Njama za kuisafisha TBS zaandaliwa na kuwahusisha baadhi ya wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njama za kuisafisha TBS zaandaliwa na kuwahusisha baadhi ya wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 26, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  Ripoti uozo TBS yaiva- Njama za kuizima zaandaliwa

  Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma ( POAC) imebaini matatizo mengi ndani ya TBS yakiwemo ukaguzi wa bidhaa usiokidhi viwango na mazingira ya rushwa miongoni mwa maofisa waandamizi. Na kutokana na kubainika kwa madudu hayo, Kamati hiyo imependekeza baadhi ya maofisa waandamizi wa TBS, akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Charles Ekelege, wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

  Na licha ya Kamati ya Bunge kukamilisha ripoti yake hiyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti la Uhuru unaonyesha kuwa kuna mipango inasukwa kwa kuwahusisha baadhi ya wabunge, ofisi ya bunge na wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha suala hilo halifikishwi katika mkutano ujao wa bunge na kuchukuliwa hatua.


  Uchunguzi wa gazeti Uhuru unazidi kuonyesha , kuwa wahusika wa mpango huo ni baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) na maofisa wa bunge kwa kushirikiana na maofisa waandamizi wa wizara.


  Kwa mujibu wa gazeti Uhuru, mmoja wa wajumbe wa POAC alithibitisha kuwepo mipango hiyo na kuongeza kuwa, baadhi ya wabunge wanatumiwa katika suala hilo.

  Mjumbe mwingine wa kamati hiyo alisema, kwa uozo ndani ya TBS uko wazi kwa sababu hata wafanyakazi wa chini wamekuwa wakilalamika kuwa wanakwamishwa kufanya kazi ipasavyo na viongozi wao.

  ” Wafanyakazi walitueleza kuwa wanapogundua kuna bidhaa mbovu na kuzizuia, wafanyabiashara wanazungumza moja kwa moja na viongozi wa juu wa shirika na matokeo yake bidhaa zile ambazo ni mbovu zinaruhusiwa kutumika.

  ” Kama watu walioaminiwa na kupewa nafasi kuongoza shirika kubwa kama hili wanakiuka utaratibu, kuna imani gani tena? Hii inaonyesha watu hawa hawana nia njema na maisha yetu na wako tayari kuwaangamiza Watanzania kwa sababu ya maslahi yao”. Alisema mjumbe huyo.

  Kwa mujibu wa gazeti Uhuru, Makamu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge , Mbunge wa Ludewa , Deo Filikunjombe, ameweka bayana msimamo wa kamati yake, kuwa hawatakubali suala hilo kuzimwa au kumalizwa kinyemela kwa sababu kufanya hivyo ni kukubali Watanzania waendelee kuangamia kwa kutumia bidhaa mbovu.


  Filikunjombe anasema;


  ” Upo ushahidi kwamba zipo bidhaa zisizo na viwango kama kondomu, mafuta ya kupikia, matairi, vyakula na blue band ambazo zina nembo ya TBS na zinatumika. Huu ni uoza mkubwa, ni lazima tufike mahali tuseme basi. Ni lazima TBS isafishwe na wahusika wa mchezo huu mchafu lazima waondolewe haraka”. ( Deo Filikunjombe, Uhuru Februari 25, 2012)
   
Loading...