Niulize juu ya ugonjwa wako nikwambie tiba ya maji ya matunda za mboga za majani

jibu maswali haya:-
je haoneshi dalili za uvimbe maeneo ya mashavu au karibu na taya au masikio?
Je haongelei puani?
Je hapati tabu kupua?
Amekwisha wahi kupima kifua kikuu?Jee si mtumbukiza "earphone" masikioni?
Baada ya kujibu takushauri uende hospitali kubwa ya rufaa ya serikali upate vipimo zaidi kama hawaja gundua matatizo tena unijulishe
Hizo dalili hazipo,ila tu kwenye pua tundu moja huziba na kuachia then jingine pia. Na si mtumiaji sana wa earphones na kuhusu kupima kifua kikuu halijafanyika
 
Nasumbuliwa na mafua yasiyokwisha. hasa napokuwa maeneo ya baridi kama Mbeya. napiga chafya sana na kukohoa kidogo na koromeo kuwashwa then nikilikuna nakuwa nanguruma kama nguruwe.
Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwa moyo wako wa upendo kujitolea kwa ajili yetu! Mungu azidi kukuzidishia maarifa kwa uwezo wake, naomba kufaham, kuna Tatizo lolote mtu anaweza kulipata kwa kunywa maji ya baridi asubuhi kabla ya kula kitu chochote??
 
Kausha maganda ya ndizi halafu uyaponde ponde mpka yawe unga kbs....matumizi Asubuhi vijiko viwili vikubwa vya unga na asali....mimi binafsi Nilikuwa natumia hiyo mpka nimepona kbs
Asali kiasi gani unachanganya au unatanguliza chochote kati ya maganda ya ndizi na asali na unatakiwa utumie kabla ya kula au baada ya kula?? na nikae muda gani kabla ya kula na nile baada ya muda gani kunywa dawa???

nisaidie kaka hali ni mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tunapoumwa ni vema kwenda Hospitali au zahanati ili kupima vipimo kwa lengo la kubaini ugonjwa unaosumbua. Hili ni jambo jema kwani haishauriwi kukimbilia kwenye maduka ya madawa kununua dawa. Kumeza dawa bila kujua unaumwa nini ni hatari kwa afya ya mwili wako kwani dawa yaweza kuwa sumu ikakudhuru hata kama sio muda huo huo basi miaka ya baadae!

Wengine wetu tumeenda kutibiwa kwa dawa za kizungu na pengine hatukupona na tunaendelea kukata tamaa ya kutokupona. Hii imefanya kuibuka kwa zahanati au clinic za Tiba Mbadala. Nyingi za Zahanati au Clinic hizi hutumia tiba/dawa zinazotengenezwa kutokana na maji ya matunda na mboga za majani. Waendesha tiba hizo wengine wanatoza pesa nyingi na unapewa dawa ambayo hujui viambata (composition) vyake. Hawapendi kila mtu ajue maana watakosa wateja!

Sasa mie
Kamanda Kazi napenda wewe uwe daktari wa afya yako, wewe mwenyewe kwa kutumia tiba ya juisi ya matunda na mboga za majani. Ni gharama nafuu sana. Wewe niulize aina yoyote ya tatizo/ugonjwa unaokusibu na mimi nitakwambia tiba yake. Sikupi tiba/dawa bali utatengeneza wewe mwenyewe. Mimi kazi yangu ni kukupa maelekezo tu. Faida ya aina hii ya tiba ni kwamba haina madhara yoyote kwa mwili wako hata unywe dumu la lita 20 la dawa. Lakini hizo dawa za kizungu zidisha dozi uone...! Jambo la maana ninakusisitiza...PIMA AFYA YAKO KWANZA UJUE UGONJWA kisha jimwage hapa jamvini tuambizane!

Nimeamua kutumia njia hii ya mtandao maana nikisubiri hadi niandike vitabu itanichukua muda kutokana na majukumu niliyonayo. Pia nasukumwa na hiyari ya moyo wangu kufanyika msaada kwa binadamu wenzangu. Najua kuna wengine wamekata tamaa ya kuishi. Ndugu yangu usivunjike moyo...MUNGU YUPO! Ukishindwa kujimwaga hapa badi ni-pm tu. Kwa wale watakaopenda kuonana na mimi ana kwa ana tunaweza kupanga miadi. KARIBUNI SANA NDUGU ZANGU!

Kwa wale ambao nachelewa kuwajibu maswali yao waniwie radhi kwani ninakuwa na majukumu mengi na kikazi hata nashindwa kujibu kwa wakati. Pia napenda niseme hili. Tiba ya juisi au vyakula ni tiba nzuri sana ila unapaswa kuwa mvumilivu. Matokeo hayaonekani kwa siku moja au mbili bali vile unavyojituma kutumia tiba hiyo ndivyo una-speed up kupona kwako. Tofauti ya tiba hii na ile ya dawa zilizotengenezwa na makampuni ya madawa ni hii. Hii tiba hushughulikia tatizo kwenye chanzo chake kabisa. Mathalani kama tatizo ni viungo kuuma, tiba ya juisi na matunda hutibu chanzo kilichosababisha viungo kuuma. Wakati dawa za viwandani hushughulikia kuondoa maumivu. Maumivu yanaweza kuondoka lakini baada ya siku au mwezi yakarudi tena. Kwa nini? Sababu chanzo cha tatizo hakikushughulikiwa.

Bila kusahau madawa ya viwandani yana sumu. Kadiri unavyotumia kuna sumu inabaki mwilini. Baada ya miaka kadhaa sumu hiyo inaleta tatizo jingine mwilini mwako.


Mkuu nnapata choo cha kamasi kamasi,na ushuzi wenye harufu sana,nimemeza dawa aina nyingi sana miaka km mitatu sijapona,tatizo linarudia Mara kwa Mara,wengine wananambia nnafagus tumboni,wengine bawasiri kila mtu anasema lake,kila nikipima hospitali hawaoni kitu,
Mara ingine kiuno kinauma na kuna mt u kanambia nnamadonda ya ndani ya mdongo,
Hii ni nn mkuu,
Msaada tafadhari,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom