Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Nimezunguka DSM.

Nimewaambia nahitaji 5W30 wamesema hawana.

Na nimeongeza search kwenye petrol station za Total kutafuta mbadala ila nako nimekosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribu 10W30 badala yake.

Vile vile nimeona tangazo hilo huko mitaani linaloonyesha kuwa zinapatikana

1576115084288.png
 
Kwangu Mimi kama muuzaji oil zinazotengenezwa na wauza mafuta mfano oryx, total, gp, na puma kwa maana ya castrol ndio oil bora ambazo zinafuata viwango vya kimataifa na wengi tutambue kwamba makampuni hayo makao makuu yake hayako hapa Tanzania hivyo chemical zake nyingi zinakua designed nje ya nchi na hapa wanakuja kuchanganya na kutoa kitu ambacho kimethibitishwa kama muuzaji wa oil ningependa watu watumie oil za makampuni hayo makubwa na kuachana na hizi oil ambazo zimejaa mtaani zijulikanazo kama za kupima ambazo ubora wake ni hafifu sana japokuwa zinatoka nje ya nchi
Wananchi hawawezi kukuelewa,wao wameshazoea kuweka SAE 40.

Na kupata 5w-30 mtaani huku si mchezo,mpk maduka fulani fulani tu ingawa mimi ni mtumiaji wa 5w-30.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu gari yangu toyota ist inatatizo la kukosa nguvu, inakosa speed kabisa na unaweza kanyaga accelerator mpaka mwisho isifike 120km/hr. Tatizo linaweza kuwa nini?
Kwa kiasi kikubwa tatizo lako ni fuel pump!
 
Guys gari yangu passo 3pistons, kuna taa inawaka mda flani then inapotea, ishatokea mara mbili. Taa ya check engine then OD ina flush ila mda flan ukizima gari ukawasha inapotea, juzi nligundua ikiwaka gia namba 2 iningia kwa kushtuka ila ilitokea maramoja tu. Nn shida wajuvi wa mambo

Ni taa ya namna gani; mara nyingi taa zinazowaka na kuzmika huwa ni za oil pressure sensor. Je unapata taa ya namna hii?
1576446320386.png
 
Gari inakula sana mafuta tatizo nini?Ni Suzuki escudo cc 1590 goldwin

Sent using Jamii Forums mobile app
Kula sana mafuta kunasababibishwa na vitu vingi sana; inabidi uweke dalili nyingine, kwa mfano inakula sana mafuta lakini haina nguvu, au inakula sana mafuta na inaleta harufu ya mafuta a kwenye cabin, au inakula sana mafuta na inatoa moshi mweusi
 
Kuna mazda Demio auto mara nyingine inagoma kubadili gear, mfano kutoka P kwenda D inakataa kabisaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaelekewa kwenye matatizo makubwa sana. Hebu kwanza angalia una mafuta (ATF) ya kutosha kwenye transmission, baada ya hapo angalia kama transmission filter ina hali nzuri. Kama kuna mafuta ya kutosha na filter ina hali nzuri basi transmission yako iko njiani kwenda makaburini
 
Kula sana mafuta kunasababibishwa na vitu vingi sana; inabidi uweke dalili nyingine, kwa mfano inakula sana mafuta lakini haina nguvu, au inakula sana mafuta na inaleta harufu ya mafuta a kwenye cabin, au inakula sana mafuta na inatoa moshi mweusi
Gari nguvu inayo,moshi mweusi haitoi isipokuwa nimeona Kuna taa nyekundu ya engine hii inaashiria nini,?Tatizo langu la gari kula mafuta limeanza ghafla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom