Niulize swali lolote kuhusu kuingiza pesa kupitia YOUTUBE

floow

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
411
852
Screenshot_20190831-165744_1567259902812.jpeg

Picha ya hapo juu ulikua ni Uzi wangu ambao niliuleta hapa hapa jamii forum mwaka 2017 mwezi wa 11 ,,kipindi ambacho nilikua nimechoka kufanya kazi niliyokuwa naifanya na nikawa naskia skia eti kupitia YOUTUBE unaweza kujiingizia pesa

Kwa bahati mbaya sikuweza kupata jibu lililo jitosheleza hapa jamii forum..ikanibidi niingie chaka la ma youtuber ili wanipe maujanja ya kuingiza hela ...

Nifupishe tuu kwa kusema nilihangaika sana kuhakikisha nakuwa mmoja wa watu wanaoingiza pesa kupitia youtube ..kwa Bahati nzuri jambo hilo limewezekana na kwa sasa YOUTUBE ndio maisha yangu..

Najua kuna vijana wengi wanatamani kujiingizia kipato kupitia YOUTUBE na hawajui wapi pa kuanzia ...haya sasa nakaribisha maswali
 
watu wanaingizaje fedha youtube?
Watu hujiingizia fedha za youtube kupitia vidio wanazo zi pakia kwenye youtube Chanel zao

Kama umefungua vidio yoyote youtube na ukakutana na tangazo lolote kwenye hiyo vidio (mfano tangazo linalotaka u SKIP)
Basi wewe kitendo cha kuliona hilo tangazo ndio tayari umemuingizia Fedha
 
Unapataje pesa mkuu na unazitoaje ziwe mikononi mwako
Kituochako cha youtube kikiwa tayari kimeruhusiwa kupitisha Ads /kimekuwa monetized / kimeruhusiwa kupitisha matangazo

Basi vidio zako zote utakazokuwa unazipakia YOUTUBE zitakuwa zinapitishiwa matangazo ,hapo watu wakiangalia wengi ndio utapata pesa nyingi na wakiangalia watu wachache basi hata pesa utapata kidogo

Pesa unaingiziwa kwa njia ya Benki (unayoitaka wewe)
Pia njia nyingine inayotumia kutoa pesa ni western UNION
 
Asante mkuu kwa uzi huu, nina wiki mbili sasa npo chimbo najifunza namna ya kupiga pesa youtube na njia nyinginezo za online

Swali langu, unahitaji kuwa na at least subscribe ngapi ili hzo ads au matangazo yaruhusiwe kupitishwa kwa a/c au ni sifa gani za ziada mtu anapaswa kuwa nazo ili ads zipitishwe kwenye a/c ya mtu
 
View attachment 1194335

Picha ya hapo juu ulikua ni Uzi wangu ambao niliuleta hapa hapa jamii forum mwaka 2017 mwezi wa 11 ,,kipindi ambacho nilikua nimechoka kufanya kazi niliyokuwa naifanya na nikawa naskia skia eti kupitia YOUTUBE unaweza kujiingizia pesa

Kwa bahati mbaya sikuweza kupata jibu lililo jitosheleza hapa jamii forum..ikanibidi niingie chaka la ma youtuber ili wanipe maujanja ya kuingiza hela ...

Nifupishe tuu kwa kusema nilihangaika sana kuhakikisha nakuwa mmoja wa watu wanaoingiza pesa kupitia youtube ..kwa Bahati nzuri jambo hilo limewezekana na kwa sasa YOUTUBE ndio maisha yangu..

Najua kuna vijana wengi wanatamani kujiingizia kipato kupitia YOUTUBE na hawajui wapi pa kuanzia ...haya sasa nakaribisha maswali
#Vipi swala la tcra na usajili wa account zote Za YouTube nchini.ww hili umelimudu vipi?

#Ilikuchukuwa mda gani kuanza kulipwa na ulikuwa na views na subscribe ngapi na ulilipwa bei gani.

#kwann YouTube kunautofauti wa malipo Kwa maarifa mbalimbali.?
 
Asante mkuu kwa uzi huu, nina wiki mbili sasa npo chimbo najifunza namna ya kupiga pesa youtube na njia nyinginezo za online

Swali langu, unahitaji kuwa na at least subscribe ngapi ili hzo ads au matangazo yaruhusiwe kupitishwa kwa a/c au ni sifa gani za ziada mtu anapaswa kuwa nazo ili ads zipitishwe kwenye a/c ya mtu
Fikisha subscriber 1000
Pamoja na masaa 4000 ya watazamaji
Hapo YOUTUBE wataikagua youtube channel yako ,ikiwa safi basi watakupitishia matangazo rasmi

Zingatia
Youtube hawataki vidio zenye maudhui ya ngono,hawataki vidio za vitisho vya ukweli pia wanataka vidio zako zizingatie haki za watoto ..ukiyaweza hayo basi kituo chako cha youtube kitapitishiwa matangazo mapema sana
 
Ilinichukua miezi 7 kuanza kulipwa na youtube

Kuhusu TCRA kwa sasa nimesha jisajili na natambulika ,,lakini nilikaa mda mrefu bila kujisajili TCRA
#Vipi swala la tcra na usajili wa account zote Za YouTube nchini.ww hili umelimudu vipi?

#Ilikuchukuwa mda gani kuanza kulipwa na ulikuwa na views na subscribe ngapi na ulilipwa bei gani.

#kwann YouTube kunautofauti wa malipo Kwa maarifa mbalimbali.?
 
Ilinichukua miezi 7 kuanza kulipwa na youtube

Kuhusu TCRA kwa sasa nimesha jisajili na natambulika ,,lakini nilikaa mda mrefu bila kujisajili TCRA
#TCRA uliwalipa tsh. ngapi Kwan ajili ya channels yako.

#mara ya kwanza ulilipwa USD. Ngapi na YouTube?
 
I kuhusu swala TCRA vipi?
Unawalipa au inakuwa vipi sasa hapo Maana wanasema kumiliki youtube channel mpaka ulipie ?
Huyu Mc pilipili walimpeleka mpaka mahakamani kabisa Mkuu?
Wewe hapa umefanyaje Mkuu na mimi nina ndoto yakuanzisha youtube channel tangia kitambo ila naogopa hawa TCRA Mkuu
 
Back
Top Bottom