Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,539
- 19,389
- Thread starter
- #121
Nimejaribu leo kuingia chini ya gari ili kusikiliza ule mlio unaogonga unatokea wapi,nimegundua unatokea ndani ya oil sump.Niliwahi pia kumuuliza fundi mmoja akaniambia inawezekana chekeche la oil sump lina mauchafu kwahiyo oil inapita kwa shida wakati wa kuwasha gari kwahiyo ikipata moto inalainika na ule mlio ndio maana huwa unaacha,ushauri alionipa nikufungua na kuisafisha,hapo napo ni vipi mkuu?pia ulinishauri niangalie lile bati la juu ya exhause pipe kama limelegea,lile liko tight kabisa na nut zote ziko vizuri...
kwanza kabla sijakupa utaalamu wa muhimu zaidi, hebu niambie kwanza iwapo gari lako linatumia automatic transmission au ni stick shift transmission.
kama ni Automatic Transmission, litakuwa na oili sump mbili; moja kwa ajili ya injini, na nyingine kwa ajili ya gearbox, je unasikia sauti hizo kutoka sump ipi? Nina wasiwasi kuwa itakuwa inatoka kwenye sump ya gearbox; na hilo litakuwa siyo jambo jema kabisa.