Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Milage na matunzo yake yako vipi. Kama ina kilomita zaidi ya 300,000 na haikuwa na matunzo mazuri huko nyuma basi tumia SAE 40 tu. Chini ya hapo bado nitakushauri utumie 10W-30 tu; in fact injini za 1G zilikuwa nzuri sana kuliko injini za magari madogo ya Toyota zilizofuata.
Ni zaidi ya 300,000 mkuu.Haikua na matunzo mazur! Je nikitumia 5w-30 nini kitatokea???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nina toyota duet 1999 huwa gauge yake ya mafuta unakuta ipo karibia bar moja sometime gari inazima licha ya kuonyesha bar moja ya mafuta tatizo ni nin?
 
Ni zaidi ya 300,000 mkuu.Haikua na matunzo mazur! Je nikitumia 5w-30 nini kitatokea???

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutokana na km ambazo imeshatembea na mwaka uliotengezwa ni dhahiri shahili kwamba baadhi ya vitu kwenye engine vimeshachoka sana hivyo vinahitaki kusaidiwa na oil nzito ili viweze kufanya kazi kwa ufasaha na hiyo 5w30 ni oil nyepesi na mahusisi hasa kwa hizi modern car ambazo bado hazijafikisha km 300,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasita kukupa jibu la moja kwa moja kwani bado naona uwezekano wa kuwepo kwa majibu mengi; ngoja tuanze na lile linalooneka kuwa na yamkini kubwa. Je ukishaanza kuendesha katika mwendo wa kawaida baadaye injini inarudi katika hali yake ya kawaida? Iwapo ni hivyo basi thermostat siyo mbaya ila inawezekana radiator yako ina kutu imeanza kuziba, kwa hiyo iwapo gari haitembei, upepo unaopuliza hautoshi kupooza injini mpaka uwe katika spidi ya kuvuta upepo mwingi. Je huwa unaweka maji ya bomba au maji yale ya kijani? Maji ya bomba huleta kutu haraka sana kwenye raditor. Mwambie fundi wako aikague radianto aone kama inahitaji kuflush. Vile vama gari ina feni ya umeme inawezekana fuse ya feni yako imekufa kwa hiyo feni haifanyi kazi kabisa ya kupuliza kwenye radiator yako, na kama feni inaendeshwa kwa mkanda, basi inawezekana mkanda umechoka; injini nyingi siku hizi hutumia feni za umeme, kagua fuse ya feni.
Nilibadilisha mfuniko wa rejeta na tatizo limeisha kabisa. Mfuniko ulikuwa umeisha so ukawa unaingiza hewa.
 
Nina vitz ya mwaka 2000 yenye cc 990 nirichukua kwa mtu ilikua inatumia lita 1 ya mafuta kwa km 5 nikapeleka kwa fundi gasket ilikua inavujisha oil inapeleka kwenye plug nikaweka mpya sasa hivi inakula lita 1 kwa km 8. Wakati kwa watu wengine wenye vitz kama yangu ni 1lita kwa km 12 kwenda juu hapo tatizo litakua ni no.
 
Nina vitz ya mwaka 2000 yenye cc 990 nirichukua kwa mtu ilikua inatumia lita 1 ya mafuta kwa km 5 nikapeleka kwa fundi gasket ilikua inavujisha oil inapeleka kwenye plug nikaweka mpya sasa hivi inakula lita 1 kwa km 8. Wakati kwa watu wengine wenye vitz kama yangu ni 1lita kwa km 12 kwenda juu hapo tatizo litakua ni nn?
 
Nina vitz ya mwaka 2000 yenye cc 990 nirichukua kwa mtu ilikua inatumia lita 1 ya mafuta kwa km 5 nikapeleka kwa fundi gasket ilikua inavujisha oil inapeleka kwenye plug nikaweka mpya sasa hivi inakula lita 1 kwa km 8. Wakati kwa watu wengine wenye vitz kama yangu ni 1lita kwa km 12 kwenda juu hapo tatizo litakua ni nn? Ukizingatia gari bado ni mpya ina mwaka 1 tangu iingia Tanzania.
 
IST kuna jamaa alikosea terminals za battery positive akaweka negative na kinyume chake. Baada ya kuwasha gari likawa haliwaki. Fundi akabadiri baadhi ya fuses zilizokuwa zimebuma na gari likawaka. Ila ukiwe park gear haitoki na ABS light zinawaka muda wote ingine inapokuwa on. Ili kuitoa gear shifter kwenye P inabidi kuponyeza button moja hivi ndiyo shifter inaweza kusogezwa kuto P. Ila kutembea na performance ya engine iko vizuri kabisa. Shida ni hiyo gear shift na ABS light inayowaka continuously kwenye dashboard! Tatizo ni nini hapa na tiba yake ikoje?
 
Mkuu Kichuguu,
Gari yangu ni ist. Niliagiza Japan ikiwa na millage 55,000km na sijawahi kubadilisha transmission fluid(oil ya gear box).

Sasa mafundi wengi wanasema oil ya gear box unatakiwa ubadili pale unapo badili oil ya enjini au kutembea 5000km.

