Njaa haipo facebook,Instagram, Twitter wala jamii forum bali njaa ipo kwa masikini wanaoshi vijijini

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
881
1,033
Jamii nzima kwa hivi sasa imekuwa ikipaza sauti juu ya njaa kwa kulaumu serikali kwa kutowajibika na kushughulikia janga hilo.

Najua sehemu kubwa inayopaza sauti sio waathirika wa njaa bali uhaba wa mvua ndio kimekuwa kichocheo kikubwa na kuwa mtaji wa kisiasa kwa baadhi ya wanasiasa. Na inasikitisha kuona njaa kuathiri mitandao ya kijamii kuliko jamii yenyewe, walalamikaji wengi wa njaa ni wamiliki wa smartphone. Watanzania tuwe na huruma Si dhani kama kuna mwajamii forum ambae ni hai ameathirika na njaa.

Ni wakati sasa jamii hii inayopaza sauti kuhusu njaa, ipaze sauti katika jamii inayotuzunguka maana sehemu kubwa iliyoathiriwa na njaa ni katika familia masikini, familia ambazo hazina namna yoyote ya kujingizia kipato zaidi ya kutegemea ardhi, mifugo na mvua.

Kinachokosekana katika jamii hizi ni elimu itayokayomsaidia kupambana na mazingira yake yanayozumnguka ili kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza

Jamii hii imekuwa ikiishi maisha ambayo babu zetu waliishi ya kuhama kuhama .

Kutokana mabadiliko ya hali ya hewa kwa hivi sasa na ongezeko kubwa sana la watu tofauti na ilivyokuwa hapo zamani uliweza kuhamia popote pale bila kuulizwa kwa kufuata chakula au maji bila ya kuwa na manuniko katika serikali kama ilivyo sasa ambayo inachangiwa na ukuaji wa technologia

Mfano msukuma angeweza kuhama na mifugo yake mpaka morogoro tena kwa kuchunga tu tofauti na hivi sasa kila mtu kazungushia wigo kaeneo kake kutokana na ongezeko la watu.

Bila kuingiza siasa ni wakati serikali kuzibiti ongezo la watu hasa vijijini sababu unakuta mtu ana watoto 40 na wake wanne wakati huo mtu huyo hana njia yoyote ya kujiingizia kipato zaidi ya kutegemea kilimo cha kutegemea mvua, akate miti achome mkaa na kadharika.....kwa mjini mtu anaishi kwa heshima unamiliki familia kulingana na kipato chako hukurupuki kuzaa ovyo ovyo

Ni wakati sasa serikali kuangalia namna kusaidia jamii hasa ambazo ni masikini vijijini kwa kuwapa elimu itanayoendana na mazingira ya hivi sasa.........ni wakati wa kueneza elimu na sio siasa katika na kufanya jamii kudamaa akili ikitegemea misaada kutoka serikali
 
Hata humu JF watu tumrathirika na njaa.Kama Kilo 1 ya unga ilikuwa ikiuzwa 1,000/- saivi inauzwa 1,600/- unaweza kusemaje wanaJF hatujaathirika.Kama tuna ndugu zetu ,wazazi wetu huko vijijini wanategemea kilimo cha mvua wameathirika unawezaje kusema wanaJF hatujaathirika?? Kwa kuathirika ndugu zetu huko maana yeke sisi tunaotegemewa tuongeze msaada mara dufu ili kuokoa jahazi.

Serikali ni lazima ilaumiwe kwa kuwa inashindwa kutambua vipaumbele vya msingi.Pesa waliyonunulia ndege hizo mbili zingetumika kutengeneza irrigation schemes maelfu ya watanzania wangeweza kuzalisha kwa manufaa ya mamilioni ya watanzania.
 
Hao wazazi wako umewapa elimu gani......itayoweza msaidia kuondokana na njaa

Serikali ni pamoja ww kama unavyoshindwa kufanikisha mipango yako ndiyo hivyo serikali inavyoshindwa pia lazima tuihulimue serikali maana ina kazi kubwa katika nchi kusomesha wanafunzi bure sio kitu kidogo
 
Back
Top Bottom