NJAMA za Serikali, CCM & CUF, mikononi mwa Habari Leo, soma; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NJAMA za Serikali, CCM & CUF, mikononi mwa Habari Leo, soma;

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Isike, Sep 30, 2012.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [FONT=&amp]Wakuu
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Kile kinachoonekana kuwa ni mkakati maalum uliopangwa kati ya CCM, CUF na baadhi ya viongozi wa serikali katika baadhi ya mamlaka/ vyombo vya serikali dhidi ya CHADEMA, unaweza kukiona kwa uzuri kwenye para kadhaa 1-5, kisha 14-mwisho, za stori ya Habari Leo, iliyoandikwa Septemba 28, 2012, kama unavyoweza kuisoma hapa chini.[/FONT]

  [FONT=&amp]CUF yaitisha Chadema[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika uandishi wa habari, hasa katika kufanya kinachoitwa analytical reporting, mwandishi au mhariri asipokuwa makini au kama hawezi kufanya aina hiyo ya uandishi kwa uzembe au kwa kuzoea merely reporting (so and so said so, conveyer belt), ataishia kuweka maoni yake au kuandika kile anachokitaka yeye. Hapa inakuwa ni uhandisi wa habari, si uandishi wa habari tena.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ukiisoma hiyo habari kwa umakini. Katikati ya maneno. Ukafanya mahesabu ya kifikra, hasa katika kutafuta mantiki za hoja na hatimaye kufikia hitimisho lililo sahihi na linaloaminika, utaona wazi mchezo ambao baadhi yetu hapa mlishaanza kuuzungumza tangu jana.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kwa uhakika mpaka leo asubuhi, vyanzo vya kuaminika vilikuwa vimeshatoa mrejesho ulio kamili juu ya dokezo/angalizo la awali kabla hata ya mkutano wa Jangwani ambapo ‘jamaa' walifanya mkutano wa hadhara, kisha wakatangaza ‘copy and paste' ya kile ambacho CHADEMA walikuwa wanafanya. Haikuwa dhambi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Behind [/FONT]

  [FONT=&amp]
  Mapema sana, vyanzo vikaanza kutoa viashiria vya kuwepo kwa kitu kikubwa zaidi nyuma ya V4C kilichokuwa nyuma ya pazia. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Inajulikana wazi kuwa CCM na serikali sasa hawawezi kufanya siasa tena. Si bungeni, wala nje ya bunge. Kote huko wamechuja na hawawezi kujibu hoja za CHADEMA tena. Kwa hiyo ilikuwa lazima itafutwe mbinu ya kudhibiti watoa hoja. Kudhibiti wakosoaji. Kudhibiti upinzani usifanye kazi yake ya kikatiba. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Njia nzingine haramu za kuwinda na kutaka kuua viongozi wa mabadiliko, ikiwemo kumteka na kumtesa kutaka kumuua Ulimboka, kufungia Mwanahalisi na kutaka kuwaua baadhi ya viongozi wa CHADEMA, hatutazijadili hapa kwa sasa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Njia ya kutumia vitisho, kwa kuua watu ili kuendeleza propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha vurugu na shughuli zake zinaendana na vifo vya watu, ilikuwa futile. Hasa katika matukio mawili ya hivi karibuni. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Pamoja na polisi kumuua kwa makusudi kijana Ally Zona pale Morogoro, bado wakazi wa mji ule walikusanyika kwa wingi mno katika moja ya mikutano mikubwa ya kihistoria ya CHADEMA, achilia kwa mkoa huo wenyewe. Tukio la Polisi kumuua kwa makusudi Daudi Mwangosi likazamisha kabisa mipango yao hiyo ya kutumia vyombo vya dola.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Sasa ilikuwa lazima mkakati mwingine ubuniwe na uanze kufanya kazi. V4C ikawa moja ya fursa sahihi ambayo watu wengi wanaweza wasiione kwa haraka na kwa uwazi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kwanza; kutaka kuonesha kuwa CHADEMA na CUF wako kwenye league moja. Yaani vyama hivi vianze kujibishana. Automatically hapa focus ya kuendelea kuipiga CCM na serikali yake inakuwa imepotezwa, hivyo wakati vyama vya upinzani hivyo viwili vinajibishana, jamaa wanakatiza katikati. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Lakini pia mkakati huu ulidhaniwa kuwa ni njia nzuri ya kuirudisha CUF kwenye forum ya walau kuanza kujadiliwa kila siku. Maana kujibishana na CHADEMA kungewapatia jukwaa la bure. Ndiyo maana tangu siku ya kwanza, neon CHADEMA lilikuwa ndiyo kibwagizo kwa hoja za wazungumzaji wengi pale Jangwani. Huo mkakati ulishaonekana mapema. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Pili; ndiyo hiyo unayoiona kwenye Habari Leo. Kwamba zianzishwe vurugu kwenye mikutano au mikusanyiko inayoihusu CUF kisha lawama zielekezwe kwa CHADEMA. Kwa nguvu zote. Kwa kutumia kila njia inayowezekana. Si ajabu gazti hilo lilianza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi. Soma vizuri kuanzia para ya kwanza ya stori hiyo mpaka ya tano. Ukishasoma uzushi wa Kambaya, soma tena kwa makini para ya 14 mpaka mwisho. Katika para hizo unaona vyema kisichoonekana kwa akili ya kawaida hivi![/FONT]
  [FONT=&amp]
  Sasa kwa nini hii namba mbili; simple. Inatafutwa hila ya kuzuia kazi za kisiasa zinazofanywa na CHADEMA. Kama ilivyoandikwa hapo juu, zitaanzishwa vurugu makusudi, watu wanaweza kupigwa/kupigana kwa makusudi. Watu wataumia. Kutakuwa na tension ya kutengenezwa. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  CUF watatoka na kudai waliofanya hivyo ni CHADEMA. Hivyo nao wanajipanga kulipiza kisasi katika maeneo mengine kwa kisingizio eti wamefanyiwa fujo na CHADEMA blah blah blah! Hili tayari limefanyika hivi majuzi, ambapo CUF wamepita sokoni, wamefanyiwa fujo na watu wachache wasiojulikana, mbele ya Askari Polisi, muda mfupi kiongozi wa chama hicho anakurupuka kuhitimisha waliofanya hivyo ni CHADEMA.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Julius Mtatiro na Abdul Kambaya walipataje ujasiri wa kukimbilia kusema uongo kiasi hicho? Je wanakiri kuwa Arusha nzima ni miliki ya CHADEMA, je wanakiri kuwa soko lile ni miliki ya CHADEMA?, Je wanakiri kuwa wakazi wote wa Arusha popote walipo ni wafuasi na wanachama wa CHADEMA? Je waliofanya fujo wamo kwenye orodha ya wanachama wa CHADEMA, je wanachama wa CHADEMA wana alama kwenye mapaji ya uso, kiasi kwamba tu Mtatiro na Kambaya wakimwona mmoja wao wanajua kuwa ndiyo hawa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Je katika mkakati wao huo kwa nini tukio la majuzi Arusha lisiwe limefanywa na watu wa CCM au vyombo vya dola ili sasa kuanza kutimiza ,malengo mahsusi yanayokilenga CHADEMA kwa sababu CCM na serikali yake hawawezi tena kukikabili chama hicho kwa hoja?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Tunajua kuwa baada ya kilichotokea Arusha kweli wataachiwa kwa muda, ili kuendelea kutengeneza tension inayotafutwa iwepo. Lakini hapa watakaoanza kufanya fujo kwenye mikutano ya hadhara hasa ile inayoihusu CHADEMA, wakipiga na kuumiza watu vibaya, si lazima wawe Blue Guards wa CUF pekee. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Katika hatua hii wataingizwa vijana wa Green Guard. Wale vijana wa CCM ambao mtakumbuka ambavyo wamekuwa wakiwekwa makambini, wakipewa mafunzo ya ya kupiga, kutesa, kuteka na kuua. Hapa watapewa hiyo kazi ya kuanza kufanya fujo kwenye mikutano ya hadhara ya. Hivyo itakuwa imetengezwa tension kubwa, ambayo eti itakuwa imetokana na shughuli zinazofanywa na CHADEMA na CUF.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Zitaanza kauli za kulaani. Serikali itaingilia kati kwa kusema sasa inafikiria/inazuia operesheni hizo za vyama vyote viwili, kwa sababu zinahatarisha usalama wa Watanzania (kama walivyoandika Habari Leo na kama alivyowahi kusema Jaji Werema). Lengo litakuwa limetimia. CUF watajitokeza hadharani , tena kiongozi mkubwa kabisa (let's say Maalim au Lipumba hivi mfano).[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Atasema, eeh kweli bwana tunaona kuna matatizo, watu wanaumia, watu wanapoteza maisha kutokana na shughuli hizi za vyama vya siasa, hizi operesheni hizi…sisi tunakubaliana na agizo la serikali la kusitisha shughuli zetu hizi mara moja, sisi kuanzia sasa hivi tunasimamisha hii V4C yetu mpaka hapo baadae. Tunataka wanachama wetu wakubali suala hili, kwa ajili ya amani ya nchi unajua nchi yetu ya amani sana, blah blah blah. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Wakati huo kumbuka kuna kauli za kulaani zimetengenezwa kila mahali. Zote mlengwa akiwa mmoja, maana watakuwa wameshatengeneza mazingira ya kipropaganda kuwa watu wanakufa kwa sababu ya shughuli za kisiasa. Eti mikutano na maandamano ndiyo inaua watu, sio risasi, bunduki na mabomu ya polisi na vijana wa CCM. Serikali ya CCM itahukumu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Wasichojua CUF(/)[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Wanachezeshwa ngoma, kwa kujua au kutokujua. Lakini wanachoisaidia Serikali ya CCM na CCM yenyewe sasa hivi dhidi ya CHADEMA, ndiyo hicho hicho ambacho chama tawala na serikali yake vilifanya dhidi ya CUF. Wakati ule wakiambiwa ni chama cha kiislamu, chama cha kigaidi, kimeingiza silaha kutoka nje ya nchi. Chama kilichokuwa kikipiga hata waandishi wa habari. Tena mara mbili makao makuu ya chama hicho. Hawakuwahi kusikia CHADEMA ikiungana na watawala dhidi yao.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Wajue kitu kimoja muhimu kuwa, umaarufu wa CHADEMA haujapatikana kwa kuungana na watawala dhidi ya wapinzani wenzao. Umaarufu wa chama hiki makini cha upinzani, kinachobeba matumaini ya mabadiliko ya Watanzani wengi haukupatikana kwa kushikamana na watawala, umepatikana kwa kupambana na watawala, kutetea haki na uwajibikaji, kupinga vita ufisadi na ubadhirifu kwa wazi kabisa. Kuonesha sera na mikakati imara mbadala ya utumishi kwa umma.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  CUF hawawezi kuungana na watawala dhidi ya CHADEMA ili eti kutafuta namna ya kurudi kwenye chati. Ni muhimu wakajua hawawezi kurudi kwenye nafasi waliyowahi kuwa nayo kwa kushindana na CHADEMA…yaani kwa mgongo wa CHADEMA. That is missing the whole point. Wananchi wanaona. Wanajua. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kama alivyosema jana Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, tunawatakia kila la heri kufanya kazi ya siasa zenye tija. Lakini mpango wenu huo ukishindikana Arusha, ndiyo basi tena. Maana hiyo ilikuwa eneo lengwa kuu katika kutafuta justification.[/FONT]