Gari yangu inashida napo shift gear kutoka P hadi R au D. Nikishift kunatokea mshindo mkubwa. Yani nikishift kutoka P hadi D unasikia mshindo wa gear mkubwa, vilevile kutoka R hadi D.

Sijajua tatizo ninini, au napaswa kubadili Oil ya gear box?

Pili, nikiwa kwenye safari ndefu may be nishatembea kama 200km hivi naweza kanyaga mafuta mpk mwisho lkn speed ikasoma 80kmph. Mpaka pale nitakapo kanyaga taratibu na kuisubiri ichanganye yenyewe ndio itafika hata 150kmph. Je hapa tatizo ninni mkuu?
Sina wasiwasi na pump kwakua ina miezi 3 tangu itoke japan na haijawahi niishia mafuta kusema nimeua pump.
 
Gear box inahitaji service. Kwa kawaida mafuta ya gearbox hayabadilishwi mpaka baada ya urefu wa kama kuanzia km 50,000 hadi km 80,000 hivi kulingana na matumizi ya gari lenyewe. Ni kweli kwa gari iliyokwisha tumika, kwa vile ulikuwa hujui mtumiaji wake wa kwanza aliitumia vipi, ni vizuri kubadilish oil zote, yaani engine oil na ATF kabla ya kuanza kuitumia mwenyewe.

Tatizo unalosema hapo juu ni kweli kuwa mafuta ya transmission ama yamepungua sana au yamezidi sana. Sasa kwa vile hujawahi kuweka mafuta hayo, basi ni wazi kuwa yamepungua sana. Hata kama hayajapungua basi huenda filter yako imeziba kwa hiyo hairuhusu mafuta mengine kupita. Utakapobadilisha mafuta ya Transamission, hakikisha kuwa unabadili na filter, na vile vile kusafisha oil sump yake. Sump hiyo ina sumako ya kukusanya unga wa chuma unatokana na geara kusagana. Safisha ungao wote huo kabla ya kuweka mafuta mapaya na filter mpya. Wakati wa kubadili mafuta ya transamission, hakikisha unatumia mafundi wazuri wasije kukausha kabisa mafuta kwenye Torque converter au kuweka mafuta mengi zaidi ya kipimo na hivyo kusababisha matatizo makubwa zaidi.
 
Nina vitz ya mwaka 2000 yenye cc 990 nirichukua kwa mtu ilikua inatumia lita 1 ya mafuta kwa km 5 nikapeleka kwa fundi gasket ilikua inavujisha oil inapeleka kwenye plug nikaweka mpya sasa hivi inakula lita 1 kwa km 8. Wakati kwa watu wengine wenye vitz kama yangu ni 1lita kwa km 12 kwenda juu hapo tatizo litakua ni nn? Ukizingatia gari bado ni mpya ina mwaka 1 tangu iingia Tanzania.
Hiyo gari siyo mpya, ina umri wa miaka ya 20, kwa hiyo kuna matatizo mengi yanayoweza kusababisha ile mafuta mengi kuliko kiasi. Kwa maelezo yako, inawezekana kuwa injectros zako nazo zimechoka. au fuel pressure regulator imesihiwa nguvu. mwambie fundi wako avikague vitu hivyo.
 
IST kuna jamaa alikosea terminals za battery positive akaweka negative na kinyume chake. Baada ya kuwasha gari likawa haliwaki. Fundi akabadiri baadhi ya fuses zilizokuwa zimebuma na gari likawaka. Ila ukiwe park gear haitoki na ABS light zinawaka muda wote ingine inapokuwa on. Ili kuitoa gear shifter kwenye P inabidi kuponyeza button moja hivi ndiyo shifter inaweza kusogezwa kuto P. Ila kutembea na performance ya engine iko vizuri kabisa. Shida ni hiyo gear shift na ABS light inayowaka continuously kwenye dashboard! Tatizo ni nini hapa na tiba yake ikoje?
Kama ABS imekufa kwa kureverse voltage, sababu yake kubwa ni kuwa zile hall sensor za kwenye magurudumu zimeungua. na iwapo hizo hall sensor ziko OK, basi huenda solenoid za kwenye ABS box zimekufa. Tatizo la ABS kutokufanya kazi sawasawa siyo kubwa sana, wala haliathiri breki zako kutokufanya kazi, ila sasa ukishika breki za ghafla, gari linawezea kuteleza barabarani kama magari ya zamani ambayo hayakuwa na ABS. Kuhusu transmission, nadhani imelock. Kila gari ina njia zake za ku-unlock transmission. Ila kama fundi wako ana ile computer ya kufanyia scanning, basi anaweza kuitumia hiyo ku-unlock. Nji nyingine ambayo watu huweza kutumia ni kuondoa beteri kwa muda mrefu kidogo kama saa nzima au mbili, kusudi computer isahahu kila kitu na kuanza upya
 
Gear box inahitaji service. Kwa kawaida mafuta ya gearbox hayabadilishwi mpaka baada ya urefu wa kama kuanzia km 50,000 hadi km 80,000 hivi kulingana na matumizi ya gari lenyewe. Ni kweli kwa gari iliyokwisha tumika, kwa vile ulikuwa hujui mtumiaji wake wa kwanza aliitumia vipi, ni vizuri kubadilish oil zote, yaani engine oil na ATF kabla ya kuanza kuitumia mwenyewe.

Tatizo unalosema hapo juu ni kweli kuwa mafuta ya transmission ama yamepungua sana au yamezidi sana. Sasa kwa vile hujawahi kuweka mafuta hayo, basi ni wazi kuwa yamepungua sana. Hata kama hayajapungua basi huenda filter yako imeziba kwa hiyo hairuhusu mafuta mengine kupita. Utakapobadilisha mafuta ya Transamission, hakikisha kuwa unabadili na filter, na vile vile kusafisha oil sump yake. Sump hiyo ina sumako ya kukusanya unga wa chuma unatokana na geara kusagana. Safisha ungao wote huo kabla ya kuweka mafuta mapaya na filter mpya. Wakati wa kubadili mafuta ya transamission, hakikisha unatumia mafundi wazuri wasije kukausha kabisa mafuta kwenye Torque converter au kuweka mafuta mengi zaidi ya kipimo na hivyo kusababisha matatizo makubwa zaidi.

Sawa Mkuu,
Asante sana.
 
Pole na majukumu ya kila siku, gari yangu ilibadilishwa valve, saizi plug ya piston ya kwanza inachafuka na oli mda mwingine inachoma, mda mwingine haichomi, nikiwasha gari ahsubuhi linatoa moshi kama dakika moja ukikata hautoki tena mpaka kesho ahsubuhi ninapoliwasha ambapo huwaka kwa miss. Hapo shida itakuwa ni nini?

Mkuu Kichuguu
Kuna huyu jamaa nae ananichanganya baada ya kuomba ushauri kwenye uzi wake?

Maoni yako tafadhali

Ninj shida pale gari inakuwa inatoa mshindo unaposhift gear kutoka P hadi R au D? Unasikia mshindo mkubwa 'ndiii! Kina unaposhift hizo gera

Booster ya upepo inavunja na gearbox mounting imekufa

Jr
 
Mkuu Kichuguu
Kuna huyu jamaa nae ananichanganya baada ya kuomba ushauri kwenye uzi wake?

Maoni yako tafadhali
Nina leseni ya ufundi wa magarai ndugu yangu; hata kama huwa nakosea sehemu nyingine, kwa hili tatizo laki nakushauri ufuate ushauri wangu - badilisha mafuta ya transmission pamoja na oil filter yake, tena fanya haraka kabla gearbox haijaanza kuingia kwenye hali mbaya zaidi. Gearbox na engine mounting zikifa, ni kweli unapata pia backlash lakini siyo kwa jinsi ulivyoeleza. Vacuum booster haina uhusiano wowote na gearbox kabisa, hiyo ni kwa ajili ya breki tu.

ONYO: Kama gearbox imeshajichokea sana, ukibadilisha mafuta inaweza kufa zaidi isifanye kazi kabisa kwa vile zile clutch plates zimeshasagika sana, ila sasa zinafanya kazi kutokana na uchafu ulioko kwenye mafuta; na hivyo ukiweka mafuta mapya, zitakuwa zinateleza. Ndiyo ndiyo maana nilikushauri kuwa tafuta fundi mzuri, siyo kila fundi wa mtaani anaweza kushughulikia matatizo ya transmission.
 
Kama ABS imekufa kwa kureverse voltage, sababu yake kubwa ni kuwa zile hall sensor za kwenye magurudumu zimeungua. na iwapo hizo hall sensor ziko OK, basi huenda solenoid za kwenye ABS box zimekufa. Tatizo la ABS kutokufanya kazi sawasawa siyo kubwa sana, wala haliathiri breki zako kutokufanya kazi, ila sasa ukishika breki za ghafla, gari linawezea kuteleza barabarani kama magari ya zamani ambayo hayakuwa na ABS. Kuhusu transmission, nadhani imelock. Kila gari ina njia zake za ku-unlock transmission. Ila kama fundi wako ana ile computer ya kufanyia scanning, basi anaweza kuitumia hiyo ku-unlock. Nji nyingine ambayo watu huweza kutumia ni kuondoa beteri kwa muda mrefu kidogo kama saa nzima au mbili, kusudi computer isahahu kila kitu na kuanza upya
Okay mtaalam, nashukuru kwa maelekezo. Nitayafanyia kazi nione outcomes.
 
Pole na majukumu ya kila siku, gari yangu ilibadilishwa valve, saizi plug ya piston ya kwanza inachafuka na oli mda mwingine inachoma, mda mwingine haichomi, nikiwasha gari ahsubuhi linatoa moshi kama dakika moja ukikata hautoki tena mpaka kesho ahsubuhi ninapoliwasha ambapo huwaka kwa miss. Hapo shida itakuwa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ulibadilisha valve, inawezekana kuwa hukubadilisha "valve seat" ambayo ndizo inayoruhusu oil kuingia kwenye cylinder.
 
Back
Top Bottom