Niwaombe wabunge na madiwani mnaohama vyama katikati ya safari fanyeni hivyo baada ya vipindi vyenu vya miaka mitano kuisha, mnaumiza wananchi sana

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,361
5,808
Kifupi kwa kuhama katikati ya ubunge wenu au udiwani mnawaumiza sana wananchi nadhani muwe mnasubiri kwanza kipindi cha uwakilishi kwa vyama vyenu mlicho pewa na wananchi kikisha pita ndio muhame au mstaafu

Mnaumiza sana wananchi wenu muwe na huruma ya ndani ya nafsi zenu , ni kwa sababu tu hamuwapi nafasi wananchi wenu kuyaongelea maumivu yao kwa haki na jinsi wanavyo jisikia lakini mnawaumiza sana kimwili na kiroho.

Wengine ubunge au udiwani mliupata kwa damu za wananchi hao hao kumwagika ili kuipigania haki yako na uliwahimiza kabisa wana pigwa na dola wakaumizwa na wengine wanapata vilema vya kudumu na wengine kupoteza maisha halafu baada ya muda unaachana nao kirahisi tu na wale walio mwaga damu kwa ajili yako na kuwatelekeza kabisa muwe na huruma ya ndani tena huruma ya asili ya kibinadamu na nafsi ziwasute na kuwauma kabisa mnawatesa na kuwaumiza sana wananchi wenu walio umizwa na kujeruhiwa kwa ajili ya kukutafutia haki wakati ulipa taka kudhurumiwa haki yako

Mnawaumiza sana wananchi wenu wanaumia sana ila tu hawapati nafasi ya kutoa na kuelezea maumivu yao ila wananumia sana sana na wanakosa kabisa morali ya kupiga tena kura mnawaumiza sana nyie watu na hali hiyo haitawaacha na mwisho mzuri kwasababu wengi wenu uhamisho wenu si wa kujali walio kupandisha kabla.
 
Back
Top Bottom