VVU na UKIMWI: Historia yeke, chanzo cha maambukizi, dalili, kinga na juhudi za kupambana na ugonjwa huu

Inakuwaje unatembea na Muathirika wa HIV na haupati?
Sio mara zote mtu unapokutana na mtu mwenye maambukizi ya VVU anaweza kupata maambukizi pia. Kuna sababu mbalimbali zinaweza kusababisha mtu kutopata maambukizi, lakini kwa ufupi kabisa inategemea na afya ya huyu mtu kwa ujumla iwapo anaambukizi mengine, lishe yake, magonjwa ya zinaa, na sababu za kigenetiki na pia aina ya sex waliyofanya pamoja na hali ya afya ya mgonjwa iwapo anatumia dawa
 
Inawezekana umekuwa na maswali ambayo yamekuwa yakikutatiza juu ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI.

Leo nakupa nafasi ya kuuliza swali lolote juu ya mada hii. Twende kazi!

Naomba kufahamishwa kuhusiana na faida za dawa mpya ambayo itaanza kutumika hapa Tanzania kama FDC - First Line Regimen.... TLD ikilinganishwa na hii inayotumika sasa ya TLE.

Asante
 
Mkuu Mimi Nataka kujua haya

1. Inasemekana HIV ndo kirusi hasa anasababisha UKIMWI, je ni kweli Hamna Mtu yoyote aliwahi mwona Huyu virus?

2. Inasemekana UKIMWI haumui victim, Ila magonjwa mengine nyemelezi, so let's assume AIDS victim is exposed Katika mazingira free of any diseases, je Huyu hatakufa?

1.Virusi ni vimelea wadogo sana. Hawawezi kuonekana kwa macho lakini wanaweza kuonekana kwa kutumia electronic microscope

2.mtu akiwa katika mazingira ambayo hawezi kupata maambukizi mengine hawezi kufariki kutokana na virus hawa
 
Kuhusu virus kuwa wadogo Lazima electronic microscope hiyo si tu virus Hata bacteria, and some protozoans

Nilichouliza mimi Inasemekana kwamba HIV virus Hamna aliewahi kumwona even using such device. Je ni kweli, if so lete proof mkuu
1.Virusi ni vimelea wadogo sana. Hawawezi kuonekana kwa macho lakini wanaweza kuonekana kwa kutumia electronic microscope

2.mtu akiwa katika mazingira ambayo hawezi kupata maambukizi mengine hawezi kufariki kutokana na virus hawa
 
Naomba utupatie shule pana ya Discordant Couples katika maambukizi ya Ukimwi. Faida na Hasara zake pia
Naomba kufahamishwa kuhusiana na faida za dawa mpya ambayo itaanza kutumika hapa Tanzania kama FDC - First Line Regimen.... TLD ikilinganishwa na hii inayotumika sasa ya TLE.

Asante
Mmaswali yako yanaweza kusababisha mtu kukimbia maswali wakati wowote kuanzia sasa
 
Omary Ndama,
1.vipimo vimavyotumika ni vile ambavyo vinaangalia iwapo mwili umetengeneza kinga dhidi ya maambukizi ya VVU hivi vinatumika katika nchi mbalimbali. Matumizi ya PCR ni bei ghali!
2.Hauwezi kuwa wa kisaikolojia kwa sababu kuna medical cause ambao ni HIV. MATATIZO YA KISAIKOLOJIA HUWA HAYANA MEDICAL CAUSE.
3. Hii dhana yako sio kweli. Kwa sasa waathirika wa UKIMWI Wanaishi kwa muda mrefu sana.
4Swali lako hili umechanganya vitu. ARV zina madhara kama zilivyo dawa nyingine. Ni kweli baadhi ya dawa zinaweza kusababisha mwili kufa ganzi. Hata hivyo unapopata madhara yoyote unabadilishiwa dawa
 
Naomba maelezo mkuu why waathirika wa UKIMWI wengi wao wanakuwa ni wenye hasira mda wote?
 
Naomba utupatie shule pana ya Discordant Couples katika maambukizi ya Ukimwi. Faida na Hasara zake pia
Discordant couples kwa lugha rahisi ni kwamba mwanandoa mmoja ameathirika na mwingine hajaatharika. Kitu gani kinachosababisha hali hii kutokea hakijulikani. Hata hivyo watafiti wanafikiria juu ya mambo mengi mfano jinsia, genitiki, afya ya wanandoa, matumizi ya kondom nk nk.

Hasara kubwa ni kwamba hali hii inachangia kuenea sana kwa maambukizi
Faida ni kuwa hawa wanandoa wanaweza kuwa sampuli nzuri katika majaribio kinga na tiba ya UKIMWI
 
Naomba kufahamishwa kuhusiana na faida za dawa mpya ambayo itaanza kutumika hapa Tanzania kama FDC - First Line Regimen.... TLD ikilinganishwa na hii inayotumika sasa ya TLE.

Asante
TLD D kwenye huu mseto wa dawa ni Dolutegravir ni integrase inhibitor. Dawa hii imeonekana kuwa ina nguvu kuliko dawa zozote za jamii yake. Ndio maana FDA wameshauri itumike katika line ya kwanza ya matibabu ya HIV
 
Back
Top Bottom