Niunganishe soko la Kitunguu Kampala

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,372
3,945
Wakuu,

Kutokana na kufurika kwa soko la ndani la kitunguu kwa msimu huu,nimegundua hakuna namna zaidi ya kupeleka nje ya nchi.

Kampala inasemekana wana bei nzuri ila tatizo sijui lolote hapo sokoni.Mtu mwenye uzoefu au unamjua mwenye uzoefu naomba tuwasiliane.Mzigo uko Arusha unategemea kutoka mid December, gunia 100+

Shukrani.
 
Arusha inatembea 70,000 ,kwa kawaida ilitakiwa iwe 120,000 na ushee.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ila unavyoangalia inaweza kupanda mzee wangu
Kwa jinsi ilivyolimwa mwaka huu hata ikifika peak,yaani mwezi wa 2 haiwezi fika 250,000 kama msimu jana.
Ila inaweza fika 100,000 na kuendelea.
 
Unahitaji kibali mkuu kwahiyo hata ukipata soko bado inabidi ushughulikie kibali ili uweze kusafirisha Na kuuza huko otherwise upate mtu mwenye kibali aje kuchukua kwako mpeleke au upate Mganda aje kuchukua mzigo shambani kwako.

Nipo Kwenye mchakato wa kufuatilia soko la huko Ila mpaka sasa Hiyo ndio taarifa niliyo nayo, bado naendelea kufuatilia
 
Asante mkuu uendelee kutujuza
 
Za dukani
Na mpango wa kulima vitunguu mwakani lakini naziogopa sana mbegu za dukani kuna jamaa yangu alinunua halafu hazikuota kabisa nimeshuhudia mara,watu wanasema mbegu za kienyeji zipo vizuri zaidi na ni bei poa, me ni mzoefu sana wa kilimo cha mpunga ila nataka mwakani nilime tena mpunga na vitunguu, ila sina uzoefu na vitunguu, naomba nielimishe ndondoo mbili tatu hasa soko lake na uanikaji baada ya mavuno inakuwaje
 
Mkuu siyo kweli kwamba hazioti, yaani mimi nimetumia kilo tatu tu kwenye heka
4fdf007bed801638098c56ea3e114fec.jpg
 
Hiyo ni red Bombay na kilo ni 70,000/=, hivyo heka inakosti 210k
Nafikiri Hawa wanaouza mbegu hizi wengine sio waaminifu kabisa mbegu zinakuwa zime expiry, labda nitafute wakala mkubwa wa mbegu anaye eleweka
 
Uko wapi mkuu, moshi huwa kuna mhindi mmoja anakuuzia mbegu anakupa na guarantee, zisipoota atahusika, anasifika kwa kuuza mbegu poa
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Back
Top Bottom