Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Hapo Tops kulikua na wahuni wakutosha na ndio ilisababisha zile maskani ( garden ) kupigwa marufuku maana ilikua ganja ganjani unga ngada kwa kwenda mbele.kulikua na vile vikundi vya komando yosso kama wale panya road.Usisahau wale wahuni wa pale mwembeyanga Farmer Gusta

Farmer Gusta Mwemberadu pale juu kidogo ya mwembe yanga, Press Contractor Sandali Mamboleo,... yaani ilikuwa unakuta vijiwe vijana wanajikusanya ganja ganja, Wahuni wa mikoroshini kina Van damme..... huu music ni mzuri ni baadhi ya miziki ya asili ya watu wa uswahilini wenye kuleta raha.
 
Mkuu ilikua ndio njia yangu ya kuendea nyumbani nikitoka shule kuelekea relini
 
Iko hivi Mwandende,mziki wa mnanda hapo mwanzo kabisa ulikua unatambulika kama chakacha.Katika awamu hiyo ya chakacha mziki huu ulikua na mandhari ya ubasha na ushoga,na hata upigaji wao ulikua wa santuri ya miondoko raini na vifaa kama magitaa viliusika na madensa wake au wachezaji waliitwa mafaruku.Hapo unaweza kuziona bendi maarufu kama vile Dar Nyota na Night Star ya akina Haidary Kessy.

Lakini baadae mziki huu ulipiga hatua na kupokelewa na watoto wa uswahili,ambao wao kwanza hawakua na vifaa vya kisasa na lakini pia walitaka mziki wenye mandhari ya kuchezeka kisela na kuruka kiuswahili na si kusikiliza na kunengua mauno.Ndipo hapo mziki huu inaingia hatua ya pili kwani unabadilika mandhari na upigaji na kuitwa Mchiriku,hapa bendi maarufu iliyotamba sana ni Hisani Gari Kubwa(Meli ya sumu)wahuni kutoka Mwananyamala kwa Manjunju.

Lakini kadri muda ulivyosonga ndipo makundi zaidi yakawa yanaibuka na ubunifu ukawa unaongezeka na upigaji pia,hapa ndio mziki unaingia hatua nyingine na kuingia kwenye mnanda.Hapa kwenye kumbukumbu ya bendi nyingi sana kama Jagwa,Wanyamwezi,Chaukucha,Topaz,Kombora,Atomic,Tokyo ngoma,Miami Yankees,New Kiwembe,Seven Survivor,Buti Kubwa,Uraibu na nyingine nyingi.

Nafikiri kwa maelezo hayo utakua umeshapata picha ni wapi mziki huu ulipotoka hadi kuwa mziki kipenzi kwa makundi ya vijana na jamii nzima katika miaka hiyo ya 90 na 2000.
Sawa mkuu,,
 
Hamna mziki naukubali kama mchiriku Nawakubali sana seven survival japo sijui hata nazipataje nyimbo zao.Efm wakati inaanza ilikuwa ni mchiriku mwanzo mwenga japo na wenyewe naona wamefifia kuupromote sasa wanakumbatia masingeli ambayo hayana hata maana
 
Oscar Mkoba, hii ngoma Jagwa walimuimbia mshkaji wao baada ya kupigwa mapanga na kufariki dunia. Ila kwa wadau mnaojua kwa kina naomba mnifahamishe chanzo cha mshkaji kupigwa mapanga hadi kupelekea kufariki dunia.
Huzuni na majonzi, Yalotufika sisiiii
Kwa kuondokewa na mshkaji wetu, Oscar mkoba
Kifo chake, Oscar kinasikitisha sana
Kapigwa pigwa mapanga yani kama mdudu.

Wanangu wa Temeke poleni kwa kuondokewa na msela wa kitambo, muhuni wa zamani Ngwena.
 
Oscar mkoba alikua muhuni pale ccm mwinyi Juma jagwa walikua wanapiga show siku hiyo akacheza Sana jagwa alivyotoka akaenda maeneo ya jirani na kuvunja stoo na kuiba alivyoiba wakamkamata wakamuua
 
Hii miziki japokua ilikua ikionekana kupigwa na wahuni lakini walikua smart kwa lugha ya matusi hawakua wakitukana kama wa singeli. walitumia tafsida ya hali ya juu katika nyimbo zao.
Rejea wimbo wa Maswala kunesa, Maswala kubembea. huwezi jua maana ya huu wimbo mpaka utafsiriwe, na hii ndio sanaa inatakiwa iwe.
RIP Mnanda.
 
"Maswala kunesa,maswala kubembea.Bw Kicheko bembea mpaka ucheue.",hapo imetumika tasfida tu lakini kiuhalisia walisifia #Unga(ngada)ambayo ilikua ndio starehe ya wajanja,na isitoshe wakati huo miaka ya 91,92,93 ndio unga ulikua umeanza kutawala kwa wajanja wa uswahilini hususan Mwananyamala ilipokua makao makuu ya bendi ya Hisani Gari kubwa.
 
Mim binafsi wimbo wangu ninaopenda kutoka jagwa music kichwa cha nyoka.
"Kichwa cha nyoka" nyimbo hii ilikua ni dongo,pale Jagwa palitokea mtafaruku uliopelekea baadhi ya mastaa kutimka na kwenda kujiunga na bendi ya Chaukucha ambayo maskani yake ilikua Mwananyamala kwa Kopa,hapo ikapelekea waliobaki chini ya dogo Jack kuwapiga kijembe kwamba kichwa cha nyoka hakibebi mzigo!.
Lakini na wao waliohama chini ya utawala wa Aigoshi nao wakajibu kwenye bonge ya ngoma inaitwa "Tulipokuwepo kwenu"
 
Kuna nyimbo hisani Gari kubwa waliimba kama dongo kwa bendi nyingine, sijui jina la nyimbo ila inaanza kwa "walishindwa watu kweli wazazi wa majumbani, wenye kutoa Ukali na Radhi za midomoni," unaweza kunipa sababu Za wimbo huu kutungwa?
 
Back
Top Bottom