   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa hawana tena mpango uanotekelezeka.Chadema wamewaweka mahali wanatembelea vidole na Mungu ana abort kila mpango prematurely.CDM wapo too dynamic kwa mipango statici ya CCM na serikali yake kufit in.
   
 3. commited

  commited JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mungu atawalipa stahiki awanayohitaji, njaa mbaya sana, wao CUF walifanyiwa mengi mabaya lakini CDM haikuwa kuiunga mkono serikali na CDM wamewaunga mkono sana CUF katika chaguzi mbalimbali tangu 1995, mpaka mwaka 2005 walipoamua kujitegemea baada ya kuona CUF hawako tayari kuwaunga mkono CDM...

  CUF Wanajiua wenyewe kwakupambana na CDM badala ya kupambana na watawala wa CCM. Lakini yanamwisho na mwisho Watajulikana tu na mipango yao michafu ya kutumika.
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Plain and to the point. Thanks 2Mine
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  wao wanatujia na majungu, sisi tunawajia na neno la Mungu.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  V4C = Victory For CHADEMA.
   
 8. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lisemwalo lipo!
   
 9. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hebu Ipe jina hii illustration 007.

   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Plan za kijinga sana hizo,watadunda tu kwani wameshagundulika.
   
 11. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,969
  Likes Received: 6,746
  Trophy Points: 280
  Hii nimeipenda, kwa hiyo kucopy na kupaste kwao kumearbort.Maana hizo slogan zote 2, owner ni CDM, kwa maana ya Movement 4 change= Victory 4 Chadema!!
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  OK I will...
   
 13. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mimi sijawahi kutamka jina la kiongozi yeyote wa CUF kwasababu moyoni huwa naamini kabisa ni MAMLUKI WA CCM AU WAGANGA NJAA,wakipata mtu akawawezesha vizuri wote watakuwa kama ZZK.
   
 14. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Ukweli mtupu. Umewanyima hata cha kuongea hao Pro-Mateso oooops I meant Pro-CCM
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  M4C is within i and i, brethren and sistren Cuf is just a puppet on a string! Ccm you just cant run away from your sweat, its all over you smellin like a rotten rat. Cdm has emancipate us from mental slavery you subjected us to, now its a revolution to redeem our soul!
   
 16. a

  abousalah2 Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bias
  hii ni habari au kampeni
   
 17. B

  Bin omary Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kijana niseme kama umekurupuka. Wengi wa wenu wana cdm mumekuwa mukisema kwamba ccm na cuf wana ndoa moja. Nataka mutoe ushahidi wenu. Je? Ni wazir gani au naibu waziri au nafasi gani ya uongozi katik SMT aliyetoka cuf.
   
 18. m

  manucho JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ukishaolewa, mambo ya kulala bila pichuna siyo kitu cha kuuliza. Ni kuchezea shekel pin tu
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vuguvugu la mabadiliko ni imani ambayo watanzania wamesadiki. Ni ngumu kuizuia kwa sasa especially kwa mbinu kama hizi. Wanaopanga hii mikakati wajue kwamba watanzania wanataka mabadiliko. Na hiyo ndiyo imani yao.
   
 20. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nyerere alisema wakikoseka viongozi safi ndani ya CCM, watanzania watawatafuta nje ya CCM.......
   
Loading...