Niunganisheni na yule Mtanzania aliyefungua Mgahawa Sweden nikaoshe Vyombo. nina Diploma ya Catering

Mkuu umesema unauzoefu wa miaka minne? Naona ni uzoefu mkubwa sasa inakuaje usipate kazi...au unamatatizo yako nawewe maana it seems tayari ulishafanyaga kazi somewhere japo hujaweka wazi. Anyway jaribu kutafuta kazi hata zisizoendana na ulichosomea...hilo ndio hata mimi liliniokoa
Mkuu kwakweli sina tatizo zaidi ya kukoswa kazi. Uzoefu huo mwaka mmoja nilifanya Ilboru Safari Lodge na miaka 3 nimefanya Malaika pale Mwanza...ni kwamba ni ajira tu ndo zimekuwa ngumu mkuu...
 
hahaaaa mie kichwa changu ni hapo kimegota.

yupo Sweden au alikuwepo akarudi?

KM una kibali cha kuishi humo fungua mgahawa wako mweyewe mkuu,

Nchi nyingi za ulaya huhitaji capital kuanzisha biashara yako,kuna scheme nyingi zinazotoa grants ama loans.
Dah ndugu Sweden nimeenda lini? mie nilisoma habari za Mtanzania aliyefungua Mgahawa Sweden...so nimeona hiyo ni fursa kam tu nitawasiliana nae na kumweleza CV yangu mdogo wake niliyepo Tanzania. niko Mwanza
 
Nooo mimi ni msukuma wa Mwanza aisee

Mwangalukaa,lol,kwa nini unataka kwenda kuosha vyombo nje,anzisha biashara ya kuosha vyombo bongo,lol,kweli vile,ukipata wale wanaotoa catering services utatengeneza pesa mkuu,inawezekana isiwe much ila ya kula hukosi lol,mie mpaka june 2017,nitakua nimeanzisha biashara ya mama ntilie :):):)
 
kwa tunayoyajua maisha ya hapa mjini yaani huwa inafika kipindi unakoswa hata pesa ya kula kila ukienda kuomba kibarua nafasi zimejaa lazima nakuhakikishia utahama road.Jamaa etu hajakta tamaa bado anahitaji kusonga mbele naweza kuamini bado anahitaji kupambana zaidi ili apate ridhiki yake stahiki hivyo basi kwa anaye mjua jamaa mwenye hotel sweden amuunganishe naye japo cjui kama anataka kazi nje ya nchi tu humu jf wapo watu wanamahoteli makubwa tu pengne wangekushika mkono tu ukakomaa hapa kwa JPM.
Mkuu nimeapply sana hapa Mwanza na hadi mikoa mingine...sasa katika kufikirisha ubongo zaidi ndio nikakumbuka kuna Mtanzania mwenzangu ni Chief huko Sweden...anaweza nisaidia
 
Wakuu,

Mimi ni msomi wa ngazi ya Diploma; Hotel Management & Catering na nina uzoefu wa miaka 4. Naombeni kwa yeyote anayemfahamu au mwenye mawasiliano na yule Mtanzania mwenzangu aliye fungua Mgahawa/Restaurant nchini Sweden niende nikawe hata Muosha vyombo maana nimehangaika sana sipati kazi japo nina sifa zote za kuajiriwa.

Nimekuwa nakula kwa kuunga unga kwa rafiki yangu ambaye ni mpishi wa Hoteli flani, ananiibia chakula na kunipitishia nyumbani. Hali imekuwa ngumu nikauza simu ambapo hela imeishia kwenye kutoa copy za Vyeti na Nauli za kuwasilishia maombi ya kazi bila mafanikio. Imebidi nije Internet cafe niwaandikieni, kama unamfahamu yule Mtanzania basi niunganishe nae. Nina ile Passport ndogo lakini ntajitahidi nipate kubwa lakini sina hata elfu 5 ya kunilinda linda aisee.

Najitahidi kuwa positive na kujikaza lakini kuna wakati nalia maana kila ninaemwelezea ananiambia kila mtu ana hali mbaya. Sasa leo nikapata wazo kwamba yule mtanzania wa Sweden anaweza kunisaidia. Please niPM...Niunganisheni nae jamani.
Isakesu@gmail.com
 
Bro kwanza pole sana, Hizi ni changa moto za maisha ila ningekupa kidogo ushauri angalau ukusukume kidogo..
Usitake kaz ulio somea maana utaangaika sana kupata hyo kaz jaribu kutafuta kaz yoyote ambayo itakuwa inakuingizia kipato, pili hyo diploma yako ya hotel management and catering unaweza jikusanya watu kama watano mkatengeneza ka group mkaanzisha catering service kwaajili ya maharusi,ubariko,sendoff na events nyingine hyo ni fursa tosha ya kujikimu. ukizingatia hayo utafanikiwa bro, Maisha sio kutafuta mbali na Tanzania. Huku ughaibuni wenzetu maisha ni very Expensive sasa ukija huku unazani maisha yako ndio yatakuwa rahisi, la hasha pambana ukisha kuwa na kipato kikubwa sasa fikiria kuja kwenye nchi za wenzetu.. ila siku katishi Tamaa bro Chamsingi Angalia whats Your minds tells you do,??
Mkuu, naelewa kabisa swala zima la kujiajiri...tatizo mtaji baba...
 
Chef Issa Kapande,Namfahamu vizuri.Tulifanya wote serena hotel wakati ikiitwa Royal Palm..mwaka 2005.

Pia tulikutana Tarangire Sopa Lodge akiwa chef Mkuu.

Hatujawasiliana kwa miaka 2 sasa nitatumia email tulokua tunawasiliana kama bado ipo active then nitakupatia akisha jibu
Ntashukuru sana mkuu...yaani ntashukuru sana. Plz jitahidi and make it fast. I'm starving.
 
Mwangalukaa,lol,kwa nini unataka kwenda kuosha vyombo nje,anzisha biashara ya kuosha vyombo bongo,lol,kweli vile,ukipata wale wanaotoa catering services utatengeneza pesa mkuu,inawezekana isiwe much ila ya kula hukosi lol,mie mpaka june 2017,nitakua nimeanzisha biashara ya mama ntilie :):):)
Mkuu, kutamka neno "anzisha" sio tabu...tabu mtaji ndugu....sina hata buku hapa. nafatilia uzi wangu kupitia simu ya jirani aisee.
 
hahaaaa mie kichwa changu ni hapo kimegota.

yupo Sweden au alikuwepo akarudi?

KM una kibali cha kuishi humo fungua mgahawa wako mweyewe mkuu,

Nchi nyingi za ulaya huhitaji capital kuanzisha biashara yako,kuna scheme nyingi zinazotoa grants ama loans.
dah we dada kilaza sana, kipi hujaelewa hapo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom