Niulize juu ya ugonjwa wako nikwambie tiba ya maji ya matunda za mboga za majani

Kuna jamaa yangu anasumbuka wakati wa kupumua yani kama vile kifuani kuna hewa imeganda.Tumsaidieje huyu mkuu.

mafisadi hayana chama
 
Nina shoga yangu ana makovu mwili mzima, hajawai kuvaa nguo fupi hata vibody lazima avae mikono mirefu

Tatizo anasema aking'atwa na mbu akajikuna hilo kovu alitoki miaka alushatumia vitu vingi bila mafanikio makovu yapo mwili mzima except usoni shingon, kwenye vidole na miguuni kwa chini sehemu zilizobaki ni makovu meusi afu yeye ni mweupe so yanaonekana

Ana shape balaa kila mwanaume anamtongoza ila anaogopa kulala nao kuofia hayo mokovu yaan kweli kivuri hakikosi kasoro.

Dr naomba majibu. Thanks in advance
 
Tunapoumwa ni vema kwenda Hospitali au zahanati ili kupima vipimo kwa lengo la kubaini ugonjwa unaosumbua. Hili ni jambo jema kwani haishauriwi kukimbilia kwenye maduka ya madawa kununua dawa. Kumeza dawa bila kujua unaumwa nini ni hatari kwa afya ya mwili wako kwani dawa yaweza kuwa sumu ikakudhuru hata kama sio muda huo huo basi miaka ya baadae!

Wengine wetu tumeenda kutibiwa kwa dawa za kizungu na pengine hatukupona na tunaendelea kukata tamaa ya kutokupona. Hii imefanya kuibuka kwa zahanati au clinic za Tiba Mbadala. Nyingi za Zahanati au Clinic hizi hutumia tiba/dawa zinazotengenezwa kutokana na maji ya matunda na mboga za majani. Waendesha tiba hizo wengine wanatoza pesa nyingi na unapewa dawa ambayo hujui viambata (composition) vyake. Hawapendi kila mtu ajue maana watakosa wateja!

Sasa mie
Kamanda Kazi napenda wewe uwe daktari wa afya yako, wewe mwenyewe kwa kutumia tiba ya juisi ya matunda na mboga za majani. Ni gharama nafuu sana. Wewe niulize aina yoyote ya tatizo/ugonjwa unaokusibu na mimi nitakwambia tiba yake. Sikupi tiba/dawa bali utatengeneza wewe mwenyewe. Mimi kazi yangu ni kukupa maelekezo tu. Faida ya aina hii ya tiba ni kwamba haina madhara yoyote kwa mwili wako hata unywe dumu la lita 20 la dawa. Lakini hizo dawa za kizungu zidisha dozi uone...! Jambo la maana ninakusisitiza...PIMA AFYA YAKO KWANZA UJUE UGONJWA kisha jimwage hapa jamvini tuambizane!

Nimeamua kutumia njia hii ya mtandao maana nikisubiri hadi niandike vitabu itanichukua muda kutokana na majukumu niliyonayo. Pia nasukumwa na hiyari ya moyo wangu kufanyika msaada kwa binadamu wenzangu. Najua kuna wengine wamekata tamaa ya kuishi. Ndugu yangu usivunjike moyo...MUNGU YUPO! Ukishindwa kujimwaga hapa badi ni-pm tu. Kwa wale watakaopenda kuonana na mimi ana kwa ana tunaweza kupanga miadi. KARIBUNI SANA NDUGU ZANGU!

Kwa wale ambao nachelewa kuwajibu maswali yao waniwie radhi kwani ninakuwa na majukumu mengi na kikazi hata nashindwa kujibu kwa wakati. Pia napenda niseme hili. Tiba ya juisi au vyakula ni tiba nzuri sana ila unapaswa kuwa mvumilivu. Matokeo hayaonekani kwa siku moja au mbili bali vile unavyojituma kutumia tiba hiyo ndivyo una-speed up kupona kwako. Tofauti ya tiba hii na ile ya dawa zilizotengenezwa na makampuni ya madawa ni hii. Hii tiba hushughulikia tatizo kwenye chanzo chake kabisa. Mathalani kama tatizo ni viungo kuuma, tiba ya juisi na matunda hutibu chanzo kilichosababisha viungo kuuma. Wakati dawa za viwandani hushughulikia kuondoa maumivu. Maumivu yanaweza kuondoka lakini baada ya siku au mwezi yakarudi tena. Kwa nini? Sababu chanzo cha tatizo hakikushughulikiwa.

Bila kusahau madawa ya viwandani yana sumu. Kadiri unavyotumia kuna sumu inabaki mwilini. Baada ya miaka kadhaa sumu hiyo inaleta tatizo jingine mwilini mwako.
Kamanda Asante kwa Utoaji Hugo, Aliye tuumba Atakuja yaliyo mema
 
Kamanda KAZI, Nifahamishe nifanye nini!
Nasumbuliwa na maumivu kuanzia chini ya mgongo kupitia ndani ya matako kutelemkia mapajani kwa nyuma hadi miguuni kwenye nyayo na kupata ganzi wakati mwingine Kama moto.
Nini Tiba yake?
 
