Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Kuna wimbo wa Baba Asha, namba moja na namba mbili...
Ulikuwa na maneno yafuatayo
Huyu Baba Asha itabidi anambie usiku wa jana alilala wapi? Mimi aliniaga anakwenda kulinda usiku wa jana ndio zamu yake... Mbona mjunbe mzee Jongo lalalalalal
Sungu sungu hakukinda Baba Asha na ndani hakulala Baba Asha....
Dah jamani mwenye nao tafadhari nauomba...
 
Kuna nyimbo hisani Gari kubwa waliimba kama dongo kwa bendi nyingine, sijui jina la nyimbo ila inaanza kwa "walishindwa watu kweli wazazi wa majumbani, wenye kutoa Ukali na Radhi za midomoni," unaweza kunipa sababu Za wimbo huu kutungwa?
Kiuhalisia Maana ya neno huijua mwenye kutoa neno hilo,kiukweli kusudio halisi la Hisani Gari kubwa(Meli ya sumu)silifahamu.Lakini labda niingie kazini kuwadodo jamaa zangu ambao waliwahi kuwa wanamuzi wa bendi hiyo wanaweza kuniambia.
 
Kuna wimbo wa Baba Asha, namba moja na namba mbili...
Ulikuwa na maneno yafuatayo
Huyu Baba Asha itabidi anambie usiku wa jana alilala wapi? Mimi aliniaga anakwenda kulinda usiku wa jana ndio zamu yake... Mbona mjunbe mzee Jongo lalalalalal
Sungu sungu hakukinda Baba Asha na ndani hakulala Baba Asha....
Dah jamani mwenye nao tafadhari nauomba...
Nitakufanyia mpango,hizo nyimbo wenyewe ni Atomic Music(Omary Omary)na zipo namba 1-4,na mjumbe alikuwa anaitwa Mzee Nanga.Huyo Nanga yy alikua ni rapper kwenye bendi hiyo na baadae alihama na kuamia Seven Survivor ya Juma Mpogo.
 
Ki uhalisia huu mziki hauna kabila maalum,in short ni mziki wa watoto wa mjini.Sababu mnanda wakati unashika hatamu enzi ya bendi kama Hisani Gari kubwa,Uraibu,Tokyo ngoma,Kombora Music na nyinginezo,zilikua na watu waliochanganyika kutoka makabira tofauti jijini Dar es salaam.
Ongeza na dar nyota
 
Ashaaaa niambie ukweli kama hunitaki usinitapeli... ilikua balaaa

kondakta kaja juu akasema haiwezekani kupanda bure imeruhusiwa jeshi la polisi..
mnanda sema tu hawauelewi

Btw Asha imeimbwa na jack simela au
Asha imeimbwa na baba jey marehemu huyu,,, na ndo kilikuwa kichwa cha jagwa. Kaimba nafikili kuanzia namba Tatu mpaka tano. Baada ya kufa namba Sita kaimba igoshi. Jack simela nafikili kaanzia saba
 
Nitakufanyia mpango,hizo nyimbo wenyewe ni Atomic Music(Omary Omary)na zipo namba 1-4,na mjumbe alikuwa anaitwa Mzee Nanga.Huyo Nanga yy alikua ni rapper kwenye bendi hiyo na baadae alihama na kuamia Seven Survivor ya Juma Mpogo.
Asante sana...
Ni kweli, ni mzee Nanga na sio Jongo kama nilivyosema. Upo sahihi sana. Nilifanikiwa kusikiliza moja na mbili. Nitashukuru zikipatiakana. Kama kuna gharama itahitajika nipo tayari kuchangia. Asante
 
Bendi kama Dar Nyota na Night Star ya Haidary Kessy,hizi kiuhalisia huwezi kuziita mnanda,hizi ni chakacha.Sababu ukisikiliza kuanzia santuri ya upigaji hadi vifaa.
 
Tunaomba utusaidie tofauti ya MNANDA,MCHIRIKU NA CHAKACHA .na kama utakuwa na nyimbo za aina hizo tatu tuwekee kuwa hii ni chaka,hii ni mchi na hii ni mnand

Bendi kama Dar Nyota na Night Star ya Haidary Kessy,hizi kiuhalisia huwezi kuziita mnanda,hizi ni chakacha.Sababu ukisikiliza kuanzia santuri ya upigaji hadi vifaa.
 
Ki uhalisia huu mziki hauna kabila maalum,in short ni mziki wa watoto wa mjini.Sababu mnanda wakati unashika hatamu enzi ya bendi kama Hisani Gari kubwa,Uraibu,Tokyo ngoma,Kombora Music na nyinginezo,zilikua na watu waliochanganyika kutoka makabira tofauti jijini Dar es salaam.

Tokyo Ngoma home boys hawa.
 
Back
Top Bottom