Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Mbaya zaidi hii mbinu yao ya kiprimitive badala ya kuondoa tatizo la njaa inaleta njaa.Acheni njia primitive za kupambana na matatizo.
Kumzuia mkulima kuuza mazao yake mahali popote anapoona panampa manufaa eti kwa sababu kuna dalili ya njaa, ni njia primitive za kupambana na tatizo la njaa.
Kuna wakati kumewahi kuwa na upungufu mkubwa wa cement nchini, umewahi kusikia serikali ikipiga marufuku viwanda kuuza cement nje ya Tanzania? Kwa nini iwe tofauti kwa mkulima?
Kama Serikali itakuwa imeona kuna dalili ya uwepo wa njaa, ikanunue mazao toka kwa wakulima, ikashindane na wanunuzi wengine, ikayatunze mazao hayo kwenye maghali yake, na siyo vinginevyo.
Halafu, siyo kweli kuwa siyo kawaida kutokuwepo mvua kipindi hiki huko Nyanda za Juu. Labda umezaliwa miaka ya karibuni, na hivyo hujawa na uzoevu wa kutosha wa hali ya hewa ya maeneo ya huko.
Ni mara nyingi tu, maeneo ya Nyanda za Juu kukosa mvua kipindi hiki. Na ukizungumza na wakulima wa huko, hata miaka ya nyuma, utawasikia, 'mwaka huu mvua zimechelewa lakini Christmas lazima zitanyesha, na ikiwa hivyo kutakuwa na mazao mengi mwaka huu'.
Kwa uzoefu wangu, maeneo ya Nyanda za Juu, kukiwa na upungufu wa mvua, huwa wanapata mavuno mengi na mazuri zaidi. Tatizo la Nyanda za juu, mara nyingi ni mazao yao kama mahindi kuoza kutokana na mvua kunyesha kipindi kirefu, maharage kuungua kutokana na mvua kuzidi. Nyanda za juu, kwa wastani mahindi hukomaa ndani ya miezi 3. Hivyo mavuno mazuri ni ya mazao yanayopandwa mwezi Januari au mwishoni kabisa mwa December, ambayo hukomaa mwezi March, na hukauka mwezi April mpaka May. Hata kama mvua zikiwahi, ukipanda mwezi December, mazao hayo huharibiwa na mvua maana yataanza kukauka kipindi ambacho mvua bado zinanyesha.
Kama tutafika mwezi Januari 2022 bila ya mvua, hapo kweli Nyanda za juu wataanza kuwa na hofu ya kupata mavuno mazuri. Sasa hivi tatizo kubwa la mikoa hiyo ni bei ya mbolea, mfuko mmoja umefika shilingi 120,000. Huwezi kununua mbolea kwa bei hiyo, ukaitumie kwenye kilimo cha mahindi, upate faida. Sasa hivi nimeambiwa wakulima wameanza kutafuta mbegu zao za asili ili wasitumie mbolea, maana za kisasa haziwezi kumudu bila mbolea. Kitakachotokea ni mavuno kidogo