Niulize chochote kuhusu biashara ya mahindi na milling kwa ujumla

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,486
2,332
Niko kwenye hii biashara kwa zaidi ya miaka 7 sasa, kwa wale wanaopenda kujua ABC karibuni kwa maswali.

1622103882260.png

 
Niambie cost za uwekezaji na mashine ya kampuni gani zinafaa kwenye uwekezaji )Brand
Cost za uwekezaji zinapishana hasa kama unakodi jengo au kama jengo ni lako, lina umeme wa 3phase au halina. Ila gharama za mashine na vifaa vingine vinavyokwenda sambamba na ufungaji wa hizo mashine (kinu kimoja cha kusaga na kimoja cha kukoboa) haitazidi 8m kwa kinu cha kusaga no. 75 na kinu cha kukoboa roller 4 au 5. Mashine nzuri tumia watu wa sido wanajitahidi kuunda mashine imara.
 
1. Mtaji wa kuanzia ni sh ngapi?
2. Soko lake likoje?
3. Faida yake ikoje?
Kwa kiasi cha mtaji inategemea na mahali ulipo na aina ya mashine unazotaka kuweka. Mfano: tukiangalia mtaji wa cash yaani current assets kwa mtu aliyeko dar itakuwa tofauti na mtu aliyeko sumbawanga. Kwanini? Aliyek sumbawanga kwa kuwa amezungukwa na mahindi kila mahali hata mtaji wa 3m unaweza kumtosha kwa kuwa upatikanaji wa malighafi sio tatizo ila kwa aliye dar 3m ni kama unacheza tu.

Ila kwa kufunga mshine
Cost za uwekezaji zinapishana hasa kama unakodi jengo au kama jengo ni lako, lina umeme wa 3phase au halina. Ila gharama za mashine na vifaa vingine vinavyokwenda sambamba na ufungaji wa hizo mashine (kinu kimoja cha kusaga na kimoja cha kukoboa) haitazidi 8m kwa kinu cha kusaga no. 75 na kinu cha kukoboa roller 4 au 5. Mashine nzuri tumia watu wa sido wanajitahidi kuunda mashine imara.

Quote
 
1. Mtaji wa kuanzia ni sh ngapi?
2. Soko lake likoje?
3. Faida yake ikoje?
Kuhusu soko ni upambanaji wako watu wanakula kila siku mzee. Faida ipo ila inapishana kutokana na upatikanaji wa mahindi ulivyo katika kipindi husika
 
Vipi kuhusu usajili napita wapi na wapi mpaka nianze kusambaza unga Kama ltd company? Masoko yakoje?
 
Vipi kuhusu usajili napita wapi na wapi mpaka nianze kusambaza unga Kama ltd company? Masoko yakoje?
Limited co. Unaweza kusajili brela online, kisha baada ya hapo ukaenda tra ukapewa tini kisha leseni katika halmashauri husika. Kibali cha jengo na ukaguzi wa jengo ofisi ya afya ya halmashauri husika watakusaidia na kibali cha usalama wa bidhaa yako kilichokuwa kinatolewa na tfda siku hizi utakipata tbs, hapa bwana afya wa halmashauri uliyopo atakusaidia kukupa muongozo mzuri. Masoko ni mtaji wako na upambanaji wako tu
 
Uzi murua sana! Naomba kujua kwa mwenye kutaka kuanza ni lazima uanze kwa kuwa na mashine au waweza kusaga/kukoboa kwa mtu na wewe ukawa unasambaza unga kama kawaida.. vipi kuhusu faida ikiwa unatumia mashine za watu wengine?
 
Ukiwa na tani moja ya mahindi unapata unga wa sembe kiasi gani
Kwa unga wa kawaida unapata kilo 700, unga mkali 650. Ila pia itategemeana na aina ya mahindi uliyopata. Kuna mahindi fulani huwa ni makubwa na bapa, aina hii ni kilio katika ukoboaji. Mahindi mazuri ni yale ambayo yanakuwa na umbile dogo na yenye uzito
 
Uzi murua sana! naomba kujua kwa mwenye kutaka kuanza ni lazima uanze kwa kuwa na mashine au waweza kusaga/kukoboa kwa mtu na wewe ukawa unasambaza unga kama kawaida.. vipi kuhusu faida ikiwa unatumia mashine za watu wengine?
Si wote wanaosaga na kusambaza unga wana mashine zao. Unaweza anza kwa kutumia mashine za watu. Bei ya kusaga na kukoboa gunia itategemea na mahali ulipo. Kikubwa tafuta mashine wanayosaga vizuri then unaweza kuchonga nembo yako.

Faida inapatikana kikubwa ni kutengeneza mzunguko na unapoanza usiwe na haraka na uwe na uvumilivu kwa kuwa kuna brand unakuwa umezikuta sokoni.
 
Nipo DSM mkuu
Biashara ya chakula ni watu, Dar ni mahali pazuri. Unaweza kupata jengo la gharama nafuu? Hii biashara ni nzuri kama unaweza kuwa na jengo lako au la kupanga lenye gharama nafuu. Ukipata la gharama kubwa basi hakikisha una mtaji mkubwa wa kutosha.
 
Back
Top Bottom