Njaa ya miaka 10 itakuja kuliangamiza Taifa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Hakuna ubishi sasa hivi mafisadi yamebanwa kwenye kona mbaya, yanalalamika kwa kuzibiwa vichochoro vyao vya kupiga madili.

Bila shaka kwa miaka 10 ya Rais Magufuli madarakani yatakuwa yamedhoofu kwa njaa, kiu na kuishi kama mashetani, wanatamani miaka 10 ya Rais magufuli ipite haraka kama upepo.

Hofu yangu mimi ni baada ya miaka 10 ya Mh. Magufuli kumalizika kwa mujibu wa katiba yetu. Je, nini kitafuata ili kuendeleza moto aliouwasha JPM dhidi ya ubadhilifu nchini baada ya yeye kumaliza muda wake Ili juhudi za JPM zisipotee bure kama vile zilivyopotea zile za Mwl. Julius K. Nyerere (rip) baada ya kung'atuka urais 1985 watu wakakimbilia kulinyonga Azimio lake la Arusha na kuunda Azimio la Zanzibar?

Ni heri JPM atengeneze polepole utaratibu, chombo na mfumo ambao utakuwa na uwezo wa kupambana wenyewe na ufisadi na uvivu kabla hajamaliza kipindi chake badala ya kutegemea juhudi na ufundi wa mtu binafsi.

JPM anaifahamu vilivyo mianya iliyoko kwenye katiba na sheria zetu ambayo ni rahisi kutumiwa na watawala wenye nia mbaya, afanye kazi ya kuiziba polepole wakati anaelekea mwaka 2025, vingine majizi haya ambayo yatawekwa na njaa na hasira za miaka 10 ya JPM siku yakibahatika kuikamata Ikulu tena hakiyamungu taifa litakujajuta.
 
Fisadi hana shida zaidi ya vilaza kulia njaa....uliwahi sikia Mo au Bakhresa Analia sukari imepanda bei au nauli kubwa au ada iko juu??
 
Fisadi hana shida zaidi ya vilaza kulia njaa....uliwahi sikia Mo au Bakhresa Analia sukari imepanda bei au nauli kubwa au ada iko juu??
Umetumwa wewe toka zako mpelekee upuuz alie kutuma
 
Hakuna ubishi sasa hivi mafisadi yamebanwa kwenye kona mbaya, yanalalamika kwa kuzibiwa vichochoro vyao vya kupiga madili. Bila shaka kwa miaka 10 ya Rais Magufuli madarakani yatakuwa yamedhoofu kwa njaa, kiu na kuishi kama mashetani, wanatamani miaka 10 ya Rais magufuli ipite haraka kama upepo. Hofu yangu mimi ni baada ya miaka 10 ya Mh. Magufuli kumalizika kwa mujibu wa katiba yetu je, nini kitafuata ili kuendeleza moto aliouwasha JPM dhidi ya ubadhilifu nchini baada ya yeye kumaliza muda wake? Ili juhudi za JPM zisipotee bure kama vile zilivyopotea zile za Mwl. Julius K. Nyerere (rip) baada ya kung'atuka urais 1985 watu wakakimbilia kulinyonga Azimio lake la Arusha na kuunda Azimio la Zanzibar ni heri JPM atengeneze polepole utaratibu, chombo na mfumo ambao utakuwa na uwezo wa kupambana wenyewe na ufisadi na uvivu kabla hajamaliza kipindi chake badala ya kutegemea juhudi na ufundi wa mtu binafsi. JPM anaifahamu vilivyo mianya iliyoko kwenye katiba na sheria zetu ambayo ni rahisi kutumiwa na watawala wenye nia mbaya, afanye kazi ya kuiziba polepole wakati anaelekea mwaka 2025, vingine majizi haya ambayo yatawekwa na njaa na hasira za miaka 10 ya JPM siku yakibahatika kuikamata Ikulu tena hakiyamungu taifa litakujajuta.
Nimekuja mbio kusoma nikidhani ni mada ya maana, una uhakika gani kuwa Magufuli atashinda tena 2020?
 
Kwanza nikusahihishe hapo; katiba ya Tanzania haimfanyi rais kukaa miaka 10 katika ofisi ya urais bali ni miaka 5. Kila baada ya miaka 5 uchaguzi mkuu ni lazima ufanyike kuwachagua wawakilishi wa wananchi Bungeni na rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania.
Ukisemacho wewe ni utaratibu wa chama cha Mapinduzi kumpendekeza mwenyekiti wa chama katika muhula mwingine wa miaka 5. Hata huyo umuongeleaye anaweza asishinde muhula ufuatao kama wananchi wataamua wasimpitishe kwa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao.
 
nani kaondoka baada ya miaka 5?
 
Alaf hiz ramli za mchana ni mbaya mnoo acha kututisha ndio mnajiandaa tena kutuletea tabia za kikwenu ee ?
 
Hakuna njaa yoyote utabiri wa hali ya hewa umesema kutakuwa na mvua za kumbikumbi(nswa)mahindi bwelelee
db_zambian-food-nshima-nsima-ugali-sadza07inswa1.jpg
 
Mkuu hawa wadudu ni watam balaa kabisa nimewamiss zaid ya miaka miwili sijawapata senene mjinga kwa kumbikumbi
Mpaka leo wanasayansi wameshindwa kufananisha ladha ya kumbikumbi na ladha yoyote. ya samaki imo,ya mbuzi imo yaani hata ya mamba.
 
Wapiii kaone acha kutuletea tabia za kufikiri kuliko duni IQ yako ni ngapi ? UMETUMWA ee
IQ ndo nini? IQ mwenyewe, ala!! ulikuwa wapi wakati wa Mkapa vs. Mrema, Kikwete vs. Slaa na Rais Shein vs. Hamad? si tungeona hiyo nadharia yako ya 5 years kama inafanyakazi Tanzania? Hapa tumuombe tu Mh. Rais wetu atutengenezee na kutuachia mfumo ambao utakaowasaidia watanzania kukabiliana na viongozi na wafanya biashara wezi kwakuwa watanzania hawana uwezo wa kumkataa kumchagua kiongozi asiyefaa kwao. Unafahamu kuwa Tanzania tuna mfumo mzuri sana wa ulinzi ambao uliundwa enzi hizo kwa nia njema ya kutulinda dhidi ya maadui wa nje kama vile makaburu, wareno na majasusi wengine wakati ule wa harakati za ukombozi wa Afrika ambao sasa unatumika kwa kazi nyingine za ndani baada ya harakati za ukombozi wa Afrika kumalizika na idadi ya wale maadui zetu kupungua. Nafurahi sasa kuona Mh. Rais wetu akiutumia sasa kikamilifu katika kupambana na wakwepa kodi, wapiga dili, wezi na wahalifu wengine wakati wa enzi zilizopita viongozi wachafu waliutumia vibaya mfumo huo kwa kupigia madili yao, binafsi kama madawa, meno ya tembo, wahamiaji, kung'oa meno. Kwanini wewe uwe na mawazo ya kumpa miaka 5 tu mzalendo kama huyu ambaye badala ya kumuongezea miaka mingine 10 ili iwe 20 ya kuwanyorosha? Kuna nchi wanatamani angekuwa wao.
 
IQ ndo nini? IQ mwenyewe, ala!! ulikuwa wapi wakati wa Mkapa vs. Mrema, Kikwete vs. Slaa na Rais Shein vs. Hamad? si tungeona hiyo nadharia yako ya 5 years kama inafanyakazi Tanzania?

hahahahhhahahahaah ngoja nisije nikakuongezea tafran akilin uko stressed sasa nsije nikakuharibia siku tulia totoo tufanye umeshinda IQ bado hujajua ni nini ? bure kabisa hovyooo sijui umetumwa griiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mkuu Kuna ubaya gani kuniambia maana ya IQ na namna inavyofanyakazi zake? normal ni ngapi, ya juu ikoje, ya kwako ni iko ngapi, unakokotoaje na sababu ya kuwa chini au juu au kukosa kabisa, n.k. AU umesikia tu kwa watu wakisema kuhusu IQ? swine!!
 
Oyooooooo unaka-abnormality flan amazing
 
Back
Top Bottom