Niwaonavyo wagombea watatu wa urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niwaonavyo wagombea watatu wa urais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ami, Oct 16, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa.
  Mimi binafsi kwa nafasi hii namuamini zaidi Ibrahim Haruna Lipumba.Namuona ana elimu ya mambo ya kiuchumi ambalo ndilo tatizo sugu la watanzania.Ana uchangamfu wa kiuraisi na huzungumza kwa hekima.Wale wanaompinga si kutokana na kukosa sifa bali zaidi ni kutokana na chuki zao za kidini.
  Pamoja na hivyo ikiwa umesalia muda mfupi kabla ya uchaguzi wenyewe,mpambano unaonekana upo zaidi kati ya Slaa na Kikwete.
  Waislamu kwa kiwango kikubwa wanaonekana kumuunga mkono Kikwete,si kwamba wanamuona bora bali ili kumpinga Slaa ambaye wametoa takwimu nyingi kuonesha hisia zao dhidi yake.
  Mbali na kuwa ana historia ya kupinga ajenda za waislamu bali anaonekana ni mtu muovu wa tabia hasa kutokana na kosa la kumnadi mke wa mtu kuwa ni mchumba wake.Wanahisi pindi akishika uraisi atakuwa ni mtu wa nuhsi moja baada ya nyengine.
  Hisia hizo unaweza kuzipata wazi wazi kupitia redio kadhaa za kiislamu na magazeti yao hasa An-nuur na ALhuda.
  Kutokana na kupigwa pande na kundi kubwa la wapiga kura na kampeni za kawaida za CCM, ni dhahiri kuwa dkt.Slaa hatoweza kupita katika uchaguzi huu hata.
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Teh tehh teh bora 31.10 ije tumalize mambo tu.:mmph:
   
 3. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...presha inapanda, inashuka...
   
 4. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Avatar yako tu dah mi hoi haki ya nani
   
 5. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii ya kwako ndio hoi zaidi kwangu!.
   
 6. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwa Avatar yako wewe hata kunigusa hutakiwi ni haramu kabisa
   
 7. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ikiwa hata kuguswa hufai,basi tuachie tujadiliane wenyewe na wewe kakae na wenzako mubwekeane.
   
 8. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hivi hata kama nakuona unasinzia karibu na shimo siruhusiwi kukubwekea bandugu?
   
 9. M

  Mikomangwa Senior Member

  #9
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ami hayo ni mawazo yako hupaswi kulaumiwa lakini tafakari yafuatayo: Prof. Lipumba anaangushwa sana na wafuasi wake wanapokuwa wakijitambulisha kwa udini. Anapohutubia utadhani ni swala ya Ijumaa kwa jinsi wafuasi wake wanavyoonekana. Pia nyaraka zinazoandikwa kuwahimiza wapiga kura wa dini yake zinazidi kuweka kando baadhi ya wapiga kura wa dini zingine. JK ametekwa na wenye pesa. Huwezi kusema anaangushwa na wasaidizi wake wakati wananchi tumemkabidhi rungu la kuwashughulikia anashindwa. Ni kiongozi dhaifu na kwa viwango vya Mwalimu Nyerere angetukanwa kuliko hata Mwinyi. Anapendeza kuwa ceremonial leader na siyo executive leader. Dr Slaa anawapiku kwa sababu ameonyesha uthubutu wake wa kutetea maslahi ya taifa bila woga. Ameonekana kutambua watanzania maskini wanahitaji nini nao wanamuunga mkono bila kujali udhaifu wake binafsi. Remember Bill Clinton's saga? Tafakari.
   
 10. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ningekuwa nakufahamu wewe Ami wewe, ningekufata popote pale ulipo nikakuwasha vibao ili akili yako iamke maana naona bado uko kwenye usingizi mzito. Usipayuke payuke kuhusu mambo usiyo yafahamu, nitakuita chai jaba. HATUDANGANYIKI
   
 11. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama umechoka bora ukalale. Utumwa wa namna hii ni fedheha. Unaweza ukauza hata baadhi ya viungo vyako ili mradi upate mlo kama wafanyavyo baadhi ya dada zetu.

  Nakushauri uachane na fedheha ya utumwa wa namna hii.
   
 12. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inshallah tutashukura ukimpigia Dr. Slaa
   
 13. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkomwanga achana na utetezi wako wa Dkt Slaa kwa kutaja visa vya Bill Clinton na Jacob Zuma.Watanzania tulio wengi utamaduni wetu ni tofauti na wa kwao.
  Kipi kimekujulisha sifa hizo za Slaa,ilhali hali ndani ya chama chake inamshinda.
   
 14. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  crap!:tsk::tsk::tsk:
   
 15. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mtoka mbali makeke yako ndio sifa za chama chako.Hamtufai.Tukiwapa nchi tutakuwa tukichapana chapana bila mwisho.
   
 16. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mie niko kwenye tourism industry na sifa moja ambayo hufahamika kwa kila mgeni anayekuja hapa nchini ni ustaarabu wa watz. Kama ustaarabu ni nature yetu sitegemei kwamba sisi wastaarabu tutaanza kuchapana chapana bila sababu. Chadema ni chama cha watu waaminifu na waadirifu.
  Chagua CHADEMA chagua Dr. Slaa.
   
 17. M

  Mikomangwa Senior Member

  #17
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ami bahati mbaya hupendi kujenga na kujibu hoja. KInachowaangusha Lipumba na Kikwete umeviona? Slaa atatinga ikulu kama hamtaki kukosolewa na kufanyia kazi changamoto mnazopewa. Kikwete anafaa kufungua matamasha, kuweka mawe ya msingi, kuzima mwenge, taja inaugurations zozote. Hawezi kumaintain discipline ndani ya serikali yake. How can he summon Lowasa, Chenge, Mramba, Rostam, Manji, Dewji, ...? But Slaa can. You remember the list of shame? God Bless this Nyerere's REPLICA!
   
 18. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Haya ukimaliza ukalaleeee,mtoto mzuri.
   
 19. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  siwezi kupoteza muda wangu kumjibu au kumshauri Ami. kufanya hivyo ni sawa na kumkimbiza kichaa aliekuibia taulo wakati unaoga.mwisho wa siku watu hawataona tofauti kati yako na kichaa
   
 20. M

  MjengaHoja Member

  #20
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru ndugu yangu lakini mie naona JK badi anastahili hiyo nafasi ya Urais,Lipumba sawa ni msomi mzuri lakin katika usomi wake huo umekua hauna manufaa kwa Taifa letu,niulize kwa nini??Alishawahi kuwa mshauri wa Mstaafu Rais alhaji Ali Hassan Mwinyi lakin alishindwa kulipelekea Taifa hili kuyumba kiuchumi na akaondolewa,si hayo tu pia alichukuliwa kuwa mshauri wa Rais Y.MUSEVEN Kama mshauri wake lakini pia huko jitihada zake hazikufikia kiwango akarudi nchini....Hivyo basi mi naona JK bado anatufaa sana
   
Loading...