vijisenti wajing'atue wenyewe ndani ya siku 90 vinginevyo, watang'atuliwa!.

  Akazunguka nchi nzima akitangaza hiyo kujivua gamba bila kujua kumbe alikuwa akipiga vuvuzela tuu!.

  EL alitoa msimamo kuwa yeye na JK hawakukutana barabarani!. Siku 90 zilipita bila bila japo RA alijivua gamba kwa hasira.

  Story za vua gamba zilianza kubadilika hatimaye sasa imebaki ni hadithi tuu ya Sungura na fisi!.

  Huu ni mwaka wa uchaguzi wa CCM. The most powerful man wa CCM ni RA ambaye sasa amejeruhiwa na yuko nje ya ulingo!. Ukimjua adui yako na kumuona, unaweza kupambana nae na kujua jinsi ya kujihami!.

  Simba aliyejeruhiwa ni hatari zaidi kuliko simba mzima!. Na huko msituni kwa vile hujui ata strike kutokea upande gani, hivyo huwezi kujua ujihami vipi, salama yako ni kuzungusha zungusha kichwa ili kujaribu kumuwahi toka kwa mbali!, hivyo sasa ndio maisha ya huyu kijana wetu ndani ya CCM na fainali ni mwaka huu!.

  Kufuatia nguvu za maadui zake, kijana mwisho wake ni either kupigwa chini jumla kwenye uchaguzi huu na kubakia ni mwanachama wa kawaida kusubiria kumvaa JJ. Mnyika jimbo la Ubungo 2015 ambapo atapata kipigo cha mbwa mwizi na kuangukia pua, hivyo kusubiria kufia tuu CCM kama wenzake wengi wanaosubiria!.

  Ila akisurvive uchaguzi wa ndani wa CCM, atakuwa ameprove kuwa yeye ni mwamba, na juu ya mwamba huo, CCM itajenga ngome yake!.

  Baada ya uchaguzi wa CCM, kijana akisurvive, tafadhalini sana, huyu atakuwa sio mtu wa kubezwa tena kwa sababu 2015 ataingia bungeni japo CCM inauwezekano mkubwa wa kupigwa chini na 2025 ataibuka kinara wa CCM mpya iliyotoka likizo ya miaka 10 kuupisha upinzani!. Huyu jamaa itakuwa ni habari nyingine!.

  Ile dhana ya " Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni", inaweza ku apply kwa kijana huyu!.
   
 5. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Nepi ni MBWA, mwenye MBWA yupo,,,
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mropokaji
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Anaongea saizi baada ya Tendwa kuinyima CCJ usajili wa kudumu na kukataliwa kujiunga na CDM. Mtu mnafiki mara nyingi hujifanya ana uchungu sana na kitu. Hata wake za watu wanaoliwa sana nje akimpigia simu mumewe utasikia baby, sweet, honey, malavidavi... Huku pembeni kuna jamaa linampumulia taratiiibu. Kama ana uchungu na chama aje huku SITE kwa wanachama waliokata tamaa na sasa wameamua kuvaa Magwanda, sio kuongelea runingani au redioni. Unafikiri CDM wangefanyia M4C redioni na runingani ingefana? Ni kwa sababu wanakuja kwa wananchi, tunaongea nao na kuwasikiliza live bila chenga. Nape aanze kuitisha mikutano ya uhamasishaji asilete porojo
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Nje ya uenezi, Nape ana cheo cha uenyekiti wa wapaka poda Tanzania.
   
 9. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hivi kunaweza kuwa na chama chenye mwanachama mmoja? Maana ya chama ni nini? Nafikiri Nape kwanza afafanue maana ya chama kabla hajaeleza ccm itapona vipi akiwa amebaki peke yake. Wanahaha!
   
 10. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama huwezi siasa au huna mchango kaa kimya....huwezi kumuita mwanadamu MBWA haijalishi mmetofautiana kiasa gani....aliyeemuumba alimuumba akiwa mtu, tena kwa mfano wake.....wewe ni nani hata umwite mwanadamu mbwa???????!!! tumia vizuri keybodi yako acha ufedhuli

  mix with yours
   
 11. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usiumize kichwa jamaa kalewa madaraka madogo ya chama, huoni anajiita mheshimiwa ukichanganya na mtumbo ule anajiona ndo muasisi wa chama. Jamaa mroho wa madaraka sana ndo maana aliponyimwa akaanzisha CCJ
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio maana katika NEC iliyopita Mzee Yusup Makamba alimchana live Nnauye Jr kwamba anaendesha chama kama mali yake binafsi.

  TUMBIRI,

  tumbiri@jamiiforums.com
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Nje ya ukatibu mwenezi wa ccm Nape ni mwanachama wa ccm.
   
 14. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  Mimi huwa nahisi nape ni mamluki wa CHADEMA ndani yaCCM...huwa simuelewi elewi
   
 15. J

  Jimy P Senior Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama Imara , wakati tunapata uhuru tulikuwa na barabara ya lami moja, sasa kila mkoa unaunganishwa na lami, hata Chadema wakipata nchi hawatawapatia pesa mfukoni zaidi wataiba tu kama ambavyo Slaa kaanza kuchukua kwenye chama bila idhini na kujenga nyumba.. Je akikabithiwa nchi atabeba kila kitu.
  Cha Msingi kupata viongozi wazalendo
   
 16. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 663
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 180
  muacheni aseme asiposema anaweza akateuliwa mwingine nafasi yake!!
   
 17. a

  anophelesi JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 612
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  wakuu nadhani mheshimiwa katibu wa uenezi ccm ndg nape hamjamuelewa. alichosema ni kua hata akibaki mwenyewe ccm haiwezi kufa, point yake hapa ni ccm kutokufa na sio ccm kubaki madarakani au kuendelea kutawala kama by implication mawazo ya wengi yanavoonesha. in fact nape is saying what he means and means what he's saying! asalam aleikum.
   
 18. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asigwa,
  Nnauye Jr ni mamluki wa CCK ndani ya CCM. Chadema hatuna haja kupandikiza watu ndani ya CCM wakati wao wenyewe wakitoka kwenye vikao wanaleta minutes za vikao vyao hapa Ufipani Kinondoni.

  TUMBIRI,

  tumbiri@jamiiforums.com
   
 19. U

  UNO Senior Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio ukweli
   
 20. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kibwabwaja.
   
Loading...