Niulize swali lolote kuhusu Wilaya ya Kilombero

Mvidunda

Senior Member
May 30, 2020
122
170
Wakuu, mwenye kutaka kujua lolote/ chochote kuhusu Wilaya ya Kilombero iliyopo mkoani Morogoro, aulize nitamjibu. Iwe ni fursa za kibiashara, kilimo, siasa nakadhalika.

Karibuni kwa maswali, Karibuni Kilombero.

Wenu,

Mvidunda.
 
Safi sana mkuu

Gharama ya viwanja ikoje?
Shughuli za kiuchumi zinaendeshwa hapo wilayani?
 
Ukiacha Ifakara, kuna miji/senta gani nyingine zinafaa kwa wapambambanaji?

Ungekuwa wewe na una mtaji, na ni mgeni hapo kilombero na unataka kufanya biashara ya mpunga, ungelima au ungenunua na kuuza?

Tuanze na hayo kwanza
 
Vipi kilimo cha mpunga huko?mashamba yanapatikana kirahisi? Heka moja ya majaruba sh ngapi kununua?tuanze na hayo kwanza
 
Ni kweli wanawake wa huko hawana utaratibu wa kua na mume mmoja kwa kauli mbiu yao ya chungu hakienei kwa figa moja , na huwezi kubeba dumu ama ndoo ya maji bila ya kidumu?
 
Mkuu samahani, naomba hili jibu kwanza kabla ya mengine.

Ukiwa unaenda kilombero(Mimi niliishi ifakara) njiani kuna sehemu Ukipita tuu daraja flani kubwa unaacha rasmi lami unaingia barabara ya vumbi, ile sehemu inaitwaje na daraja nalo linaitwaje?

Yeyote anaweza kunijibu hili.

Nahitaji hili jibu serious.
 
Pale
Mkuu samahani, naomba hili jibu kwanza kabla ya mengine.

Ukiwa unaenda kilombero(Mimi niliishi ifakara) njiani kuna sehemu Ukipita tuu daraja flani kubwa unaacha rasmi lami unaingia barabara ya vumbi, ile sehemu inaitwaje na daraja nalo linaitwaje?

Yeyote anaweza kunijibu hili..
Nahitaji hili jibu serious.
Ile sehemu (Darajani) ni mpaka wa wilaya ya Kilombero na Kilosa. Kabla hujavuka Daraja unakuwa eneo linaitwa Ruaha, ukivuka Daraja ni Tarafa ya Mwanzo wilaya Kilombero, Tarafa Kidatu kijiji Mkamba. Hiyo ni kama unatoka Morogoro.
 
Asante,
Maliasili ni wapi? mkamba napo ni wapi?

Maana kuna mtu mwingine nilimuuliza katika kunielezea akataja hayo majina?
Alikosea au Ni maeneo karibu na pale?
 
Vipi kilimo cha mpunga huko?mashamba yanapatikana kirahisi? Heka moja ya majaruba sh ngapi kununua?tuanze na hayo kwanza
Kilombero ni wilaya inayozalisha zao la mpunga kwa wingi. Maeneo mengi yanafaa kwa kilimo hicho. Bei ya hekali kukodisha ama kununua inatofautia eneo mpaka eneo. Kukodi kwa msimu mmoja kwa kawaida inaanza 80 Elfu mpaka Laki na 20. Kutegemeana na eneo.
 
Maliasili unaamaanisha geti la maliasili, Geti lipo hatua hatua chache baada ya kuvuka daraja ukitokea Moro. Ni kijiji cha Mkamba Tarafa Kidatu.
Asante,
Maliasili ni wapi? mkamba napo ni wapi?

Maana kuna mtu mwingine nilimuuliza katika kunielezea akataja hayo majina?
Alikosea au Ni maeneo karibu na pale?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom