Njaa Somalia: Je, Tanzania itoe msaada kwa hawa wenzetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njaa Somalia: Je, Tanzania itoe msaada kwa hawa wenzetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 28, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Desperate: Seven-month-old Mihag Gedi Farah weighs just 7lbs and was hours from death after arriving at a field hospital in Dadaab, Kenya


  Ukiondoa Kenya na baadhi ya nchi za karibu ambazo zimejikuta na wakimbizi wa Somalia hasa kutokana na baa la njaa ni nchi chache za Kiafrika zimejitokeza kutoa misaada - as a matter of fact sijaona bado ni nchi gani. Tumekuwa na haraka kweli tunapoona nchi za magharibi zinakuja kutuondolea madikteta wetu na kuwakemea mara moja - ooh tuachieni Afrika tutatue matatizo yetu. Hatuchelewi kupeleka ujumbe Libya, Ivory Coast n.k ili kujionesha kuwa tunaweza kutatua matatizo yetu na kusaidiana wenyewe.

  Then comes Somalia. Ukiondoa matatizo mengine ya nyuma hakuna tatizo ambalo linagusa nafsi ya mwanadamu na utu wake kama njaa. Vita haikaribii njaa kwa madhara yake. Lakini inashangaza, hatujasikia viongozi wa Afrika wakimobilize watu wao kusaidia chakula huko! Hata sisi Tanzania hatujasema tunatoa japo msaada wa fedha au chakula - si kwamba hatuna uwezo. Lakini hadi hivi sasa ni hawa hawa wazungu tusiotaka watusaidie kwenye madudu yetu mengine wamekuwa tena wa kwanza na kwa nguvu zaidi kutoa misaada ya chakula.

  Tatizo letu ni nini hasa? Wakati Somalia wanakufa njaa, sisi tulikuwa na mashindano ya kula sana pale Morogoro; wakati Somalia wanakufa njaa sisi tunaendelea na mizunguko ya Fiesta! Ooh sina tatizo na sherehe hizo au watu kufurahia lakini can we be a little bit responsible nation miaka 50 baada ya uhuru wetu? I'll share you a short story, hotuba ya Nyerere.

  Najiuliza; were we in a better position to help our brothers in Kenya and Nyasaland (now Malawi) then than now? Kama matatizo ya uhuru tuliyaona yanatuhusu hivyo, je matatizo ya chakula hayatugusi hivyo? Najiuliza, kuna kiongozi yeyote Tanzania anayeweza kutoa wazo hili na kulisimamia simply kwa ajili ya utu wa mwanadamu? Si kwamba katiba yetu inasema "kila mtu (haisemi kila Mtanzania) anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"?

  Nauliza: Makanisa, na Misikiti yetu wako wapi kutekeleza wito wao wa kusimama na wale wenye njaa na shida? Nauliza, makundi ya vijana ma wanaharakati wetu, wako wapi?

  Kwa upande wangu, I'll do something, the only little thing I know I can do. Siwezi kuangalia macho ya huyo mtoto na kuendelea kula kama kawaida. NI DHAMBI dhidi ya uanadamu wake.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Mosi, hiyo picha inatisha. Ungeweka angalizo kama 'viewer discretion is advised' ingekuwa bomba.

  Pili, niseme nini tena. Unauliza mbona Waafrika hatusimami kusaidia Waafrika wenzetu....hahaaa....ningesema lakini nishasema sana hadi nimechoka.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Mzee, ndio maana nimeweka hiyo picha.. kati ya mtu kushtuka na huyo mtoto kutuangalia nadhani, yeye anatakiwa asione picha za sisi tulioshiba, atashtuka. Wouldn't you agree?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj hujui kwamba sisi ni masikini hahahaha!!!!! sisi ni watu wa kusaidiwa bana si kusaidia afteralll kwani Marekani, Uingereza wamegoma kusaidia hahahahah!!

  Nacheka lakini kwa uchungu, kuna watu wanaweza kuwa wanamshangaa JK kwenye hili wakati hili ni jukumu la kila mmoja kama mwananchi, people can mobilize themselves in small groups wakachangia chochote walicho nacho na kuchannel thru say RED CROSS.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo picha, is it a kid au mzee? It's really shocking! 7 months????? Unaweza fikiri mzee wa miaka 70 akiwa anaishia kwa ngoma!!!!!!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Ni mtoto huyo.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Wanasema a picture worth 1000 words, nashukuru kwasababu nimeliongelea kwa hoja ya 'Je ile kauli mbinu ya matatizo ya Afrika yanahitaji suluhu ya Afrika' inayotumiwa na AU ina maana!

  Tunalaani uvamizi wa nchi za magharibi kwa mapovu midomoni tukitetea Libya, Ivory coast n.k. vema! Je hili la njaa halihitaji AU.

  Sisi ni wanafiki nasema bila kuuma maneno. Kwanini tulumbane kwenye mablog, magazeti ,warsha na semina kuhusu neo-colonialism wakati wakoloni hao hao sasa ndio wapo Somalia wakigawa chakula. Sisi tupo wapi kwenye matatizo kama haya.

  Je ina maana watoto wanaokufa kwa vita ni bora kuliko wanokufa kwa njaa?
  Je miaka 30 bado tunamsubiri Harry Belafonte na akina Lionel Rich waje kuimba ili kusaidia wenzetu.

  Kuna 'moral authority gani kwa mawaziri wa mambo ya nje kama akina Mh Membe kukimbia huku na huko ili kumuokoa Gaddhafi ili hali watu wanakufa Somalia na wao wapo Dodoma.

  Wale wanaowapa Alshaabab silaha wako wapi kuwapa chakula. Wale waliokuwa wanapigania Sudan kusini ijitenge wapo wapi kusaidia Somalia?

  Kwanini hatulalamikii uvamizi wa mgharibi nchini Somalia tunabaki tukilumbana dhidi ya Ghadaffi na Bagbo.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama wiki tatu zilizopita nilikuwa naangalia historia ya utumwa marekani niliguswa sana na namna watumwa walivyokuwa mistreated mfano hawakuruhusiwa kufanya mikutano au kutembea usiku. Watumwa hata wale walionunua uhuru wao waliweza kukamatwa na kuuzwa tena. Kunyang'anya mali ya mtumwa au kuua mtumwa ilikuwa si dhambi wala kosa kisheria. This was in the 17th century, sasa cha ajabu in the 21st century watawala kama Mugabe they are doing the same to their country men just because they have different political beliefs. Weusi kwa weusi, watu wanapotea, wengine kuwa detained hata zaidi ya miezi sita bila kufunguliwa mashtaka, ZANU PF akimuumiza sometimes hata kumuua MDC hakuna kesi wala ufuatiliaji, this is done miaka hii ya 2000.

  Kwa hiyo kama ulivyoongelea kwenye hoja yako sisi kweli ni wanafiki na tunakuwa driven na maslahi binafsi zaidi kuliko ya the entire human race?????
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Once again, guess who is at the top? the most hated nation.. wanasaidia nchi gani? why?
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza katika siku mbili au tatu zijazo, nitafurahi nikiona zile tende zinazogawiwa na watu kwenye TV sasa zinafungashwa kupelekwa Somalia.
  Nitafuahi nikisikia Jumamosi na Jumapili huko makanisani wanachanga pesa kuwasaidia Somalia.

  Kama viongozi wa dini wanasimamia amani ya dunia, basi watueleze amani ni vita peke yake au zaidi ya hapo? Mzazi wa huyo mtoto ana amani gani hapo alipo na huyo mtoto ana amani gani tunayoambiwa tuwape wenzetu.

  AU ina askari wa kulinda amani, amani ipi kwa familia hiyo hapo kwenye picha?
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  kwa kweli hali ni ya kutisha, na inabidi kuchukua hatua za haraka kuwaokoa wenzetu.
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwanakijiji,

  Hivi kweli unategemea sisi kujifunga mikanda tuende kumsaidia jirani aliye na njaa? Ikiwa kulisha watoto ndani na kuhakikisha wana afya bora na mahitaji ya lazima tunaona kana kwamba ni anasa, na ni mkao wa kula umbakishie Baba lile paja kubwa na matonge mengine, Baba ambaye hajui watoto wameamkaje, wamekula nini au wamevaa nini, leo ndio tuone kibanzi kwa jirani?

  Ni aibu kuwa leo hii tunaambiwa na Serikali iko mbioni kutathmini athari za kukosekana umeme! Now wenzetu wanakufa njaa, tuko mguu pande tunatalii dunia mzima kubembeleza watu wachangie bakuli letu ilhali tunauwezo wa kujikimu wenyewe na hiyo misaada inapaswa kwenda Somalia na Djibuti na hata Kenya!

  Ni uroho, ulafi, ubinafsi total selfishness! As huyu msukuma wako would say...MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  yaani!! hayo maneno ya mwisho yamenichoma hadi maini. Yaani tumefikia hapo kweli?
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hii ni AIBU KWA ALSHABAB waliotayari kutawala mafuvu ya vichwa.
  Hii ni AIBU KWA MAJIRANI WA SOMALIA waliotayari kula na kumwaga huku wanafumbia macho hali hii.
  Hii ni AIBU KWA TANZANIA kutokana na historia yake ya ukombozi wa Afrika.
  Hii ni AIBU KWA VIONGOZI WA AFRIKA, bara lenye kila utajiri lakini watoto wa Waafrika wamefikia hali hii.
  Hii ni AIBU KWA ULIMWENGU WOTE kwa sababu 1001.
  HII NI AIBU YANGU MIMI NA WEWE.
  Mwanakijiji, Maxence, Wana JF wote, ninashauri tupitishe bakuli ndani ya JF.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  The question is what do we do?
   
 16. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  MMJJ hongera sana kwa kutujuza juu ya hawa ndugu zetu, wangeweza kuikimbia hiyo njaa lakini watapita wapi ? Visa,PP,rushwa nk.ni vikwazo na vitu vya kuongeza machungu. hata wale ambao wanaweza toroka na kufanikiwa kufika hata mbeya ambako neno 'njaa' maana yake ni kukosekana kwa wali au ugali. AU wangekaa na kutafakari upya namna ya kuhakikisha nchi zenye ahueni ya chakula zifungue mipaka na kuondoa vikwazo ili watu waweze kusafiri au kusafirisha chakula,nafikiri umesikia serikali yetu ikipiga marufuku mahindi kusafirishwa kwenda nje ?????!!!!!!
   
 17. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Tuanze leo mkakati wa kuwafikia hao watoto,ni aibu na nidhambi kuona chakula kinazagaa jikoni kwangu,huku watoto wakifa kwa kukosa hicho ambacho wanangu wanaonja na kukiacha...Something must be done now,through JF we can do something for these innocent kids.
   
 18. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Kwenye masoko yetu ya chakula bado 'supply' ni kubwa kuliko 'demand' lakini bado watawala wetu kwa kuogopa vivuri vyao na ubinafsi wa kiafrika wako radhi kuona inzi wanafaidi vyakula vilivyooza kwa kukosa soko na kuwaumiza wafanyabiashara wetu kuliko vyakula hivyo kupelekwe kwenye mahitaji makubwa na ya kweli ya chakula kama somalia...Inahuzunisha sana
   
 19. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Makanisa yapo bize kupanga na kutekeleza miradi ya kujiongezea kipato. KANISA LA SASA LIMEPOTEZA DIRA HALINA HATA MWELEKEO LILILOACHIWA NA BWANA WETU YESU KRISTO.Kanisa liko bize na miradi huku likisubiri kubatiza watoto na kuzika wafu,ndo injili pekee ambayo kanisa la sasa linaiweza.
   
 20. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Charity begins at home..., Africans can not even help oneself let alone a neighbour
   
Loading...