Njaa yabisha hodi Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njaa yabisha hodi Tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Jul 14, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wakuu habari zenu,

  Njaa imebisha hodi Tanzania dalili zote tayari zimejidhihirisha,bei ya vyakula imepaa wananchi wa kipato cha chini na kati hawamudu milo mitatu kwa siku.Nimetembelea sehemu mbali mbali [Karatu,Katesh,Dongobesh,Hanang,Babati,Haydom,Himo,Rombo,Marangu,Handeni,Soni na Muheza] kote huko njaa imetamalaki hakuna chakula cha kutosha sokoni.

  Bei ni tatizo debe la mahindi linauzwa kati ya tsh 10,000/= mpaka 15,000/= serekali imeshindwa kuingilia kati kwa kuruhusu akiba ya mahindi yake SGR inasaidia kushusha bei ili mlaji wa mwisho apate unafuu wa bei.

  Nilishuhudia mwenyewe malori makubwa Scania yakivusha mahindi mpakani Holili kwenda nchini Kenya.Vyombo vya ulinzi na usalama havichukui hatua ya kuzuia uvusha wa chakula nchini.

  Arusha nimeshuhudia mwenyewe wananchi wakiwa kwenye foleni ndefu ya unga NMC kwa masharti mengi ikiwa ni pamoja na kuuziwa mfuko mmoja tu !.Huu ni mwezi wa 7 hali ni mbaya kiasi hiki je mwezi wa 8,9, hadi 10 hali itakuwaje ?.
   
Loading...