Niunganisheni na yule Mtanzania aliyefungua Mgahawa Sweden nikaoshe Vyombo. nina Diploma ya Catering

IamHumble

Senior Member
Dec 4, 2016
137
225
Wakuu,

Mimi ni msomi wa ngazi ya Diploma; Hotel Management & Catering na nina uzoefu wa miaka 4. Naombeni kwa yeyote anayemfahamu au mwenye mawasiliano na yule Mtanzania mwenzangu aliye fungua Mgahawa/Restaurant nchini Sweden niende nikawe hata Muosha vyombo maana nimehangaika sana sipati kazi japo nina sifa zote za kuajiriwa.

Nimekuwa nakula kwa kuunga unga kwa rafiki yangu ambaye ni mpishi wa Hoteli flani, ananiibia chakula na kunipitishia nyumbani. Hali imekuwa ngumu nikauza simu ambapo hela imeishia kwenye kutoa copy za Vyeti na Nauli za kuwasilishia maombi ya kazi bila mafanikio. Imebidi nije Internet cafe niwaandikieni, kama unamfahamu yule Mtanzania basi niunganishe nae. Nina ile Passport ndogo lakini ntajitahidi nipate kubwa lakini sina hata elfu 5 ya kunilinda linda aisee.

Najitahidi kuwa positive na kujikaza lakini kuna wakati nalia maana kila ninaemwelezea ananiambia kila mtu ana hali mbaya. Sasa leo nikapata wazo kwamba yule mtanzania wa Sweden anaweza kunisaidia. Please niPM...Niunganisheni nae jamani.
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,449
2,000
Pole sana mkuu,am speechless hizi nchi za watu zina changamoto nyingi sana,huo mji uliopo hauna kazi zozote hata caring kny nursing homes?au mkuu kibali chako cha kuishi humo kishaisha?
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
8,881
2,000
Mkuu umesema unauzoefu wa miaka minne? Naona ni uzoefu mkubwa sasa inakuaje usipate kazi...au unamatatizo yako nawewe maana it seems tayari ulishafanyaga kazi somewhere japo hujaweka wazi. Anyway jaribu kutafuta kazi hata zisizoendana na ulichosomea...hilo ndio hata mimi liliniokoa
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,449
2,000
Msome vizuri utaelewaa
hahaaaa mie kichwa changu ni hapo kimegota.

yupo Sweden au alikuwepo akarudi?

KM una kibali cha kuishi humo fungua mgahawa wako mweyewe mkuu,

Nchi nyingi za ulaya huhitaji capital kuanzisha biashara yako,kuna scheme nyingi zinazotoa grants ama loans.
 
TATIANA

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
4,365
2,000
Wakuu,

Mimi ni msomi wa ngazi ya Diploma; Hotel Management & Catering na nina uzoefu wa miaka 4. Naombeni kwa yeyote anayemfahamu au mwenye mawasiliano na yule Mtanzania mwenzangu aliye fungua Mgahawa/Restaurant nchini Sweden niende nikawe hata Muosha vyombo maana nimehangaika sana sipati kazi japo nina sifa zote za kuajiriwa.

Nimekuwa nakula kwa kuunga unga kwa rafiki yangu ambaye ni mpishi wa Hoteli flani, ananiibia chakula na kunipitishia nyumbani. Hali imekuwa ngumu nikauza simu ambapo hela imeishia kwenye kutoa copy za Vyeti na Nauli za kuwasilishia maombi ya kazi bila mafanikio. Imebidi nije Internet cafe niwaandikieni, kama unamfahamu yule Mtanzania basi niunganishe nae. Nina ile Passport ndogo lakini ntajitahidi nipate kubwa lakini sina hata elfu 5 ya kunilinda linda aisee.

