NJAA KALI : Watumishi wa umma hawakopi tena kwenye mabenki, wamehamia benki za mtaani za chap chap !

Mkuu. Tunaweza kuilaum serikali asubui mpaka jioni na kumwangushia lawama Magufuli na chama cha mapinduzi.

lakini tunasahau kila mtu au mtanzania ana sehemu yake ya kutimiza wajibu wake kabla ya kulalamikia serikali na chama cha mapinduzi.

chama cha mapinduzi au rais haikuwekei hela mfukoni, wala haikuletei chakula mezani. Niwajibu wako wewe kama mtanzania kupambana uishi vizuri na familia yako.

tukibadilisha fikra hizo mgando na kuanza kuchangamka kutafuta fursa mafanikio yataanza kudhiirika kwetu na tutaanza kuacha kuilaumu serikali.

nirudi kwenye mada.
watumishi wa serikali wanaponzwa na matumizi mabaya ya pesa. Wewe kama mshahara wako ni M1 Na unataka uishi maisha ya M5 Kwa mwezi serikali inahusikaje?

hapo tatizo liko kwa watumishi wa serikali wenyewe kushindwa kudhibiti matumizi.

serikali ya awamu hii imejitaidi sana kuwalipa watumishi wake kwa wakati tarehe 20 au 21 tayari pesa imeshaingia kwenye akaunt. Mungu awape nini tena? Tuachekutafuta visingizio tutimize wajibu wetu.
 
Ingelikuwa kuna akili kidogo hazina ndiyo ilipaswa iwakopeshe kwa riba ndogo
 
Hizi chap chap za mtaani ni shida. Kuna jamaa wana kitaasisi chao cha kukopesha walimu na wamewapiga sana hawa ndugu.

Yaani unakopa 100k unarudisha 140k, (40% interest) unawaachia ATM na password.

Kimbembe sasa.
Mama mmoja yeye deni lake haliishi kama la HESLB., Kumbe deni linakatwa officially, badae humohumo wafanyakazi wao wanaenda wanavuta mpunga kwa mara nyingine., mama akienda anakuta Account inasoma 20,000 siku zingne 10,000.

Nafanya utafiti zaidi ntakuja na full details.
 
Mikopo ni jambo jema tu ila inahitaji umakin wa hali ya juu sana na akili ziwepo zote kwakwel vinginevyo utaishia kujuta sana.
 
Nipeni mfano mzuri wa watanzania 10 matajiri kutokana na kilimo
Kilimo chetu hakikuwahi kuwa cha kibiashara toka enzi. Hatuwezi kufanana na Kenya. Tulipoondia settlers 1967, na kilimo cha kibiashara kikafia pale.
Ila haina maana hakiwezekani. Kuna dada kule Iringa anafanya maajabu. Arusha wameanza kuuxa maua. Kwahiyo hata unachofanya kitawezekana kama utadhamiri
 
Wengi wetu tunakopa bila sababu ya Msingi yenye mapana na hatima ya kesho yetu.

Na wenye sababu hawafati taratibu kamili za kuwezesha Pesa kuwainua hivyo inakuwa mzigo kwao.

Pesa tukope ikiiwa tayari tumesha anzisha kile kinacho kufanya tukope.

Unakopa Pesa ukanunue chelehani wakati ufundi hujui, hujui uzoefu wa kudeal na mteja hapo lazima uukalie mpini.

Unakopa ukanunue bodaboda umpe mtoto wa Dada yako ikiwa hana uzoefu wa bodaboda hana Leseni hapo lazima uukalie.

Unaenda kukopa ili ukalime lakini huna Shamba, hujui Ardhi yako inafaa kwa mazao gani? Hujui watu utakao shirikiana nao ni watu wa namna gani hapo lazima uukalie.

Kuna Mzee mmoja nilikuwa nae karibu ghafla akapokea simu iliyo mtoa katika mood,

Baada ya kumaliza maongezi akaanza kunielezea kuwa, kachukua mkopa katafuta shamba Songea, Mtu wa kusimamia ni kaka yake mwenye umri wa miaka 63, Sasa shemeji yake anamlaumu kuwa toka ampe Pesa kaka yake kaongeza Wake watatu, Nyumbani haonekani.

Mzee akamuliza shemeji yake vipi kilimo? Akajibiwa hakuna chochote bora asinge mpa zile pesa na wala asingekuwa anatuma maana zimembadili tabia

Mzee aliumia sana, nilimwonea huruma huyu mfanyakazi wa uma Mtiifu na mwenye Upendo, Ilibidi nipate kazi ya kumbeleza na kutumia uzoefu wangu wa mtaa kumuweka sawa, na hivi ndivyo Pesa za mikopo zinapotea kwa wafanyakazi wa Uma wanabaki wanaishi kama mashetani .
 
Mkuu. Tunaweza kuilaum serikali asubui mpaka jioni na kumwangushia lawama Magufuli na chama cha mapinduzi.

lakini tunasahau kila mtu au mtanzania ana sehemu yake ya kutimiza wajibu wake kabla ya kulalamikia serikali na chama cha mapinduzi.

chama cha mapinduzi au rais haikuwekei hela mfukoni, wala haikuletei chakula mezani. Niwajibu wako wewe kama mtanzania kupambana uishi vizuri na familia yako.

tukibadilisha fikra hizo mgando na kuanza kuchangamka kutafuta fursa mafanikio yataanza kudhiirika kwetu na tutaanza kuacha kuilaumu serikali.

nirudi kwenye mada.
watumishi wa serikali wanaponzwa na matumizi mabaya ya pesa. Wewe kama mshahara wako ni M1 Na unataka uishi maisha ya M5 Kwa mwezi serikali inahusikaje?

hapo tatizo liko kwa watumishi wa serikali wenyewe kushindwa kudhibiti matumizi.

serikali ya awamu hii imejitaidi sana kuwalipa watumishi wake kwa wakati tarehe 20 au 21 tayari pesa imeshaingia kwenye akaunt. Mungu awape nini tena? Tuachekutafuta visingizio tutimize wajibu wetu.
Ni kweli kuwa serikali na chama havileti pesa wala chakula mezani. Lakini sera zao ni muhimu kuweka mwongozo wa jinsi maisha yatakavyokuwa.
Pili kutoa mshahara tar 21 haipunguzi siku za kupokea kwani ukipata mshahara tar 21 ya mwezi Match kisha ukapata mshahara tar 21 ya mwezi April ni mwezi mmoja net hakuna upungufu wa siku hapo
Usilete hoja ya tar 21 kila mwezi ukajua ni upendeleo ni siku30 zile zile ambazo ni mwezi. Hata kama mshahara ungekuwa unatolewa kila tar 10 ya kila mwezi bado ni vile vile hapatakuwa na upungufu wa siku kati ya mshahara mmoja na mwingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom