Mjue Eugene Maganga mhusika wa njama za kuipindua Serikali ya Rais Julius Nyerere Januari 9, 1982

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
MJUE EUGENE MAGANGA MHUSIKA WA NJAMA ZA KUIPINDUA SERIKALI YA RAIS JULIUS NYERERE Jan 9, 1982.

"Tunajutia tu kushindwa mapinduzi, lakini hatujutii kupanga mapinduzi" -Capt. Eugene Maganga.

JAN 9, 1982 Palitokea jaribio la kuipindua serikali ya Rais Julius Kambarage Nyerere, rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Baba wa taifa) jaribio lililoshindwa kufanikiwa kwa kile kinachotajwa kuwa ni uimara wa kitengo cha intelejensia (usalama wa taifa) ya rais Nyerere.

Kwa ufupi kabla ya jaribio la kumpindua Rais Nyerere la mwaka 1982, palikwisha tokea majaribio mengine mawili awali, jaribio la kwanza lilitokea mwaka 1964 almaarufu kama "Maasi ya kijeshi ya mwaka 1964" na jaribio la pili ni jaribio la Mapinduzi la mwaka 1970." Na Yote yalishindwa kumng'oa gwiji huyu wa siasa za ukombozi wa Afrika.

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1982, hili ni jaribio la mwisho kabisa la mapinduzi katika uongozi wa rais Julius Nyerere na jaribio la mwisho kabisa kutokea katika utawala wa maraisi wa Tanzania, hakuna mtawala yoyote mwengine aliyefanyiwa jaribio la kupinduliwa tokea hapo na jaribio hili linalotajwa kuwa ndio jaribio la mapinduzi yakukusudia kabisa kuukomesha uongozi wa Julius Nyerere kama rais wa watu wa Tanzania.

Ni nani huyu capt. Eugene Maganga?
Eugene Maganga alizaliwa katika kijiji cha Itaga, Mkoani Tabora mnamo Mwaka 1956, alisoma na baadae kujiunga na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 1976 na kufanikiwa kupanda cheo hadi renki ya kepteni, kufikia mwaka 1982.

Akiwa Jeshini, Maganga alikuwa askari shupavu, mwenye utimamu na utayari kama askari kamili, pia alipata mafunzo maalumu ya kijeshi jijini London, Uingereza. Kepteni Maganga anatajwa Kama mmojawapo wa askari waliokuwa mstari wa mbele na waliotusaidia sana katika kushinda vita vyetu na fascist Iddi Amini Dada wa Uganda kati ya mwaka 1978-1979.

Mei 1980, Eugene Maganga alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza Uhusiano wa Kimataifa na Utawala wa Umma. Yapo yanasemwa kwamba Maganga aliamua kusoma kozi hii ili kujiandaa na majukumu ya kiutawala mara baada yakuja kufanikiwa kwa mpango wake wa kuipindua serikali ya Julius Nyerere, mpango uliokuja kushindwa.

-Wazo la kuipindua serikali ya Julius Nyerere.

Inasemekana wazo la kumpindua Nyerere, liliishi kichwani kwa Maganga tangu akiwa vitani (Vita vya Uganda kumg'oa Iddi Amin), na baada ya kumalizika Kwa vita, wazo lake lilishamirishwa na kile alichokiita "Kuyumba kwa Mwalimu Nyerere" na chini chini alimshutumu Mwalimu kwa matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, Maganga hakukubaliana na sababu za Mwalimu Nyerere kuingiza nchi vitani kupigana na Idd Amin.

Wazo la kumpindua Nyerere halikuwa kichwani mwa Maganga peke yake, bali lilikuwa wazo la askari kadhaa hususani wale waliopigana vita vya Uganda, baadhi ya askari walirudi wakiwa na mtizamo tofauti juu ya sababu za kweli za Mwalimu Nyerere kumpiga Amin, askari hao walikuwa na mtizamo kwamba Mwalimu hakupigana vita kwa maslahi ya taifa, bali kwa maslahi yake na rafiki yake Milton Obote. Kumrejesha madarakani.

- -Mpango wa Mapinduzi ulivyopangwa.

Awali Mpango ulikuwa wa watu wasiozidi kumi; Mohamed Tamimu, Eugene Maganga, Suleiman Kamando, Zakaria Hans Pope, Vitalis Mapunda, Mbogolo, Kajaji Badru, Hatibu Gandhi (Hatty MacGhee) na Christopher Kadego, lakini baadae watu wengine waliongezwa katika mpango ili kukidhi haja ya mpango huo wa Mapinduzi.

