Njaa inanukia, mvua zimegoma. Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi

Habari za mida..

Kuna dalili za njaa mwaka ujao kutokana na Hali ya ukame inayoendelea Nchini kwa sasa.

Sio jambo la kawaida kwa mwezi huu wa disemba mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokuwa na mvua.Sehemu nilipo wananchi bado hawajaotesha Mazao kwa sababu mvua hazipo.

Hali ya hewa ni jua,joto,upepo na manyunyu tuu huku nzi wakitamalaki.

Chonde chonde Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi maana hivi tunavyoongea bei za Mazao zimeanza kupanda.Hata wale wa mahindi waliokuwa wanalia saizi wanauza kwa bei ya Kati ya 45,000-55,000 kwa gunia huku mikoani.

Ili kunusuru chakula kilichopo,nashauri serikali ipige marufuku exports ya Mazao yote ya chakula.

Kama Hali hii itaendelea ,Wananchi tujiandae kisaikolojia.Ukame umeeneo si tu Tanzania bali Hali ni mbaya zaidi Ethiopia,Kenya na Somalia.

Watu wa Hali ya hewa walitabiri hali hii toka mwezi wa tatu,wakarudia mwezi Juni na mwezi November.
Acha Mambo yako, kama unaona kitapanda Bei nunua Sasa weka store ama kalime chakula chako wewe. Wakati mkulima analima ulimchangia Chochote?
Songea bado mahindi Bei chini 300 - 350 kwa kilo, hakuna faida hapo. Madibira bado mpunga ni mwingi Sana acha uchawi wako.
Mind your own business
 
Mleta mada tumia vizuri kichwa na siyo kubebea masikio peke yake, inaonekana hujawahi kulima hujui adha zinazowakumba wakulima
 
Wazo ni zuri sana, bei za Mahindi zimepanda hadi kufikia sh.10,000/12,000 kwa debe kutoka sh.4500/5000.
 
Habari za mida..

Kuna dalili za njaa mwaka ujao kutokana na Hali ya ukame inayoendelea Nchini kwa sasa.

Sio jambo la kawaida kwa mwezi huu wa disemba mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokuwa na mvua.Sehemu nilipo wananchi bado hawajaotesha Mazao kwa sababu mvua hazipo.

Hali ya hewa ni jua,joto,upepo na manyunyu tuu huku nzi wakitamalaki.

Chonde chonde Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi maana hivi tunavyoongea bei za Mazao zimeanza kupanda.Hata wale wa mahindi waliokuwa wanalia saizi wanauza kwa bei ya Kati ya 45,000-55,000 kwa gunia huku mikoani.

Ili kunusuru chakula kilichopo,nashauri serikali ipige marufuku exports ya Mazao yote ya chakula.

Kama Hali hii itaendelea ,Wananchi tujiandae kisaikolojia.Ukame umeeneo si tu Tanzania bali Hali ni mbaya zaidi Ethiopia,Kenya na Somalia.

Watu wa Hali ya hewa walitabiri hali hii toka mwezi wa tatu,wakarudia mwezi Juni na mwezi November.
UMEKOSEA SANA KUSEMA SERIKALI IPIGE MARUFUKU KUUZA MAZAO YA CHAKULA NJE YA NCHI KUMBUKA UNAZUNGUMZIA MAZAO YA WAKULIMA SIYO YA SERIKALI UJUE HUO NI UKANDAMIZAJI WA WAKULIMA KUINGILIA UHURU WA MAZAO YA BIASHARA YAO
 
Wa kwanza kupata njaa ni hao hao unaowaita wakulima.Bora wabaki na chakula kuliko kukosa vyote.
 
Wewe mtoa mada bure kabisa, yaani unataka mkulima asifaidike na kazi yake ya shambani? Serikali inatakiwa inunue mazao kwa mkulima kwa bei ya soko ili wakati wa njaa iwalishe watu kama wewe. Usilete mawazo ya kijamaa
 
wazo la mtoa mada ni nzuri kwa mtu ambaye anafakiria kwa mapana na marefu kuhusu usalama wa nchi na watu wake kwa kipindi kijacho iwapo hali iliyopo itakuwa hivi.Nimetoka wiki iliyopita toka Tundu
 
Back
Top Bottom