Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Hicho kisanga huwa kinanitokea na mm hasa nkiwa kwenye gia ndogo inalia kakakakaka nkikanyaga acc ila ukiachia ukakanyaga tena inapotea gar imeandikiwa 5w30 but huwa naweka 5w40 bcz huku mkoani ndio easy kuipata na engine ni 1kr-fe 1.0l
Kwa sababu oil huwa zinaexpire baada ya miaka mitano kwann ushindwe kuagiza oil carton moja utumiwe huko uliko ili kila ukienda services unachukua dumu lako unaweka siku zikiisha unaagiza tena na sidhan kama garama ya mzigo kutuma kwenda huko mikoani itagharimu zaidi ya 20000 na hapo utakua umeokoa vitu vingi sana kumbuka engine ndio moyo wa gari kuiwekea oil ambayo sio recommended kwake ni kuiua taratibu taratibu
 
Chief mm nikiweka 5w-30 huwa inapungua haraka sana kwenye ingine tatizo nn bora 5w40 engine 1kr-fe
Inategemeana na matumizi yako na ujazo wa gari unaweza kukuta gari inataka uiwekee oil litre 5 wewe ukanunua lt4 bila kuongezea litre moja unategemea nn kitokee mkuu? Na pia uzito wa hizo oil unatofautina kidog ndo maana unaona moja inapungua sana nyingine inachelewa ni sawa na kikombe kimoja cha chai na uji ukimwaga kwa pamoja kipi kitawah kumalizika?
 
Chief mm nikiweka 5w-30 huwa inapungua haraka sana kwenye ingine tatizo nn bora 5w40 engine 1kr-fe
Kagua gari huenda kuna leakage mahali...au huenda piston rings zimeisha ukute oil inapenya na kuingia kwenye combustion chamber...
 
Mkuu asante sana kwa darasa zuri.....mm nina gari aina ya vitz , mara nyingi huwa nikiendesha nasikia harufu ya mafuta ya petrol ndani ya gari. hii husababishwa na nini maana tanki la mafuta limefungwa vizuri halina shida ila harufu ya mafuta inaingia ndani.
 
Harufu ya mafuta ndani ya gari siyo jambo jema kwani upande wa pili wake unaweza kuunguza gari lako na hata kuchukua uhai wako.Kwa hili nitapenda nikusaidie kwa kukupa ushauri wa makini sana kwani ni jambo linaloweza kuwa la hatari sana. Hebu niambie, je gari lako linatumia kabyuretor au in EFI, halafu je linaonekana kula mafuta sana kwa mwendo mfupi tu? Matatizo ya kabyuretor na EFI yanatofautiana
 
Kinachoshauliwa kwenye gari tumia engine oil ambavyo iko recommended na watengenezaji hata kama gari itafikia km 300000 tumia oil iliyoshauliwa kinachobadilika hapa ni mda wa kumwaga oil tu kwa wakati na kuweka mpya: naomba nieleweke vizuri ni kumwaga oil na kuweka mpya na sio kuongezea oil maana kuna watu nawauzia oil hivyo hivyo ukimshauri amwage yey atakwambia imepungua kidog nataka ya kujazia tu hilo ni kosa kubwa sana unaua engine yako bila wewe mwenyewe kujijua
Nimekupata kiongozi, msaada hapa nmesoma engine oil inayotakiwa kwa engine husika ni kati ya hizi 5W-30, 10W-30, 15W-40, 20W-50 kwa hali ya hewa ya Iringa ushauri wako ipi ni muafaka zaidi?
 