Maganga na wenzake, walikutana na Marehemu Pius Rugangira (Uncle Tom) ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Tanzania aliyejiimarisha sana kiuchumi nchini Kenya. Baba yake Rugangira hakuwa na uhusiano mzuri na Rais Nyerere, kwamujibu wa Maganga, naye alikuwa amekwenda kuishi na kufanyakazi nchini Uganda. Na kwasababu yakuwa Uganda, Rugangira alishutumiwa kuwa ni mpelelezi toka Uganda, shutuma ambazo zilisababisha mtafaruku na serikali ya rais Nyerere.

Rugangira alimua kuwasikiliza wapanga mapinduzi akatathimini mpango wao na baadae aliamua kugharamia shughuli hio, hasa pale walipofikia kukubaliana kuwa Bwana Rugangira ndiye atachukua nafasi ya Nyerere baada ya Mapinduzi kufanikiwa, baada ya hapo Maganga na maafisa wenzake wa jeshi ambao waliokubaliana katika mpango huu walijiweka sawa zaidi katika kuimarisha shambulio siku itakapo wadia. Wakiwa sasa wamepata uhakika wa msaada kutoka kwa Rugangira.

Pamoja na kwamba wana Mapinduzi walikubaliana na Rugangira kuwa ndiye atakuwa Raisi baada ya Mapinduzi lakini mioyoni mwao hawakuwa na ukweli huo, walikuwa wakiitaji msaada wa kifedha tu na baadae wangemgeuka, tungewaza kuthibitisha hili kama mapinduzi yale yangefanikiwa.

Wakati mipango yote ilipokuwa tayari ,walisubiri kuwasili kwa rais ambaye alikuwa katika ziara nje ya nchi. Kwa mujibu wa Maganga, rais alirudi Januari 1982 baada ya kukaa miezi miwili nje ya nchi na akaenda kijiji kwao Butiama ."Sababu ya kutaka kuipindua serikali wakati yeye akiwa nchini ni kwamba tulikuwa na nia ya kumuua". Maganga aliwahi kusema. Alikuwa Rugangira aliyepinga mpango huo na badala yake alipendekeza kumkamata rais.

-Mpango wa Mapinduzi ulivyoshtukiwa.

Inasemekana mpango wa mapinduzi haya ulivuja kutoka kwa askari mmoja aliyehusika na mpango huu, kulewa na kuanza kuropoka ovyo habari za Mpango wa mapinduzi, Bwana huyo akiwa umeutwika (amelewa) alitaja baadhi ya Majina ya maafisa waliomo kwenye mpango huo na vyeo watakavyopewa baada ya mapinduzi kufanikiwa, Hapo ndipo intelejensia ya Mwalimu iliponasa habari na kuanza kuzifanyia kazi, ingawa inasemekana pia taarifa zilikwisha wafikia watu usalama mapema zaidi.

Katika Majina yaliyonaswa na maafisa usalama wa Mwalimu Nyerere, Mtu hatari zaidi alionekana kuwa ni Mohamed Tamimu. Tamimu alikuwa komandoo aliyewiva vizuri, akipata mafunzo ya kijeshi ya hali ya juu (Komando) nchini Cuba, Tamimu ni mmoja Kati ya makomandoo wa Kitanzania aliyesifiwa sana na Fidel Castro kwa umahiri wake, alifanya Vizuri sana mafunzoni. Hivyo intelejensia ya Mwalimu ilikuwa lazima ihakikishe inamthibiti Tamimu kwanza, na pengine kwa kumthibiti Tamimu wengine wangeogopa na kujisalimisha.

Ilikuwa ni kazi yenye uzito wake kwa maafisa usalama wa Nyerere katika kuhakikisha mpango wa Maganga na wenzake unakufa, walimshauri Mwalimu aendelee kubaki kijijini kwao Butiama asirudi kwanza Dar es Salaam hadi watakapo weka mambo sawa. Kuwathibiti Maganga na genge lake la wanamapinduzi.

Ijumaa kabla ya Januari 6, 1982, ilikuwa ni siku ambayo wapanga Mapinduzi walikuwa wamepanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla ya kufanya utekelezaji wa mpango wao wa mapinduzi siku tatu zijazo yaani Januari 9, 1982, lakini baadhi ya wenzao hawakutokea kwenye mkutano. Akiwemo Tamimu

"Tulikuwa na wasiwasi na tuliamua kutuma mmoja wetu Kinondoni Mkwajuni kuuliza lakini tulishtuka kuona kwamba polisi walikuwa wamevamia nyumba yake na aliuawa katika mapambano yaliyodumu saa mbili akifukuzwa kutoka uwanja wa Leaders, alipofika Kinondoni eneo maarufu la sinema (ubalozi wa Marekani leo) alizidiwa nguvu na kuuawa na kikosi cha majasusi kilichokuwa kikiongozwa na jasusi na mwanasheria nguli Mabere Nyaucho Marandu". alipata kusema Maganga.

Katika hatua hiyo, walijua utambulisho wao na mipango yao haikuwa siri tena. Tamimu, kwa mujibu wa wenzake, alikuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu za mikutano na majina ya washirika. Ilikuwa ni suala la muda tu kabla hawajakamatwa. Tamimu alipangwa kuwa mdunguaji maalumu kwaajili ya kumuua rais Nyerere aliyekuwa akirejea toka nje ya nchi. Hisia zao zilikuwa sahihi. Polisi walikuwa kila mahali kusaka kikundi.

Kadego na Maganga waliamua kutoroka kupitia Tanga na Mombasa hadi Nairobi ambako walikaa kwa miezi kumi kama wakimbizi wa kisiasa. "Hatujui nini kilichotokea kwa watu wengine ambao tuliwaacha Dar es Salaam lakini hatukukata tamaa tulipofika Nairobi. Tulitaka kujipanga tena na kurudi kuipindua serikali , "alisema Maganga .

Kamwe hawakuweza kulaumiana wao kwa wao kwa kushindwa kufanya mapinduzi ingawa Maganga anaamini bahati yao iliondoka kwa sababu MacGhee alikuwa raia wa kawaida na hakujua jinsi ya kutunza siri . Anamtuhumu MacGhee kwa kuvujisha taarifa kwani karibu watu wote walijua kabla ya kukakimilka kwa mpango.

Maganga pia anahisi kuwa Tamimu alijua kwamba MacGhee hakuwahi kuwa askari wa Marekani kama alivyokuwa akidai lakini hakuwaambia . " Tuligundua baadaye kwamba jina lake halisi alikuwa Hatibu Hassan Gandhi na alikuwa rubani wa Tanzania " Mjini Nairobi , hawakuwa na ajira na walikuwa wanaishi chini ya msaada wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi.

Maganga anasema walikuwa na baadhi ya mawasiliano na ubalozi wa Marekani mjini Nairobi ambako waliomba udhamini na kuanza msingi upya jijini Nairobi ambapo wangeweza kujipanga vizuri na kupanga kwa ajili ya mapinduzi mengine ."Walisema walikuwa na shughuli nyingi zinazofanana na wasingeweza kutuunga mkono". alisema Maganga.

Siku chache baadaye Maganga na Kadego wakizunguka katika mitaa ya Nairobi, ghafla waliingia kwa mpanga mapinduzi mwenzao Uncle Tom na MacGhee waliyekuwa wamemwacha Dar es Salaam . Wawili hao walikuwa wamekimbia toka gereza la Keko jijini Dar es Salaam ambako walikuwa wamewekwa baada ya kukamatwa kwao.

Ingawa walikuwa huru na maisha yao mjini Nairobi Rugangira aliamua kusafiri kwenda London kuangalia namna ya kuingia Malawi. Alikuwa na mashaka kuwa serikali jijini Nairobi na Dar es Salaam zinaweza kula njama na kuwakamata. Wote nane walikuwa kwa namna fulani wameweza kutoroka kwenda Nairobi.

Kukamatwa kwa wapanga mapinduzi
Kabla Rugangira kurudi kutoka London, kundi hili lilikamatwa na mamlaka jijini Nairobi na kubadilishana na Senior Lance Koplo Ochuka na Sergeant Pancras Oteyo ambaye pia alifanya majaribio ya kuipindua serikali ya Rais Daniel Arap Moi mwaka 1982 na walikimbilia Tanzania .

"Tulifungwa sana pingu na kufunikwa macho na kupelekwa gereza la Isaka lenye ulinzi wa hali ya juu mjini Dodoma ambako tulikaa kuanzia Novemba 1983 hadi Oktoba 1984", alipakusema Maganga .

-Hukumu ya wapanga mapinduzi.

Mwaka 1985 Maganga na wenzake saba; Suleiman Kamando, Zakaria Hans Pope, Vitalis Mapunda, Mbogolo, Kajaji Badru, Hatibu Gandhi (Hatty MacGhee) na Christopher Kadego walihukumiwa kufungwa maisha jela. Pius Lugangila alitoroka.

-Msamaha wa Maganga na wanamapinduzi wenzake.

Jumamosi asubuhi ya Oktoba 22, 1995 Maganga aliamka mapema na alipowasha radio yake ndogo, ulikuwa wakati muafaka kwake kupata taarifa fupi zikisema kwamba Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa msamaha kwa wafungwa akiwemo yeye pamoja na wafungwa wengine wengi.

Huu ni wakati ambapo kundi la watu wanane walikuwa wakiusubiri, kwa miaka kumi ambayo wamekuwa kifungoni wakitumikia kifungo cha maisha kwa uhaini.

Kamwe hawakuweza kupoteza matumaini. " Wafungwa katika jela mbalimbali ambao pia walisikia habari hizi walianza kushangilia ,"anasimulia Maganga." Cha kushangaza sikufurahia kwa sababu nilikuwa naisubiri siku kama hii kwa muda mrefu. Mara zote ilikuwa inatisha kufikiria kuwa ningeweza kutumia maisha yangu yote gerezani. "

Jumatatu Oktoba 24, 1995, siku mbili baada ya habari kufika kwenye redio, Maganga alitangazwa kuwa mtu huru. Anakumbuka vizuri siku hiyo alipovuka milango ya gereza kwa uhuru. Ilikuwa ni majira ya saa saba mchama. "Tulikaribishwa nje ya gereza na ndugu zangu wenye furaha pamoja na wale wa mfungwa mwenzangu Hatty MacGhee . Hisia zangu zilikuwa juu kiasi kwamba ni vigumu sana kuelezea kwa sasa ," anasema Maganga. Wafungwa wengine sita wa uhaini waliachiwa siku mbili baadae kutoka Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Wakati wa kutolewa kwao, Maganga alikuwa amezungushwa katika magereza kadhaa ikiwa ni pamoja na Ukonga jijini Dar es Salaam na sehemu yake ya mwisho ilikuwa Butimba jijini Mwanza. Licha ya matatizo waliyovumilia gerezani, Maganga anasema hakuna hata mmoja wao aliyewahi kujuta kwa kujaribu kuipindua serikali. "Tunajutia tu kushindwa mapinduzi lakini hatujutii kupanga mapinduzi".

-Maisha ya Maganga baada yakutoka gerezani.

Baada ya kutoka gerezani 1995, Maganga hakuwa na kazi aliishi maisha Magumu sana, na alidai, baadhi ya rafiki zake wa zamani walifikia hatua ya kumkimbia waziwazi wakati alipoonyesha amewaona na akitaka kuwasogelea. Alidai kuwa baadhi ya ndugu, walimpiga marufuku asikanyage katika nyumba zao.

“Inawezekana wengi hawakubaliani na kile tulichotaka kukifanya lakini walau tulifanya maamuzi. Mtu anaweza kufanya uamuzi mbaya au mzuri lakini ni afadhali huyo kuliko anayelalamika tu kila siku bila ya kufanya lolote. Hapa ndipo ninapotaka tubadilike,” -Maneno ya Maganga.

Mwaka 2004, Maganga aliamua kujitosa kwenye ulingo wa siasa, akajiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hii ilitokana na hofu kuwa asingeweza kukubalika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichopata kukifanya mwaka 1982.

Mwaka 2005, Maganga alijitokeza kuwania ubunge kupitia CHADEMA katika Jimbo la Tabora Mjini ambako hata hivyo alishindwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Siraju Kaboyonga.

Kutokana na uwezo wake na taaluma yake kama askari mahiri, Akiwa CHADEMA alipewa kazi kama ofisa katika Kurugenzi Ulinzi na Usalama nafasi aliyoipoteza alipohamia CCM.

Jumatano, Januari 10, mwaka 2007, Maganga alitangaza kuhama CHADEMA na kuhamia CCM akidai kwamba hakuridhishwa na namna vyama vya upinzani vilivyokuwa vikiendeshwa.

“Kile nilichokitarajia, sicho nilichokutana nacho katika upinzani. Hakuna mfumo mzuri wala utaratibu. Kwa mwenendo huu, hatuwezi kufika kokote,” - Maganga

Hatua hiyo haikubadilisha maisha yake kwa namna yoyote. Hali yake ya maisha iliendelea kuwa ileile hadi mauti yanamkuta, Octobar 2010, nakuzikwa kijijini kwao Itaga Mkoani Tabora.

1635365786705.jpg
 
Kwa hiyo Pius Lugangira ndiye aliyewachoma? Yeye ndiye alikuwa snitch kwenye hilo kundi na ndiyo maana aliweza kutorokea UK wakati wenzake wanasota jela. Tena inawezekana serikali ilimsaidia kuhamia UK. Hiyo stori ya kulewa na kulopoka ndiyo wana usalama wakajua si ya kweli.
 
Kwa hiyo Pius Lugangira ndiye aliyewachoma? Yeye ndiye alikuwa snitch kwenye hilo kundi na ndiyo maana aliweza kutorokea UK wakati wenzake wanasota jela. Tena inawezekana serikali ilimsaidia kuhamia UK. Hiyo stori ya kulewa na kulopoka ndiyo wana usalama wakajua si ya kweli.
Pombe ilisababisha siri hii kuvuja
 
Kwa hiyo Pius Lugangira ndiye aliyewachoma? Yeye ndiye alikuwa snitch kwenye hilo kundi na ndiyo maana aliweza kutorokea UK wakati wenzake wanasota jela. Tena inawezekana serikali ilimsaidia kuhamia UK. Hiyo stori ya kulewa na kulopoka ndiyo wana usalama wakajua si ya kweli.
Pombe ilisababisha siri hii kuvuja
Uzuri wa walevi... Hawadanganyi!!
😀
 
soma hapa vizuri "
Mpango wa Mapinduzi ulivyoshtukiwa.

Inasemekana mpango wa mapinduzi haya ulivuja kutoka kwa askari mmoja aliyehusika na mpango huu, kulewa na kuanza kuropoka ovyo habari za Mpango wa mapinduzi, Bwana huyo akiwa umeutwika (amelewa) alitaja baadhi ya Majina ya maafisa waliomo kwenye mpango huo na vyeo watakavyopewa baada ya mapinduzi kufanikiwa, Hapo ndipo intelejensia ya Mwalimu iliponasa habari na kuanza kuzifanyia kazi, ingawa inasemekana pia taarifa zilikwisha wafikia watu usalama mapema zaidi.
 
soma hapa vizuri "
Mpango wa Mapinduzi ulivyoshtukiwa.

Inasemekana mpango wa mapinduzi haya ulivuja kutoka kwa askari mmoja aliyehusika na mpango huu, kulewa na kuanza kuropoka ovyo habari za Mpango wa mapinduzi, Bwana huyo akiwa umeutwika (amelewa) alitaja baadhi ya Majina ya maafisa waliomo kwenye mpango huo na vyeo watakavyopewa baada ya mapinduzi kufanikiwa, Hapo ndipo intelejensia ya Mwalimu iliponasa habari na kuanza kuzifanyia kazi, ingawa inasemekana pia taarifa zilikwisha wafikia watu usalama mapema zaidi.
Ukizingatia Mwl Nyerere alikua na upeo mkubwa sana wa akili, kufanikisha azima hiyo isingekua rahisi hasa tukitizama mpango wa Idd Amin ulivyoshindwa, inaonesha ni jinsi gani kumkabili Mwl Nyerere ilikua vigumu sana
 
Kwa stori hiyo msishangae kuona akina mbowe wanatuhumiwa kwa ugaidi, lolote laweza kutokea!
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Mbowe kwasababu makosa yake hayajawekwa barabara kwamba alifanya wapi na muda gani, pengine Mahakama itaweka wazi tusubiri uamuzi wa mahakama kama chombo kikuu cha sheria
 
Mwishoooni alikuwa akinywa pombe maeneo ya Sinza, niliwahi kumnunulia pombe. Ulikuwa ukimnunulia pombe anakupa story zote za mipango yao hadi kutoka Gerezani!
Alikuja kuwa ndugu na rafiki yangu .Jamaa alikuwa kichwa Sana sema kukaa gerezani na kutengwa vilimuathiri Sana.Waroto wake kina Ray (chotara) walikosa wakuwasaidia.Hivi Kadagho yuko wapi?
 
Kwa hiyo Pius Lugangira ndiye aliyewachoma? Yeye ndiye alikuwa snitch kwenye hilo kundi na ndiyo maana aliweza kutorokea UK wakati wenzake wanasota jela. Tena inawezekana serikali ilimsaidia kuhamia UK. Hiyo stori ya kulewa na kulopoka ndiyo wana usalama wakajua si ya kweli.
Uncle Tom hakuwa na asingeweza kuwasnitch.Aliyechomesha ni McGhee.Wengine wanadai,usalama wa taifa na polisi walikuwa wanamtafuta mhalifu mwingine tuu,wakapata fununu .Ilikuwa coincidence tu wanadai
 
Back
Top Bottom