Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,502
19,341
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.

Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through part-time activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu.

Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake, lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto-repair shop.

Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.

Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.

Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.
 
Engine check ya Harrier kuwaka bila hitilafu kwenye Engine. Nini la kufanya
Engine Check ikiwaka ni lazima kuwe na hitilafu fulani. Jibu sahihi litapatikana tu kwa kuinganshia na computer scanner kusoma code zake.

Kama gari inatembea vizuri wala haionyeshi hitilafu yoyote, basi sababu mojawapo ya engine light inaweza kuwa ni catalytic converter kwenye exhaust kuishiwa nguvu, haichuji gesi chafu kutoka kwenye Moshi wa exhaust sawasawa.

Kama hauendeshi kwenye barabara za California, hilo litakuwa siyo tatizo kubwa sana, ila sasa ujue gari yako inachafua mazingira sana. Hiyo ndiyo sababu inayoonekana mara kwa mara hasa gari likisha kuwa na umri wa kuanzia miaka minane.
 
Mkuu no kwanini inakuwa vigumu ku-overhaul engine za Suzuki Carry NA ukijaribu kufanya hivyo gari hawezi kabisa kutembea katika ule uimara wa awali.

Ahsante
Hi swali nilishawahi kulijibu katika thread nyingine. Overhaul ya engine yoyote kwanza huwa siyo jambo la lazima sana labda kama gari ilitumika vibaya bila kuwa na oil na coolant ikafikia kuunguza Crankshaft bearings na mpaka kuharibu pistons.

Overhaul yoyote hupunguza ubora injini hiyo kwa sababu huondoa genuine parts na kuweka OEM parts ambazo hazina ubora kama ule wa genuine parts. Mara nyingi overhaul huwa siyo ya lazima kwa sababu injini nyingi huchoka kwa kuharibika vitu vichache tu ambavyo zaidi ya Spark plugs na ignition coils, ni pamoja na oil seals, bearings, AC/Clutch, timing belt, valve lifters(tappets), fuel pump, timing belt, fuel filter, fuel pressure regulator, labda na sensors za injini kama air flow sensor, oxygen sensor, manifold absolute pressure sensor, throttle position sensor na sensor nyingenezo ambazo utazitambua kwa kupitisha injini yako kwenye computer scan. Vyote hivyo huweza kubadilishwa bila kufanya engine overhaul.

Matatizo ya kufanya Overhaul hasa unapofikia kubadilisha pistons ni kuwa mara nyingi piston unazoweza huwa hazina uzito sawa na zilie zilizokuwamo mwanzo, na hapo ndipo mwanzo wa matatizo ya injini kushindwa kazi, na tatizo hilo huwa ni kubwa zaidi iwapo utabadilisha piston chache tu na kuacha nyingine.

Tatizo jingine la overhaul ambalo ni rahisi sana kufanywa na mafundi wasiokuwa makini ni kukosea kidogo sana ile crank angle ya TDC na BDC. Ni pembe ndogo sana lakini inapokosewa basi nayo huleta matatizo makubwa katika utendaji wa injini yako. Kuna injini ambazo ni sensitive sana kwenye makosa hayo na kuna injini ambazo ni robust kiasi cha kuyahimili..

Mwisho ni vigumu kukupa jibu sahihi mpaka nikague injini yako, majibu hayo hpo juu ni yale ya jumla jumla tu.
 
Kuna uwezekano wa kufunga injini ya passo kwenye hilux ili isinywe mafuta
Nisikudanganye, jibu la swali hilo silijui ingawa pia naamini huenda haiwezekani kwa sababu nadhani injini hizo zina mounting zinazotofautiana. Kwa hiyo hata ukifanikiwa kufanya hivyo, unaweza kukuta unasababisha gari kuwa na vibrations sana.
 
Kichuguu,

Mkuu nina gari dogo la 1.5L, kwa kawaida likiwa idle mshale wa RPM unakua chini kidogo ya moja.

Leo nikiwa nimesimama kwenye foleni limenizimikia. Nikaliwasha likawaka na kuweza kuondoka bila shida yoyote.

Gari halikuwa lime-overheat, sikua nimewasha AC, tank lilikua chini kidogo tu ya nusu.

Level ya coolant, oil zote zipo sahihi na sehemu liliponizimikia ni tambarare. Tatizo linaweza kuwa nini? Maana kitu pekee nilichobadili hivi recently ni redio na nimenotice saa ya kwenye redio ilireset baada ya kutokea hivyo.
 
Engine Check ikiwaka ni lazima kuwe na hitilafu fulani. Jibu sahihi litapatikana tu kwa kuinganshia na computer scanner kusoma code zake.

Kama gari inatembea vizuri wala haionyeshi hitilafu yoyote, basi sababu mojawapo ya engine light inaweza kuwa ni catalytic converter kwenye exhaust kuishiwa nguvu, haichuji gesi chafu kutoka kwenye moshi wa exhaust sawasawa. Kama hauendeshi kwenye barabara za California, hilo litakuwa siyo tatizo kubwa sana, ila sasa ujue gari yako inachafua mazingira sana. Hiyo ndiyo sababu inayoonekana mara kwa mara hasa gari likisha kuwa na umri wa kuanzia miaka minane

Mkuu nadhani ungebenchmark in terms of milage ikaeleweka vizuri engine iwe imetembea kuanzia km ngapi ndo haswa tatizo huwa maarufu kuliko kiumri. kwasababu kuna Lililotembea km elfu 10 kwa miaka nane na lililotembea km laki na 20 kwa miaka nane tangu litoke kiwandani. Kwa scenario ya umri sidhani kama inaapply vizuri hapa.
 
Asante saaana kwa nafas hiyo. Mimi naomba unishauri nitumie oil gani ya engine na gearbox ambapo gari ni Toyota Premio yenye cc 1490 ya mwaka 2005 na mpaka sasa imetembea jumla ya km 71,179 na hiyo oil nibadili kila baada ya km ngap kwan wapo wanaoshaur km 3000 na km5000!!

Pia naomba unijuze ipi oil nzur kati ya Total na Castrol ambapo mm ni mkaazi wa mkoani mbeya ambapo hali ya hewa huku n baridi.

Asante boss!
 
Asante saaana kwa nafas hiyo,,mimi naomba unishauri nitumie oil gan ya engine na gearbox ambapo gar ni toyota premio yenye cc 1490 ya mwaka 2005 na mpaka sasa imetembea jumla ya km 71,179 na hiyo oil nibadili kila baada ya km ngap kwan wapo wanaoshaur km 3000 na km5000!!
Pia naomba unijuze ipi oil nzur kati ya Total na Castrol ambapo mm ni mkaazi wa mkoani mbeya ambapo hali ya hewa huku n barid.
Asante Boss
Mwenye uzi yupo lunch....
Me nakushauri tumia Total Quartz 9000 5w 30 au 10W 30 au 5W 40 kwa mqzingira ya Mbeya na umri wa gari siyo mbaya...

Ila zaidi tumia 5W 30... Hii kama umefunga oil filter genuine unaweza kwenda mpaka km 8000.
Castro ni nzuri sema zina soko sana hivyo kuna feki...kuwa makini..
 
Suzuki Swift inawaka taa ya EPS kwenye dashboard halafu usukani unakuwa mgumu, mafundi wangu wameshindwa kutengeneza utansaidiaje kwa hilo mkuu.
Aisee...
Electric Power Steering....EPS...
Brother kwenye gari kuna vitu unaweza kuvipuuza kwa muda lakini si EPS, Taa ya oil na Taa ya Temperature..

Hiyo EPS nenda kafanye vipimo...please usipige ramli hapo...hicho ni kifo cha faster...

Gari nyingi hata zikiwa na Low voltage ,EPS huzingua.
 
Back
Top Bottom