Natumia gari rav4 oldmodel, kuna mlio unaitwa kiduku hasa kwenye magari mengi ya rav4 , mlio huu hutokea pale unapoweka gia kwenye D or R. Hulia mara moja tu. Shida ni nin
 
Nimekupata kiongozi, msaada hapa nmesoma engine oil inayotakiwa kwa engine husika ni kati ya hizi 5W-30, 10W-30, 15W-40, 20W-50 kwa hali ya hewa ya Iringa ushauri wako ipi ni muafaka zaidi?
Kwa hali ya hewa ya iringa ambayo kuna barid kiasi kulingana na mikoa ya hapa nchini oil ninayokushauri utumie ni 5w30 kwani inawah kuchanganya sana kwani ni nyepesi kuliko zingine zote hizo ulizotaja na hii bei yake imesimama kidog kulingana na kampuni unayotumia
 
Selonoidi ina kazi gani kwenye gari. Fundi kanambia imekufa, ila kashindwa kunipa maelezo ya kutosha.
 
Nimekupata kiongozi, msaada hapa nmesoma engine oil inayotakiwa kwa engine husika ni kati ya hizi 5W-30, 10W-30, 15W-40, 20W-50 kwa hali ya hewa ya Iringa ushauri wako ipi ni muafaka zaidi?
5W-30 au sana sana umeelemewa weka 10W-30; hizo nyingine mbili zitakuchakazia injini mapema.
 
Mkuu pole na kazi, Mimi natumia Toyota rav4, nilifanya overhaul apa majuzi lakin baada ya apo gari limekuwa na tabia ya kukata moto ninapokuwa kwenye mwendo mdogo, yaani inanilazimu nikanyage mafuta ya kutosha ili lisizime, hasa ninapoanza kuliwasha niondoke, sijajua tabia hii ya kukata moto imetokana na nini?
Mkuu hili tatizo na mimi limenitokea katika 5A engine ya gari langu. Mimi nilibadili piston rings, gasket na valve kwani fundi alichek piston akaona zipo vizuri. Baada ya kazi gari ikaanza tabia ya kuzima kila nikiweka D au R engine inapokuwa na joto ila ikipokea fresh mwendo na nguvu kwa kweli umeongezeka. Baada ya mizunguko ya kutafuta tiba nikaangukia kwa fundi umeme ambaye kabla ya kuanza kulipima gari akashauri tubadili vacuum ya presha pale juu ya engine. Hapo ndio ukawa mwisho wa hiyo shida ya kuzima kila nikiweka D au R kwani gari ikatulia na rpm zikawa hazidrop hadi kupelekea gari kuzima. Shida iliyobaki sasa ni gari kuzima ninapokata kona wakati gari imesimama na ipo katika D au R. Kama una tiba please share na mimi.
 
Natumia paso nliipeleka kwa fundi then nimerudi ila ikifika 100 inaanza kuvibrate usukani
 
Natumia paso nliipeleka kwa fundi then nimerudi ila ikifika 100 inaanza kuvibrate usukani
Sijui Paso zikoje, lakini gari yoyote ikiwa inavibrate usukani maana yake ni ama wheel alignment ni mbaya (peleka wakunyooshee wheel alignment angles) au steering stabilizer imechoka (badilisha weka mypa). Kama Paso haina steering stabilizer, basi wheel ni alignement tu, na kama ina stabilizer, huenda hata shock absorber nazo zitakuwa zinahitaji kubadilishwa kwani stabilizer na shock absrober zinachooka kwa kipindi kimoja.
 
Kabla ya hii 5w-40 ulikua unatumia oil gani?Na uliitumia kwa muda gani boss?
Muda wotw natumia 5w40 full synthetic huwa inapungua kwenye engine ilifika kuanzi km 1500 inabid nianze ongeza kidogo lkn nilisoma kwenye bonet nkaona nitafute 5w30 ambayo ndio recomended bas ikifika km 1000 ishapungua
 
Yaaezekana kuna sehemu oil inavuja
 
.... consumption ya mafuta?
Hiyo haifanywi na fundi, kila gari lina fuel consumption yake kulingana na design ya injini yenyewe toka kiwandani.
Makadirio kwa Toyota Hilux vigo 2500cc inaweza ku-consume fuel kwa kiwango gani? (Km/l)

Kuna moja inauzwa 27m nataka nione kama inawezekana.
 
57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom