Niulize chochote kuhusiana na biashara ya duka la jumla

Wholesale Shop
FB_IMG_1622486656077.jpg
 
Bei za kuuzia unapangaje ?
Au unaangalia wenzio wanauza vipi ?
ukiwa mgeni kwenye biashara swala la kupanga bei halitokuchua muda kulielewa


Kwanza utaangalia wenzako wanauzaje bidhaa

Pia: sehemu unayoenda chukua mzigo watakusaidiaa jinsi ya kupanga bei
 
Maduka yamegawanyika kwenye makundi mengi


Kuna maduka yanauza jumla tu

Kuna maduka yanauza jumla na rejareja

Kuna maduka yanauza rejareja
 
Kwa uhitaji wa lotion za Amara, Nivea bidhaa za nywele Kama Dexe color shampoo, miadi, TCB na Eco gel utapata.

Karibuni
Screenshot_20210528-203310.png
 
Moja kwa moja twende kwenye mada

Kama unamalemgo yakufua biashara ya duka hii jumla achana na haya maduka ya mtaania ya Mangi nazungumzia biashara ya jumla mfano pipi, Tambi, Unga, Mafuta,sabuni,nk...

Karibu nipo tayari kushare my experience yangu kwenye hii biashara nayafahamu mengi zaidi na zaidi kwenye hi biashara...

Bidhaa nyingi zinapatikana kwenye viwanda ndipo wanapo nunua hawa matajiri nakuweka kwenye maduka yao ya Jumla

Almost asilimia 98% zinazalishwa hapa hapa Nchini.

Unga wa sembe,unga wa ngano Mfuta yakupikia, Pempers, Sabuni Soft aina zote, chumvi, biscuits, Tomato,majani ya chai,madaftari Aina zote marapa sabauni za unga Aina zote vibiriti nk...

Chamsingi nikuangalia bidhaa zipi utaanza nazo kutokana na mataji wako.

Hebu tuelezee jinsi unavyoweka rekodi ya mauzo na kuhakikisha kila kitu kinakuwa kwenye order na jinsi unavojua hapa nimepata hasara kwa kitu fulan au faida na mambo mengine ambayo hatuyajui. Manake hiyo kitu ndo inanichanganya sana nikifikiria kuanza biashara
 
Hebu tuelezee jinsi unavyoweka rekodi ya mauzo na kuhakikisha kila kitu kinakuwa kwenye order na jinsi unavojua hapa nimepata hasara kwa kitu fulan au faida na mambo mengine ambayo hatuyajui. Manake hiyo kitu ndo inanichanganya sana nikifikiria kuanza biashara
Swali zuri Sana

Kwanza kabisa duka lako unatakiwa kuli-manage unatakiwa kuwa na list nzima ya bidhaa unazotaka kuziuza : unaweza kutumia Software kwenye kutunza kumbuka kumbu au Daftar....


Mfano umeingiza mzigo


1 Tomato souce dozen 10

2 Chumvi kubwa dozen 15 ndogo dozen 10

3 Sabuni White wosh dozen 15

4 Big G Gomba dozen 5

5 Pipi kijiti dozen 5

6 Biscuits chocolate dozen 10

7 Biscuits Maziwa dozen 7

8 vibiriti dozen 10

9 Sembe viroba 50


Ukiuza kwa siku unaandika record

Mfano

Tomato dozen 1 au 3

Biscuits chocolate dozen 2 au 4

Chumvi kubwa dozen 3

Vibiriti dozen 2

Sembe viroba 12



Kwahiyo hii itakusaidia kujua kwa siku umeuza bidhaa ngapi na faida kwa siku pia utaijua


Store pia utajua bidhaa fran imebakia ngapi



Ili uweze kujua faida ulipata kwa siku na rahisi mfano Tomato ulinunua dozen elf 11,000 na wewe ukauza dozen moja elf 15,000 ujue faida yako hapo elf 4,000


Mfano biscuits chocolate dozen ulinunua dozen 13000 ukauza elf 16000 ujuee faida yako elf 3,000

Mfano Sembe ulinunua mfuko 15500 na ukauza 17500 ujue faida yako kila mfuko elf 2000 kwa mifuko 12 jumla 2,4000


So kwa mifano hiyo I hope umenielewa mkuu?
 
Back
Top Bottom