Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,519
Mimi kila siku huwa nauliza hao wahisani nani aliwapaga msaada wakaendelea? Sasa unapokuwa na watu ktk nchi/serikali kama huyu katibu mkuu Lyimo anayesema "Hawa mabwana wana masharti magumu sana, ndiyo maana tunashindwa kuyafikia maendeleo… hii inasababisha nchi yetu kuendeshwa na wafadhili badala ya kujiendesha wenyewe," ...halafu wazungu wakisema sisi hatuna akili wala uwezo wa kujitawala tunakuja juu wakati ukweli wa mambo uko bayana kabisa. Hivi bila ya hawa wahisani, ni nini kitatokea? Ina maana hatuwezi ku-exist?