Najitahidi kuwa positive na kujikaza lakini kuna wakati nalia maana kila ninaemwelezea ananiambia kila mtu ana hali mbaya. Sasa leo nikapata wazo kwamba yule mtanzania wa Sweden anaweza kunisaidia. Please niPM...Niunganisheni nae jamani.
. Stay strong life is a real struggle... Milima na mabonde tambarare ni chache
 
njiro

Senior Member
Nov 7, 2010
118
225
Fungus baba/mama ntilie yako, then ifanye iwe bora zaidi. Unaweza anza kwa kupika chai then unajiongeza Mdogo mdogo
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,839
2,000
Next time nikitembelea site yake ntakuletea email.
Ila kama walijua jina unakosa vipi kumpata,just google it
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,449
2,000
Fungus baba/mama ntilie yako, then ifanye iwe bora zaidi. Unaweza anza kwa kupika chai then unajiongeza Mdogo mdogo
Mie nilitaka kufungua,watu wakanikatisha tamaa,naskia kuna wanamgambo kibao,wanakimbizana na mama ntilie,ni kweli???nini changamoto za biashara hii....?
 
Mr Alola

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
478
1,000
Fungus baba/mama ntilie yako, then ifanye iwe bora zaidi. Unaweza anza kwa kupika chai then unajiongeza Mdogo mdogo
Hujamsikia akilia kwamba hana hata elfu 5 ya kumlinda, pia hana msaada kwa ndugu anakula kwa kuungaunga.

Sasa huo mtaji wa kufungulia ndo kimbembe.
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,839
2,000
Siku zote nilikuwa najiuliza Ethiopia ina uchumi mkubwa,treni za umeme,umeme wa uhakika,
kwanini watu wanakimbia toka kwa ethiopia na kujazwa kwenye matenka ilimradi wafike nchi nyingine kutafuta maisha,

mimi naona bora kurudi kwenye kile wanachokiita eti maisha fake ya awamu iliyopita,
punde tutaanza kuzalisha wakimbizi wa kiuchumi kwa maelfu
 
Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,456
2,000
kwa tunayoyajua maisha ya hapa mjini yaani huwa inafika kipindi unakoswa hata pesa ya kula kila ukienda kuomba kibarua nafasi zimejaa lazima nakuhakikishia utahama road.Jamaa etu hajakta tamaa bado anahitaji kusonga mbele naweza kuamini bado anahitaji kupambana zaidi ili apate ridhiki yake stahiki hivyo basi kwa anaye mjua jamaa mwenye hotel sweden amuunganishe naye japo cjui kama anataka kazi nje ya nchi tu humu jf wapo watu wanamahoteli makubwa tu pengne wangekushika mkono tu ukakomaa hapa kwa JPM.
 
Pilato Mweusi

Member
Dec 21, 2016
84
125
Bro kwanza pole sana, Hizi ni changa moto za maisha ila ningekupa kidogo ushauri angalau ukusukume kidogo..
Usitake kaz ulio somea maana utaangaika sana kupata hyo kaz jaribu kutafuta kaz yoyote ambayo itakuwa inakuingizia kipato, pili hyo diploma yako ya hotel management and catering unaweza jikusanya watu kama watano mkatengeneza ka group mkaanzisha catering service kwaajili ya maharusi,ubariko,sendoff na events nyingine hyo ni fursa tosha ya kujikimu. ukizingatia hayo utafanikiwa bro, Maisha sio kutafuta mbali na Tanzania. Huku ughaibuni wenzetu maisha ni very Expensive sasa ukija huku unazani maisha yako ndio yatakuwa rahisi, la hasha pambana ukisha kuwa na kipato kikubwa sasa fikiria kuja kwenye nchi za wenzetu.. ila siku katishi Tamaa bro Chamsingi Angalia whats Your minds tells you do,??
 
zanga

Senior Member
Dec 8, 2011
185
250
Chef Issa Kapande,Namfahamu vizuri.Tulifanya wote serena hotel wakati ikiitwa Royal Palm..mwaka 2005.

Pia tulikutana Tarangire Sopa Lodge akiwa chef Mkuu.

Hatujawasiliana kwa miaka 2 sasa nitatumia email tulokua tunawasiliana kama bado ipo active then nitakupatia akisha jibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom