Niupate wapi moyo wa Kikwete nisiugue presha?

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
647
500
*NIUPATE WAPI MOYO WA JAKAYA NISIUGUE PRESHA?*

Hatimaye Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa anakwenda kukabidhi hadhi na Madaraka ya juu kabisa ya Chama kwa Rais wa sasa John Joseph Magufuli kama ulivyo utaratibu wa CCM.
Sina mashaka na utaratibu huu maana ni utaratibu wa kawaida kwa Chama kikongwe kama CCM na hii sio agenda yangu kwa leo.

Agenda yangu mimi ni aina ya Mtu anaekwenda kukabidhi madaraka hayo! *Jakaya Mrisho Kikwete.*
Haliwezi kuwa jambo jepesi kuamini kwamba Jakaya Kikwete anakwenda kukikabidhi Chama, kwamba hatakua tena Mwenyekiti wa Chama kama nilivyozoea kumwandika ktk Makala zangu. Yaani baada ya tarehe 23.06.2016, Jakaya anakwenda kujiunga na Mzee Mkapa Benjamin pamoja na Mzee Mwinyi Alhassan, Karume Aman na wengine ktk Balaza la wazee. Hawa ndio wazee washauli wa Chama cha Mapinduzi.

Kwamba baada ya Mkutano Mkuu wa Tarehe 23. 07.2016, Jakaya hatafungua na kufunga Mkutano wowote wa CCM Taifa. Si ajabu kwa utaratibu wa Chama kuwa hata Mkutano huo wa Tarehe 23.07.2016 Jakaya hataufunga baada ya kuufungua maana kutakuwa kumepatikana Mwenyekiti Mpya.
Inahitaji moyo wa ganzi kuamini kwamba Jakaya amestaafu Uenyekiti wa CCM. Kwangu mimi Jakaya huyu ni mtu wa kukumbukwa sana.
Kama yuko mtu ndani ya CCM atakayekumbukwa kwa mengi mema kwa Chama cha Mapinduzi, basi ni Jakaya Mrisho Kikwete!
Kumkumbuka Jakaya sio hiari!
Ilimradi tu uwe ulitimiza miaka kumi na nane wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2015.
Basi utake usitake wewe utamkumbuka Jakaya.
Haijalishi ni kwa namna gani,kumbukumbu ni kumbukumbu tu!
Niupate wapi Moyo wa Jakaya nisiugue Presha?

Tarehe 11.07.2015,Jakaya alifanya kile ambacho watu wengi hawakutarajia. Na hiki ndicho kitamfanya akumbukwe na watu wengi, mimi na wengine wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume.
Ni Jakaya Kikwete ndiye aliongoza Kikao kilichokata jina la Edward Ngoyai Lowassa kutoka ktk majina yaliyotakiwa kuwania Urais wa Tanzania.
Kulikata jina la Lowassa haikuwa kazi nyepesi kwa namna yoyote ile.
Licha ya ugumu huo bado haikuaminika kwamba ingewezekana ndani ya Chama cha Mapinduzi kutokea mtu jasiri mwenye uwezo wa kuliondoa jina la Lowassa katika kinyang'anyiro kile. Lowassa alikua amemaliza formula zote za ku win Urais.
Matambo ya Lowassa yalitosha kabisa kubomoa ujasiri wa kila aliyedhani kwamba anaweza kumuondoa!
Lowassa alikua Mungu mtu ndani na nje ya CCM.
*Niupate wapi Moyo wa Jakaya nisiugue Presha?*

Kwa mara ya kwanza kulitokea Mafuriko ya watu ktk Nchi hii. Haikuwahi kuonekana kwa macho mafuriko ya watu namna ile. Lowassa alizichanga karata zake vizuri zikawa za ushindi. Tulilia na kushinda njaa tukiomba atokee mtu jasiri atakaeweza kufunga spidi zile za Mamvi.
Wakati huo wengi tulitakiwa kumpenda Lowassa ama kuchagua kula limao! Hivi ndivo Askofu wa Mungu Gwajima alitushauli.
Tuliokula limao tulikula hadi tukakinaiwa!
Lowassa bado alichanja Mbuga.

Wakati wote huu Jakaya alikua na siri yake moyoni. Moyo wake ulikua kama kuzimu isiofikirika, ulijaa siri kubwa na ya hatari. *Siri ya kumkata Lowassa!*
Pamoja na Siri kubwa na ya hatari kama ile,bado Jakaya hakuwahi kuugua Presha. Aliendelea kutabasamu kila wakati hata pale alipokutana na jinamizi Lowassa ana kwa ana.
Hilo lilipotokea Jakaya alijiwazia kimya kimya kwamba *"Lowassa alipaswa kukatwa mara moja!"*
Lowassa ni lazima akatwe, JK alijisemea moyoni!
Ilipofika July 11, Nuru ikazima ghafla, giza likafunika anga, ndoto za Ikulu zikayeyuka kama Siagi juani. Mafuriko yakazuiliwa kwa Mikono,hatimaye Edward Lowassa akakatwa!✂✂
*Bravo JK!*
Niupate wapi Moyo wa Jakaya nisiugue Presha?

Naam!
Tarehe 23.07.2016, Jakaya atauacha Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa. Hadaiwi lolote ndani ya Chama kwa sasa.
Amemaliza kila kitu!
Kazi kubwa aliotakiwa kuifanya ameifanya sawasawa!
Kazi ya kumkata Lowassa ndio pekee alidaiwa kuifanya kwa wakati wote huo! Lowassa alitakiwa kukatwa tangu mwaka 2010. Aliponapona baada ya mpango wake wa kukivunja chama kukwama!
Lowassa has go to hell!
Jakaya amaeifanya kazi hio kwa ubora wa kutosha.
Niupate wapi moyo wa Jakaya nisiugue presha!
Ni wengi hatutakusahau Jakaya. Wewe ndie mtu pekee utakaesalia kwenye Ubongo wa Edward hadi itakapofika safari yake ya mwisho maana umemfanya Ikulu aendelee kuisikia ktk vyombo vya habari.

Tutakukumbuka sana Jakaya,kwa mengi utakumbukwa!
Kila mtenda mema hulipwa wema, umetenda mengi mema katika Chama chako na hivo hivo utalipwa sawasawa na matendo yako . Unazo kila sababu za kujipumzikia kwa sasa huko kwako Musoga.
Chama umekiacha katika mikono salama ya John Joseph Magufuli na kwa sababu hiyo tunakuahidi kuzifuata nyendo zako!
Tutawakata tu!
Kwa haya machache nimejitahidi sana kusema kila lililo jema kutoka kwako. Hivi ndivo nitakavyofanya katika wakati wote uliosalia wa maisha yangu!
Ninachoomba kukipata kwako sasa ni aina ya Moyo wako, natamani kuwakata akina Lowassa waliosalia ndani ya Chama.
Niupate wapi Moyo wa Jakaya nisiugue Presha!

*Wako ktk maumivu ya kwaheri,*
*Menuka Jr.*
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,767
2,000
Kwa msukosuko ule...toka kura za maruhani....na sekeseke lile...nani kama J.!! Bila subira na uvumilivu...angetimua mbio kabla ya 23/07.
 

Chosen generation

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
4,379
2,000
Acha KUJIPENDEKEZA wewe!

Na Lowasa hayuko CCM tena ... Acheni kumhusisha na chama chenu.

Nendeni mkafanye USANII wenu tarehe 23, msitupigie kelele.
 

rais wako

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
604
1,000
Hakuna jipya Sasa cha ajabu nn kwan yeye ndo mwenyekiti wa kwanza kukabidhi madaraka hayo mbona benja alikabidhi
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,635
2,000
Hata Mimi naungana nawe kumpongeza kwa dhati Mh JK kwa ujasiri wa kulikata fisadi kuu kabisa na hatimaye likakimbia na kwenda kwenye chama cha mafisadi Chadema!

Hakika utakumbukwa Mh JK.
 

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,487
2,000
Lowasa anabahati mbaya 2020 Mbowe atamkata tu, hakuna namna, kama Dr Slaa aligeuziwa gia angani, Babu EL kuwa makini utahama CDM sijui kuelekea wapi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom