Niyawazayo kuhusu uteuzi wa Chief Scout wa Simba

Hichilema

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
1,018
912
Nawasalimu.
Wiki hii Klabu ya Simba imemteua Mholanzi, Melis Daadler kuwa msaka vipaji mkuu(chief scout )wa Klabu.

NIna mtazamo tofauti na watanzania walio wengi wanaodhani kaja kusajili wachezaji dirisha hili ili simba abebe ubingwa msimu huu.

Lengo la timu ni la muda wa kati na mrefu. Wengi wanajiuliza Mzungu na kuscout wachezaji Tanzania wapi na wapi?

Taarifa ikufikie kuwa Daadler anaijua sana bongo na Afrika na ameshatembelea maeneo mengi ya Tanzania na kaoa Mtanzania.

Lengo kuu la Simba ni kumtumia Daadler kunasa vipaji vya vijana wadogo watakaoisaidia Simba hapo baadae.

Kuna uwezekano mkubwa Daadler kuonekana mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA yatakayoanza hivi karibuni. Najaribu kuhusianisha mkataba wa milioni 500 kwa ajili ya timu za vijana za Simba na ujio wa Daadler.

Jambo jingine ninaloliona kwa SSC ni kumfanya kocha kuwa manager wa timu maana yake ni kwamba huyu chief scout atakuwa na watu wa chini yake ila wote watakuwa chini ya kocha mkuu ambaye sasa atakuwa manager.

Jambo la tatu, huyu scout atatumika kwenda kwenye viwanja vya timu pinzani kuwasoma wapintani na kupeleka ripoti kwa kocha.

NB: Soka letu linapiga hatua. Tegemea timu nyingine kuiga kitu hiki. Tegemea huyu jamaa kuwa maarufu sana
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom