Nje ndani za Chuo Kikuu cha Dodoma

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wanaJF. Naoma nielezee histori fupi ya hiki chuo. Baada ya kuona kuna chuo kikuu kimoja tu,Mwalimu alitoa wazo la kujengwa kingine. Wapambe wakaanza kumshauri Mwalimu mkoa ambapo chuo icho kijengwe.

Wengine KLM, oh Arusha, sijui Mbeya n.k. Kama kawaida ya Mwalimu akaja na maamuzi ya kipekee kabisa,akasema anataka kijengwe Dodoma. Ivyo akawaagiza CDA watenge eneo kwajili ya chuo icho. Wakati wa Mwinyi,mpango huo wala haukufanyiwa kazi.

Alipokuja BWM,ndio akaanza mikakati ya utekelezaji wa mpango huo (initial preparations). Mkwere alichokifanya na kutake over alipoishia BWM. Ivyo basi UDOM ni mpango mrefu wa serikali,na si wazo la Mkwere kama ambavyo anataka kupotosha historia (ni aibu hata kina Kikula nao wameingizwa kwenye mkenge kwa kuandika historia ya uongo).

Hali ya sasa ya chuo: ujenzi unaendelea wa college mbalimbali. Ingawa kihalisia ujenzi ni wa kiwango cha chini sana,kwani kuna majengo ambayo yameanza kukarabatiwa kutokana na kua na nyafu na mengine plaster kubanduka! Pia kwa kupakwa rangi nyeupe,majengo yamefubaa kwa vumbi ivyo kuwa na gharama za ku repaint mara kwa mara(mafundi walipendekeza chuo kijengwe kwa matofali ya kuchoma,Mlacha na wenzake wakakataa. Mafundi wakasema basi hisipakwe rangi nyeupe,Mlacha pia akasema NO!).

Mlacha na wenzake waliona kwa matofali ya kuchoma ujenzi utachukua mda mrefu wakati wenyewe wanataka kudahili wanafunzi 40 elfu by 2012! (sasa wapo 20k+).

Hali kwa upande wa wakufunzi ni mbaya,kwani wana ofisi zisikuwa na viti wala meza,hakuna internet,madarasani hakuna meza pia, chuo kizima kina projectors zisizozidi 10! Chuo kinadahili unqualified students,ivyo kuwapa shida wakufunzi katika lecturing!

Masilahi ya wakufunzi hayapewi kipaumbele. Pesa za kujikimu kwa wakufunzi wapya hakuna,mishahara mipya hakuna mpaka sasa. Kuna tofauti ya mishahara na vyuo vikuu vingine vya umma! Wakufunzi wakidai haki zao,wanatishiwa kufukuzwa! Hali izo,zimesababisha wakufunzi wengi kuondoka.

Itaendelea..............
 
Nasikia Mwigulu akisema anamshukuru Kikwete kwa uamuzi aliochukua kuhusu UDOM. Mimi nalidhani UDOM ilianza enzi za Mkapa na sio Kikwete. They are trying to justify 'Deni la taifa'. I think CCM is a living hell.
 
Deni la taifa halina uhusiano na UDOM. Hela nyingi tena na ufisadi ndani kama kawaida zimetoka kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Wameifilisi mifuko hiyo kwa uchotaji usio na mpango. Sidhani kama watu wa PPRA walihusika hapo.
 
Tatizo linalotuumiza kwa kuwa na kiongozi kama huyu wa sasa ni kwamba hata kwenye chama chake haijulikani kama alipita kihalali au nguvu ya pesa ya wapambe
 
Nasikia Mwigulu akisema anamshukuru Kikwete kwa uamuzi aliochukua kuhusu UDOM. Mimi nalidhani UDOM ilianza enzi za Mkapa na sio Kikwete. They are trying to justify 'Deni la taifa'. I think CCM is a living hell.

Hapana haikuanza enzi za Mkapa, Hicho ni chuo Kikuu kilichoweka rekodi ya dunia toka kilipotangazwa nia ya kujengwa mpaka kilipojengwa na kuchukuwa intake ya kwanza ya wanafunzi, ni juhudi za Kikwete pekee.
 
Mbona madeni matupu, mashirika ya hifadhi ya jamii ndiyo yamejenga kile chuo na wanadai pesa zao kwa riba. udom wamejenga kwa pesa za mkopo, tunadaiwa na mashirika ya hifadhi almanusura yafilisike kwa kujenga kile chuo.na deni lile ktk bajeti ya mwaka huu wwameweka bajeti tutaanza kulilipa kwa kodi zetu.
 
Tuwe wakweli, Wazo la kuanzisha Chuo lilianza wakati wa Jakaya ya Edward Lowassa, likakamilishwa wakati wa Jakaya ya Pinda. National Stadium ndo ilianzishwa na Mkapa akamalizia Jakaya. Kwenye la Chuo cha Dodoma nampa A Jakaya, Mengine namtoa kwenye chumba cha mtihani hana hata vigezo vya ku attempt mtihani wa Urais
 
Hapana haikuanza enzi za Mkapa, Hicho ni chuo Kikuu kilichoweka rekodi ya dunia toka kilipotangazwa nia ya kujengwa mpaka kilipojengwa na kuchukuwa intake ya kwanza ya wanafunzi, ni juhudi za Kikwete pekee.
Cool, Kikwete deserves credit on this. Big one. :poa Lakini ndio deni la Taifa limefikia hapa, maana naona Mwigulu anakazia UDOM kama ndo chanzo kikuu cha Deni la Taifa.
 
Chuo kilianza kujengwa kwenye awamu ya JK. Lakini ni mpango ambao ameukuta kutoka kwa mzee Mkapa. Hii ni kutokana na uanzishwaji wa MMEM kwa Shule za Msingi na MMES kwa Shule za Sekondari. Hivyo lengo la kuanzishwa kwa UDOM Muasisi wake ni Mzee Mkapa ili ni ku accommodate zao na mipango hiyo ya MMEM na MMES.
 
Naunga mkono hoja. Hata Jk mwenyewe alipokuwa anatangaza azma ya ujenzi huo alisema ni muendelezo wa kupanua wigo wa wasomi ulionzia MMEM and MMES. Kimsingi serikal ina mipango ya muda mfupi na mrefu.
 
Nasikia Mwigulu akisema anamshukuru Kikwete kwa uamuzi aliochukua kuhusu UDOM. Mimi nalidhani UDOM ilianza enzi za Mkapa na sio Kikwete. They are trying to justify 'Deni la taifa'. I think CCM is a living hell.
My friend UDOM iliasisiwa na jk na lowasa.lowasa ndye alowaita wakuu wa mifuko ya jamii na kutoa maelekezo.hutaki unaumwa degedege
 
My friend UDOM iliasisiwa na jk na lowasa.lowasa ndye alowaita wakuu wa mifuko ya jamii na kutoa maelekezo.hutaki unaumwa degedege

Kumbe ni mpango wa Prof. wa Kichina ndo maana kipo chini ya kiwango...??
Yaani yule jamaa boya sana.... Sijuhi kipi alianzisha na kikamilika bila dosari...
 
My friend UDOM iliasisiwa na jk na lowasa.lowasa ndye alowaita wakuu wa mifuko ya jamii na kutoa maelekezo.hutaki unaumwa degedege
Mi nimesema nadhani, sasa mambo ya degedege yanatoka wapi. Kwani huwezi kuelekeza. Na kwa Taarifa ni kwamba Kikwete amejenga tu, mpango uliasisiwa na BWM.
 
Cool, Kikwete deserves credit on this. Big one. :poa Lakini ndio deni la Taifa limefikia hapa, maana naona Mwigulu anakazia UDOM kama ndo chanzo kikuu cha Deni la Taifa.

Deni la Taifa lisikutie wasiwasi, utajiri tulio nao sasa na anaotuwachia Kikwete tunaweza tukakopa hata mara 1,000 ya deni tulilonalo sasa hivi na tusitetereke, mpaka sasa tuna cubic feet trillion 55 zilizovumbuliwa za Gas na utafiti unaendelea - Kumbuka hilo.
 
Kwa Viongozi wa aina ya Kina Ngeleja, sidhani kama tutakombolewa. Nchi zenye utajiri wa mafuta na gesi zimeishia kupigana vita. Mimi sina imani kabisa na hiyo gesi. Kama hatutapata kiongozi mzuri, ndo basi tena.
 
Back
Top Bottom