Njama mbaya dhidi ya watu wasio na hatia ugeuka na kuwa kilio kwa wanaozipanga na neema kwa waliokusudiwa mabaya

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu wanaopenda kufatilia mambo mbalimbali yanayoendelea duniani na hasa wale wanaofatilia maandiko matakatifu ya vitabu vitakatifu watakubaliana na mimi kuwa njama mbaya dhidi ya watu wasio na hatia ugeuka kuwa kilio kwa wanaozipanga na neema kwa waliokusudiwa mabaya.

Nitatoa mifano michache kutoka kwenye Biblia.
Katika kitabu cha Mwanzo 37 tunajifunza jinsi ndugu zake na Yusufu walivyomkusudia mabaya na kupanga njama ya kumwangamiza. walimtupa shimoni na kisha kumuuza kwa wamisri, ila Mungu aliyahifadhi maisha yake na siku moja alikuja kuwa msaada kwa ndugu zake na wote walimwinamia.

Katika kitabu cha Esta 3 kuna mtu aliyekuwa anaitwa Hamani bin Hamedatha alipanga njama mbaya ya kumwangamiza Mordekai na wayahudi, akatengeneza mkakati mkubwa na maandalizi yote yalikamilika mfalme akaidhinisha, matokeo yake mambo yalikuja kubadilika na yule aliyepanga njama pamoja na watu wake wote waliangamizwa na yule aliyekusudiwa mabaya alipandishwa cheo.

Katika kitabu cha Daniel 3 tunawaona vijana watatu Shedrack, Meshack, na Abadnego walifanyiwa njama mbaya za kuwaangamiza hadi wakatupwa kwenye tanuru la moto, ila walitoka wakiwa wazima na matokeo yake wale wote waliowalia njama waliangamizwa na hao vijana kupandishwa vyeo.

Katika kitabu cha Daniel 6 tunamuona Danieli akipangiwa njama mbaya hadi kutupwa kwenye tundu lenye simba wakali ila hawakumla, wale waliopanga njama walitupwa humo na watoto wao hawakuweza kupona hata mmoja.

Kama mtu anaweza kupigwa risasi 16 akaendelea kuishi tafadhali sana achaneni naye, inawezekana kabisa kuna kusudi la Mungu ndani yake, msije kupambana na mkono wa Mungu mkajikuta mahali pabaya na kusababishia familia zenu maafa. NI USHAURI TU.
 
Ukweli mtupu bali mchungu upande ule lakini ,uchungu wanaoupata hautabadilisha mipango ya mungu ,sidhani kama Lumumba wataonekana hapa.
 
Ukweli mtupu bali mchungu upande ule lakini ,uchungu wanaoupata hautabadilisha mipango ya mungu ,sidhani kama Lumumba wataonekana hapa.

Naamini kila mtu mwenye ufahamu wa kutosha ataogopa sana kuwatendea mabaya na kupanga njama mbaya dhidi ya watu wasio na hatia.

Kwa wanaojishughulisha sana na huyu jamaa watajishangaa sana...hivi mtu kapigwa risasi hajafa bado mnamwandama tu mnashindwa kujua kuwa kuna mkono wa Mungu juu yake? Nawaonya sana mjiepushe na mtu kama huyo
 
Back
Top Bottom