Njama za kudhoofisha Chadema-NCCR ubunge wa kuteuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njama za kudhoofisha Chadema-NCCR ubunge wa kuteuliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]
  Uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa na Rais Kikwete wa hivi karibuni akiwemo mmoja kutoka chama cha upinzani NCCR Mageuzi ni kitendawili kilichoteguliwa tayari na mteule licha ya ukweli kujulikana hadharani hivi karibuni.

  Historia ya habari hii inaanzi huko miezi michache iliyopita ambapo aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Halima Mdee kushindwa uchaguzi na hivyo kupinga mahakamani ambapo kesi yake imefutwa baada ya pande mbili za vyama vya upinzani Chadema na NCCR Mageuzi kukaa meza moja na kukubaliana kufuta kesi hiyo kitendo kilichomhalalisha Mdee Kuendelea na Ubunge wake kwa makubaliano nje ya mahakama.

  Hatua hiyo imewaumiza sana CCM na hivyo kufanya njama za kushinikiza huyo aliyeshindwa uchaguzi ateuliwe na Rais kuingia bungeni ili kujaribu kuleta mpasuko wa mahusiano kati ya Chadema na NCCR Mageuzi. Kitendo cha uteuzi huo kiliwashangaza wengi kwani hakikutegemewa, na kwa vyo vyote kuna kila dalili ya kuwa na kitu kinachoendelea nyuma ya pazia.

  Mteule anaonekana kushtukia deal hiyo, na hivyo kutamka hadharani kwamba hayuko tayari kuwa chambo cha kudhoofisha vuguvugu la mageuzi ndani ya kambi ya upinzani kwa kuteuliwa na Kigogo wa CCM kuingia bungeni, bali atakuwa bega kwa bega kujenga hoja ya utetezi wa wapinzani wenzake dhidi ya wabunge wa CCM.

  Ndoa ya Chadema na NCCR Mageuzi ina dalili ya kuimarika ingawa haionyeshi wazi kwa nje, ila kwa vyo vyote kuna kila dalili ya kufanya kazi kwa karibu na pamoja zaidi.

  Mfano dhahiri ni huu wa Makamanda wa Chadema kutanguliziwa kwenda kanda ya kusini NCCR Mageuzi kusafisha njia na kutengeneza mazingira ya kupita Chadema. Dalili hizi njema zinaweza kuigwa na vyama vingine vya upinzani kuunganisha nguvu kuing'oa CCM kama ilivyotokea kule Kenya upinzani ukiongozwa na Mwai Kibaki kuisambaratisha kabisa KANU.

  [​IMG] [​IMG]
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  well said
  ila ningependa kufahamu kwani rais haruhusiwi kuchagua mbunge upinzani?
  kama ndio kuna ubaya gani kumchagua Mbatia?
  huoni ameongeza kiti cha upinzani bungeni?
  nijuavo hajachaguliwa kwa maslahi ya CCM bali atawajibika kama mbunge.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sababu ya Rais kutengewa viti vya wabunge wa kuteuliwa naye ni kutokana na hitaji zaidi la Rais katika kuteua watendaji ambao wanatakiwa watokane na kofia ya ubunge kikatiba. Kwa vile Waziri kwa mfano hawezi kuteuliwa mpaka awe mbunge, hivyo kama Rais anamwona mtu anayefaa katika nafasi fulani na papo si mbunge basi anachoweza ni kumteua kuwa mbunge kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

  Kinachochatakiwa ni katika katiba mpya kufanya mabadiliko ya kupunguza mamlaka ya rais, hivyo kama mmoja anateuliwa kutoka nje ya wabunge anatakiwa athibitishwe na mkutano wa bunge, huu utaratibu umezoeleka katika nchi nyingi hata mataifa makubwa duniani.
   
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  kwani nccr bado ipo!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama haipo Kikwete angewezaje kumchagua mbunge toka Chama hicho? Mbunge Kafulila anatoka chama gani kama si NCCR Mageuzi?
   
Loading...