Nataka ni nenepe walau nikivaa suti nipendeze, cz kamwili kangu ni kadogo kuliko hata Mliki wa JF.
Please.
Mnyama anayeliwa pekee ndo akinenepa anapendeza.... fanya mazoezi epuka unene uzio wa lazima
 
Chukua mdarasini uusage (usiwe unga saana..kiasi tu), weka kwenye maji chemsha. Kisha mimina kwenye glasi, miminia unga wa pilipili kidogo na kisha tia asali kijiko kimoja cha chakula. Kunywa. Tumia mara tatu kwa siku na endelea kutumia kila siku mpaka upone.

Angalia pia mazingira unayoishi, fyeka majani, fukia madimbwi ya maji, ondoa vigae vinavyotuamisha maji. Ukiweza tumia mosquitor repelant kupaka ikifika jioni.

Tumia hiyo then utaleta majibu. Zipo tiba zingine pia ila anza na hiyo.
Mkuu utakuja kuua watu wewe. Hakuna malaria parasite anayeondolewa kwenye damu kwa unga wa mdalasini
 
Tunapoumwa ni vema kwenda Hospitali au zahanati ili kupima vipimo kwa lengo la kubaini ugonjwa unaosumbua. Hili ni jambo jema kwani haishauriwi kukimbilia kwenye maduka ya madawa kununua dawa. Kumeza dawa bila kujua unaumwa nini ni hatari kwa afya ya mwili wako kwani dawa yaweza kuwa sumu ikakudhuru hata kama sio muda huo huo basi miaka ya baadae!

Wengine wetu tumeenda kutibiwa kwa dawa za kizungu na pengine hatukupona na tunaendelea kukata tamaa ya kutokupona. Hii imefanya kuibuka kwa zahanati au clinic za Tiba Mbadala. Nyingi za Zahanati au Clinic hizi hutumia tiba/dawa zinazotengenezwa kutokana na maji ya matunda na mboga za majani. Waendesha tiba hizo wengine wanatoza pesa nyingi na unapewa dawa ambayo hujui viambata (composition) vyake. Hawapendi kila mtu ajue maana watakosa wateja!

Sasa mie
Kamanda Kazi napenda wewe uwe daktari wa afya yako, wewe mwenyewe kwa kutumia tiba ya juisi ya matunda na mboga za majani. Ni gharama nafuu sana. Wewe niulize aina yoyote ya tatizo/ugonjwa unaokusibu na mimi nitakwambia tiba yake. Sikupi tiba/dawa bali utatengeneza wewe mwenyewe. Mimi kazi yangu ni kukupa maelekezo tu. Faida ya aina hii ya tiba ni kwamba haina madhara yoyote kwa mwili wako hata unywe dumu la lita 20 la dawa. Lakini hizo dawa za kizungu zidisha dozi uone...! Jambo la maana ninakusisitiza...PIMA AFYA YAKO KWANZA UJUE UGONJWA kisha jimwage hapa jamvini tuambizane!

Nimeamua kutumia njia hii ya mtandao maana nikisubiri hadi niandike vitabu itanichukua muda kutokana na majukumu niliyonayo. Pia nasukumwa na hiyari ya moyo wangu kufanyika msaada kwa binadamu wenzangu. Najua kuna wengine wamekata tamaa ya kuishi. Ndugu yangu usivunjike moyo...MUNGU YUPO! Ukishindwa kujimwaga hapa badi ni-pm tu. Kwa wale watakaopenda kuonana na mimi ana kwa ana tunaweza kupanga miadi. KARIBUNI SANA NDUGU ZANGU!

Kwa wale ambao nachelewa kuwajibu maswali yao waniwie radhi kwani ninakuwa na majukumu mengi na kikazi hata nashindwa kujibu kwa wakati. Pia napenda niseme hili. Tiba ya juisi au vyakula ni tiba nzuri sana ila unapaswa kuwa mvumilivu. Matokeo hayaonekani kwa siku moja au mbili bali vile unavyojituma kutumia tiba hiyo ndivyo una-speed up kupona kwako. Tofauti ya tiba hii na ile ya dawa zilizotengenezwa na makampuni ya madawa ni hii. Hii tiba hushughulikia tatizo kwenye chanzo chake kabisa. Mathalani kama tatizo ni viungo kuuma, tiba ya juisi na matunda hutibu chanzo kilichosababisha viungo kuuma. Wakati dawa za viwandani hushughulikia kuondoa maumivu. Maumivu yanaweza kuondoka lakini baada ya siku au mwezi yakarudi tena. Kwa nini? Sababu chanzo cha tatizo hakikushughulikiwa.

Bila kusahau madawa ya viwandani yana sumu. Kadiri unavyotumia kuna sumu inabaki mwilini. Baada ya miaka kadhaa sumu hiyo inaleta tatizo jingine mwilini mwako.

Hizo rangi ulizoweka Kwa uzi zinaumiza macho bhana!!!
 
Back
Top Bottom